DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ndizi inavundikwa na joto kama inkubeta wanavyofanya ,mambo ya kuweka kemikali ni uzushi....

Ndizi mbichi hata ukiiweka ndani tu ndani ya siku tatu inaiva yenyewe siyo mpaka mashine ,kwenye viwanda wanaongeza joto ili iive kwa uharaka.
Too good wala hawaweki joto, bali baridi. Maana containers zenyewr tayari zina joto. Containers zimefungwa ma freezer kwa ajili ya kuset baridi around 15°C inside na ndizi huiva siku 4 mpaka 6.

Dawa inayowekwa kwenye maji kazi yake ni kuzipa ndizi rangi ya kuvutia. Rangi ya manjano iliyokolea imvutie mlaji wala si dawa ya kuivisha ndizi. Na dawa hiyo unaweza iweka hata wewe unayeivisha ndizi kwenye mtungi wako nyumbani. Unamwagia au kuchovya tu kichana then unaacha hapo. Wala haina madhara yoyote kwa sababu dawa ile haipenyi kuingia ndani ya chakula ndani.
 
Hii tetesi itazaa taharuki kubwa sana, kwa vyanzo vya uhakika vitakapo sema ndio itakuwa taarifa rasmi. Iko hivi
👇

Ndizi Mbichi zikiwasili DSM zikiwa mikononi mwa wawekezaji wa biashara hio huvundika kwa namna ya kuchovya kwenye maji yaliyowekwa vimiminika (chemicali) na hivyo ndizi kuiva ndani ya siku 2 masaa 48, japo wenyewe hao wahuni husema ndizi inaiva ndani siku 4 wakati hizo siku 4 ni utamaduni alisia wa ndizi kuiva kwa siku 4.

Hao wahuni inasemekana hutumia liquid za ethene na oxygen (not sure) mtajua wenyewe.

Na hapa Pro. Janabi ajitokeze kukemea na kusema kuhusu madhara ya huo uuaji.

Nasisitiza hii ni tetesi, japo ninayo video ya mwandishi aliyefanya utafiti na mahojiano na wahusika sipaswi kuweka hadi pale itakapokuwa viral na moderators wenyewe wataweka pasipo shaka.

Hii ndio mixer (Acetylene+ Calcium carbide+ water)

Chukua tahadhari ya dhati kabisa.

Kufa kufaana ndio uninja wa Waafrika.

Wadiz
🙋‍♂️🙄🤔😳
 
Kuna muuza genge aliniambia chukua hizi za kijani hizo mnazopenda zinaivishwa kwa chemical kwenye freezers.
Yeah zile zinazoiva zikiwa na ukijani ndio natural. Zinaiva kiasili ila za mashine ukiziangalia kwenye tip ya chini ya ndizi lazma kuwe na greenish. Japo juu inaonekana ya njano na ganda safi sana halina hata vidoti vyeusi.
 
Maisha magumu hivi lakini bado mnataka kuendelea kuyaishi? Mi nilikuwa na mpango wa kuchoma Quran tuchapane, wenzangu bado manatafakari kuishi maisha marefu, kwa usawa huu?
 
Mkuu, mambo ni mengi saana sisi huku kwetu Kilombero kuna watu wanaivisha ndizi ndani ya siku moja tena kwa kutumia moshi tu ila sasa kiungulia chake dah.

Na kwa dunia ya sasa, kukwepa magonjwa ni shida saana sio kijijini sio mjini.

Mwezi uliopita nimefika kijijini nikakuta wanakijiji wote kwa sasa ambao ni wafugaji wanawachoma ng'ombe sindano ya booster ili ndani ya miezi mitatu tu anatoka umri wa ndama hadi dume kweli kweli na anauza hadi mil+ ng'ombe ambaye bei halisi ni laki mbili na nusu lakini wakanidokeza sio booster tu hadi ARV Wanalishwa daaah!

Njoo kwenye kuku sasaa ni madawa matupu.

Kwenye samaki niliwahi kufika kwenye kisiwa moja kinaitwa REMBA ni karibu na kisiwa cha Migingo (nadhani au ndio hiyo wenyeji watanirekebisha) nilioyashuhudia pale ni hatari. Kuna wavuvi wasio waaminifu hutumia kemikali kuvua samaki.

Kwenye mboga za majani napo siku hizi bila madawa hutoboi. Sisi enzi hizo wazee walikuwa wanaweka tu majivu kwenye mboga na mamb yanaenda fresh ila siku hizi dah.

So, hatuna pa kukimbilia.
Ishu si ni ushindani wa biashara na kutafta utajiri wa haraka. Ila tume compromise wenyewe kwa kukumbatia sayansi ya GMO kwenye kila kitu na uzuri wote itatumaliza tu bila kujali mmiliki wa kiwanda na mtumiaji.

Tulitakiwa tuikatae hii ila kwa sasa afya zetu ziko rehani tena kwenye nchi zetu za kifedhuli hizi ambapo sheria inafanya kazi kwa wasio na pesa tu hali ni ya hatari sana. TBS na TFDA wamewekwa mfukoni na wenye chochote kitu.
 
Watu wanadanganyana sana kwenye vijiwe vya kahawa ,wanashindwa kujua ukichukua ndizi mbichi ukaiweka tu ndani bila hata kuifunika haichukui siku tatu ishaiva sasa ya nini uitose kwenye kemikali ,halafu ndizi kweli uiloweke kwenye kemikali ikitoka itakuwa salama? Si itakuwa nyonde nyonde na si kavu kabisa...ndizi ikiwekwa kwenye friji kama wanavyosema inakuwa nyeusi tiii sasa hawa wauza kahawa wanakwambia zinawekwa kwenye friza.
Mjini kuna mengi usibishe bali chunguza, embe, maharage, chungwa,Mtindi, ugali tunaukula hapo kwa mama ntilie vyote hivyo hakuna anayevileta kwa mlaji kwa hualisia wake, vinakuwa vimefanyiwa makaratee kibao.
 
Hii tetesi itazaa taharuki kubwa sana, kwa vyanzo vya uhakika vitakapo sema ndio itakuwa taarifa rasmi. Iko hivi
👇

Ndizi Mbichi zikiwasili DSM zikiwa mikononi mwa wawekezaji wa biashara hio huvundika kwa namna ya kuchovya kwenye maji yaliyowekwa vimiminika (chemicali) na hivyo ndizi kuiva ndani ya siku 2 masaa 48, japo wenyewe hao wahuni husema ndizi inaiva ndani siku 4 wakati hizo siku 4 ni utamaduni alisia wa ndizi kuiva kwa siku 4.

Hao wahuni inasemekana hutumia liquid za ethene na oxygen (not sure) mtajua wenyewe.

Na hapa Pro. Janabi ajitokeze kukemea na kusema kuhusu madhara ya huo uuaji.

Nasisitiza hii ni tetesi, japo ninayo video ya mwandishi aliyefanya utafiti na mahojiano na wahusika sipaswi kuweka hadi pale itakapokuwa viral na moderators wenyewe wataweka pasipo shaka.

Hii ndio mixer (Acetylene+ Calcium carbide+ water)

Chukua tahadhari ya dhati kabisa.

Kufa kufaana ndio uninja wa Waafrika.

Wadiz
Kuna Watanzania wenzetu ni mashetani haswaa.

Hawa unaweza kuwakuta ndo wale wanaofanya uchawa kwa kulinda shughuli zao haramu
 
Ishu si ni ushindani wa biashara na kutafta utajiri wa haraka. Ila tume compromise wenyewe kwa kukumbatia sayansi ya GMO kwenye kila kitu na uzuri wote itatumaliza tu bila kujali mmiliki wa kiwanda na mtumiaji.

Tulitakiwa tuikatae hii ila kwa sasa afya zetu ziko rehani tena kwenye nchi zetu za kifedhuli hizi ambapo sheria inafanya kazi kwa wasio na pesa tu hali ni ya hatari sana. TBS na TFDA wamewekwa mfukoni na wenye chochote kitu.
Hakika umenena vyema maana kama tuna tbs na TFDA lakini bidhaa na vitu tunavyotumia kila siku hata mtu ambaye amemaliza la nne akiupa ubongo wake kazi ya kufikiri anagundua kabsa tunapigwa
 
Too good wala hawaweki joto, bali baridi. Maana containers zenyewr tayari zina joto. Containers zimefungwa ma freezer kwa ajili ya kuset baridi around 15°C inside na ndizi huiva siku 4 mpaka 6.

Dawa inayowekwa kwenye maji kazi yake ni kuzipa ndizi rangi ya kuvutia. Rangi ya manjano iliyokolea imvutie mlaji wala si dawa ya kuivisha ndizi. Na dawa hiyo unaweza iweka hata wewe unayeivisha ndizi kwenye mtungi wako nyumbani. Unamwagia au kuchovya tu kichana then unaacha hapo. Wala haina madhara yoyote kwa sababu dawa ile haipenyi kuingia ndani ya chakula ndani.
Aiseeee noma sana.
 
Back
Top Bottom