DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu, mambo ni mengi saana sisi huku kwetu Kilombero kuna watu wanaivisha ndizi ndani ya siku moja tena kwa kutumia moshi tu ila sasa kiungulia chake dah.

Na kwa dunia ya sasa, kukwepa magonjwa ni shida saana sio kijijini sio mjini.

Mwezi uliopita nimefika kijijini nikakuta wanakijiji wote kwa sasa ambao ni wafugaji wanawachoma ng'ombe sindano ya booster ili ndani ya miezi mitatu tu anatoka umri wa ndama hadi dume kweli kweli na anauza hadi mil+ ng'ombe ambaye bei halisi ni laki mbili na nusu lakini wakanidokeza sio booster tu hadi ARV Wanalishwa daaah!

Njoo kwenye kuku sasaa ni madawa matupu.

Kwenye samaki niliwahi kufika kwenye kisiwa moja kinaitwa REMBA ni karibu na kisiwa cha Migingo (nadhani au ndio hiyo wenyeji watanirekebisha) nilioyashuhudia pale ni hatari. Kuna wavuvi wasio waaminifu hutumia kemikali kuvua samaki.

Kwenye mboga za majani napo siku hizi bila madawa hutoboi. Sisi enzi hizo wazee walikuwa wanaweka tu majivu kwenye mboga na mamb yanaenda fresh ila siku hizi dah.

So, hatuna pa kukimbilia.
 
hiyo kemikali ya ethene huzalishwa pia kwa njia ya asili na mimea husika ila kusaidia uivaji wa matunda yake,....

Nina mashaka na wanaosema uongo,.. wakati tunayajua vizuri tu hayo mambo,...

kwasasa ujasiliamali umeharibu sana mifumo,... mfano kwasasa migomba na mihogo vyote vinawekwa mbolea huko mashambani,....

Kuku vibudu hawatupwi,....dawa za maiti zinatumika buchani kutunzia nyama isioze,..
🥱
 
SIo kweli.

Kuna jamaa Ubungo maziwa pale ana mashine kupuliza joto kafunga kwenye kontena anavundika ukipeleka ziko mbichi unapigiwa hesabu kesho yake unaenda chukua mbivu zako.

Hakuna cha dawa wala nini, nimeshuhudia kwa macho yangu anavyofanya
Aisee afadhali maana taarifa tunapata kwa watu wasio na elimu.
 
Hujajibu swali kajitatakia kivipi? Unaweza kusema watu wasinywe juisi za madukani, wasile mbivu za sokoni,Je mchele, nyama, samaki ,maharage, unga, maziwa ambavyo na wewe pia pengine unatumia una uhakika viko salama?
Siwezi kushauri watu kutokunywa wala kula, kila kiuzwacho na kina leseni ya SErikali tumia.

1. Shisha- vuta maana wanaovutisha wana leseni.
2. K-Vant- kunywa uwezavyo, wana leseni na inalipa kodi.
3. Kuchepuka na mume wa mtu- nenda kapigwe mashine, so long as upo juu ya 18 years.
4. Kitimoto.
 
Huku mwakaleli tunakula ndizi za asili kabisa hazina madawa Wala mbegu za kisasa, poleni mliopo mjini
Ahsante, umenitajia MWAKALELI, day, mji wangu huo. Nilifika huko kununua viazi, nimekaa Sana Kijiji Cha ntokela, ndaga na hapo KATUMBA. Vipi ile barabara kutokea katumba mpk mlima Suma mpk MWAKALELI, imewekwa lami? Lakini huko MWAKALELI dah! Nyumba Banda la nguruwe, nyumba Banda la nguruwe, aisee nilipata taabu Sana.

Nami nilivyo muislamu thabiti, ilikuwa nikikaa kijiweni na fimbo yangu mkononi. Kazi yangu ni kuzitandika tu, Nguruwe zinapita pita mpk kwenye miguu ya watu, mara limeparaza mgongoni, miguuni, ukijisahau mara limekuramba miguu, dah!
 
Duh..nchi zetu hizi ni changamoto hakuna anayejali jamani..
Yoga na Shangazi zake watakuja kuwashambulia hapa kwa kasi ya SGR utadhani ni mawakala wa huu ushetani ilimradi tu Watu wajipakie makemikali kisha wawe na kansa, waue maini, figo na kuzeeka mapema. Kweli dunia ni uwanja wa fujo.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Nimeona hii ikifanyika almost miaka mitatu sasa ...karibu na Sabasaba(Dar) kuna sehemu huwa naenda kupokea mizigo yangu
Niliacha kula ndizi ambazo sijui source
Bahati nzuri nina migomba ya kutosha
Tangu 2012 sijawahi kula matikiti ya kipumbavu ambayo kila siku yapo mitaani wala hayana msimu, ila Mwanza na baadhi ya mikoa kanda ya ziwa yapo yenyewe ya kijani halisi kabisa.

Ngoja niendelee kujirundikia matunda, mazao na mimea ya asili huku porini kwangu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Tangu 2012 sijawahi kula matikiti ya kipumbavu ambayo kila siku yapo mitaani wala hayana msimu, ila Mwanza na baadhi ya mikoa kanda ya ziwa yapo yenyewe ya kijani halisi kabisa.

Ngoja niendelee kujirundikia matunda, mazao na mimea ya asili huku porini kwangu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Ya kijani alafu ya mviringo hivi, yale ya asili, wacha vijana waendeleee kulalamika nguvu za kiume.

Mtu raundi ya kwanza hawezi kurudia tena mpaka wiki iishe.

Wanawake wanaoolewa miaka hii kati ya 10 mmoja tu ndio amefikishwa kileleni.
 
Back
Top Bottom