Interlacustrine R
JF-Expert Member
- Jan 22, 2022
- 7,186
- 14,274
Kama Watu wanathubutu kukaangia chipsi mafuta ya transformers, unadhani hao ni Binadamu halisi?Dsm ni hatari.
Kuna siku nilipita soko la Makumbusho vibanda vya kuku. Nikakuta muuzaji na mwenzake (alijifanya msaidizi wa muuzaji), huyo mwenzake anamalizia kupakia kwenye mfuko kuku kadhaa walioandaliwa. Nikataka wanichinjie kuku wawili toka bandani. Yule mwenzake akadakia "bro si tungepunguza toka kwenye oda ya huyu ninayemfungia ili tusikucheleweshe? Ntabaki na-replace tu coz ninayempelekea hana haraka."
Nikasema poa. Jamaa akaenda kunichukulia mfuko ili achomoe wawili aniwekee. Yule jamaa aliyebaki akaniambia "bro, unaonekana mstaarabu, nafsi inanisuta, acha nikwambie ukweli. Huyo jamaa si muuzaji wangu bali huwa anapita kukusanya kwa bei chee kuku waliokufa hapa sokoni au wakati wa usafirishaji, anaenda kuwauzia wauza chips na mama ntilie kwa bei ndogo. Chagua tu bandani tu uchinjiwe."
Aisee nilichoka. Na hamu ya kuku ikaisha. Nikamwambia basi bro, nikampoza kidogo. Jamaa wakati anarudi na mfuko akaniona naondoka, nikamjibu sihitaji tena, wife kanipigia alishanunua mahali so mpelekee tu jamaa oda yake.
Muuzaji aliniambia wako wengi wanapita kukusanya. Hakuna soko kuku waliokufa wanatupwa.
Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
