DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Hii tetesi itazaa taharuki kubwa sana, kwa vyanzo vya uhakika vitakapo sema ndio itakuwa taarifa rasmi. Iko hivi
👇

Ndizi Mbichi zikiwasili DSM zikiwa mikononi mwa wawekezaji wa biashara hio huvundika kwa namna ya kuchovya kwenye maji yaliyowekwa vimiminika (chemicali) na hivyo ndizi kuiva ndani ya siku 2 masaa 48, japo wenyewe hao wahuni husema ndizi inaiva ndani siku 4 wakati hizo siku 4 ni utamaduni alisia wa ndizi kuiva kwa siku 4.

Hao wahuni inasemekana hutumia liquid za ethene na oxygen (not sure) mtajua wenyewe.

Na hapa Pro. Janabi ajitokeze kukemea na kusema kuhusu madhara ya huo uuaji.

Nasisitiza hii ni tetesi, japo ninayo video ya mwandishi aliyefanya utafiti na mahojiano na wahusika sipaswi kuweka hadi pale itakapokuwa viral na moderators wenyewe wataweka pasipo shaka.

Hii ndio mixer (Acetylene+ Calcium carbide+ water)

Chukua tahadhari ya dhati kabisa.

Kufa kufaana ndio uninja wa Waafrika.

Wadiz
 
Duh nimeshajifia kudadeki kila siku lazima nile ndizi 5 za kuiva ni ratiba yangu..

Sometimes nahisi kama ndizi ninazokula zina harufu ambazo sio ya kawaida kama dawa au something; ninachofanya huwa nabadili genge tu.

Dah..
 
Siyo Dar pekee. Kuna binti aliwahi nisimulia kwamba ndicho walichokuwa wanakifanya huko Sumbawanga.

Boss wake ambaye ndo alikuwa na store, ilikuwa akishapata ndizi mbivu tokea Mbeya, alikuwa anazichovya kwenye dawa, then after a day anawauzia wale wamama wenye mabeseni na vibanda vya rejareja. Miaka kama 6 hivi iliyopita.

Kama hili lilitokea Swax, vipi DAR?
 
Ndizi inavundikwa na joto kama inkubeta wanavyofanya ,mambo ya kuweka kemikali ni uzushi....

Ndizi mbichi hata ukiiweka ndani tu ndani ya siku tatu inaiva yenyewe siyo mpaka mashine ,kwenye viwanda wanaongeza joto ili iive kwa uharaka.
 
Ndio maana kila siku nawaambia acheni kujistress kupoteza pesa zenu kulipia watoto wenu shule za English Mediums.

HAYA sasa twende kazi. Kimbia haraka sana kamchukue mtoto wako kwenye hiyo shule ya English Medium kisha mpeleke Kayumba. THANK ME LATER.

ANYWAYS: DAWA NI KUCHUKUA NDIZI MBICHI NA KUZIVUNDIKA MWENYEWE NYUMBANI.
 
Kuna muuza genge aliniambia chukua hizi za kijani hizo mnazopenda zinaivishwa kwa chemical kwenye freezers.
hii pia nimewahi kuisikia ndizi mbivu kuivishwa kwenye containers, na unaweza kula ndizi kwa nje inaonekana imeiva vizuri lakini ukiila ina ukakasi.

 
Back
Top Bottom