DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mhhhh, kuna siku nilinunua yale maembe maboribo ya kukata, yameiva vizuri tu lkn yalikuwa machachu hatari hakuna aloyaweza kuyala. Siku hizi mambo ni mengi kwa kweli, zamani hatukuyaona haya, matunda mengine mengine yanaiva na mengine kufikia kuoza mtini.
umenikumbusha matunda kuivia sambani. Yaani unaingia shamban unasikia harufu ya ndizi mbivu unaitafta mpaka unaipata. Hizi ndizi tunanunua gengeni hata harufu nzuri huisikii
 
Mwezi uliopita nimekunywa maji ya kopo hapa Dar yana chumvi kama ya kisimani.

Ni ya kampuni moja kubwa tu! Wachakachuaji wapo kila sehemu
Unashangaa chumvi kwenye maji ila kuingia uvinza aah!
 
Huku kijijini kwetu niliwahi kusikia kuwa wanachimba mashimo na kuzifukia chini,sasa kwa huko mijini kwenu mwendo wa vi pavements sijui wanachimba wapi...
Wanaziweka kwenye shimo na wanawasha Moto ili kuzifukishia moshi kwa masaa mawili halafu Kesho yake zinatolewa na zitaanza kutoa rangi, hii inaitwa kupigwa Moto.
 
Siwezi kushauri watu kutokunywa wala kula, kila kiuzwacho na kina leseni ya SErikali tumia.

1. Shisha- vuta maana wanaovutisha wana leseni.
2. K-Vant- kunywa uwezavyo, wana leseni na inalipa kodi.
3. Kuchepuka na mume wa mtu- nenda kapigwe mashine, so long as upo juu ya 18 years.
Isipokuwa usifunje Sheria za nchi
 
Back
Top Bottom