DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Siyo Dar pekee. Kuna binti aliwahi nisimulia kwamba ndicho walichokuwa wanakifanya huko Sumbawanga.

Boss wake ambaye ndo alikuwa na store, ilikuwa akishapata ndizi mbivu tokea Mbeya, alikuwa anazichovya kwenye dawa, then after a day anawauzia wale wamama wenye mabeseni na vibanda vya rejareja. Miaka kama 6 hivi iliyopita.

Kama hili lilitokea Swax, vipi DAR?
Hii ya Sumbawanga pia niliwahi sikia miaka zaidi ya 10 sasa imepita.
 
Hii nimewahi kuisikia. Duh nitakuwa mhanga wa kwanza maana mimi nikila wali lazima ndizi mbivu iwepo.
Nasikia ni zile za rangi ya kama njano sijui
Dsm ni hatari.

Kuna siku nilipita soko la Makumbusho vibanda vya kuku. Nikakuta muuzaji na mwenzake (alijifanya msaidizi wa muuzaji), huyo mwenzake anamalizia kupakia kwenye mfuko kuku kadhaa walioandaliwa. Nikataka wanichinjie kuku wawili toka bandani. Yule mwenzake akadakia "bro si tungepunguza toka kwenye oda ya huyu ninayemfungia ili tusikucheleweshe? Ntabaki na-replace tu coz ninayempelekea hana haraka."

Nikasema poa. Jamaa akaenda kunichukulia mfuko ili achomoe wawili aniwekee. Yule jamaa aliyebaki akaniambia "bro, unaonekana mstaarabu, nafsi inanisuta, acha nikwambie ukweli. Huyo jamaa si muuzaji wangu bali huwa anapita kukusanya kwa bei chee kuku waliokufa hapa sokoni au wakati wa usafirishaji, anaenda kuwauzia wauza chips na mama ntilie kwa bei ndogo. Chagua tu bandani tu uchinjiwe."

Aisee nilichoka. Na hamu ya kuku ikaisha. Nikamwambia basi bro, nikampoza kidogo. Jamaa wakati anarudi na mfuko akaniona naondoka, nikamjibu sihitaji tena, wife kanipigia alishanunua mahali so mpelekee tu jamaa oda yake.

Muuzaji aliniambia wako wengi wanapita kukusanya. Hakuna soko kuku waliokufa wanatupwa.
 
Kuna macontainer ya kuivisha ndizi zitakuwa story tu za kahawa hizi.

Watu wanadanganyana sana kwenye vijiwe vya kahawa ,wanashindwa kujua ukichukua ndizi mbichi ukaiweka tu ndani bila hata kuifunika haichukui siku tatu ishaiva sasa ya nini uitose kwenye kemikali ,halafu ndizi kweli uiloweke kwenye kemikali ikitoka itakuwa salama? Si itakuwa nyonde nyonde na si kavu kabisa...ndizi ikiwekwa kwenye friji kama wanavyosema inakuwa nyeusi tiii sasa hawa wauza kahawa wanakwambia zinawekwa kwenye friza.
 
Uwongo ni uwongo ni uwongo! Nawatetea mara tatu.

Iko hivi:

Kuna jamaa mmoja pale ubungo maziwa ana contena za futi 40 kama nne kaziwek pamoja.

Hizi kontena kavuta umeme ka isa halali wa 3face na kafunga mota (mashine ya kupuliza joto) kama AC. Ndani ya kontena zote.

Mle ndani huyu bwana ananunuaga ndizi mikoani kote kwenye masoko, ameajiri vijana wengi sana kazi yao ni kukata hizi ndizi vichane vichane na kuzipanga ndani kwenye kontena mle hadi zinajaa mwanzo mwisho chini hadi juu, haya mashine alofunga yana geji (asilimia anazoseti kupiliza joto ndani mle )akipanda ndizi mbichi leo jioni akiwasha kesho yake zote zimeiva pamoja haijalishi zimekomaa au hazijakomaa vizuri zote zinaiva kiwango sawa.

Jamaa kwa sasa ana magari bodaboda toyo hadi vikirikuu vya kusuply mzigo wake sehemu mbali mbali.

Hata wewe ukienda kununulia hapo u aruhusiwa au kupeleka ndizi zako unapigiwa mahesabu ya garama kuivisha.

Hivyo huyu jamaa kwa sasa soko amelipatia na anaendelea.

Huu uwongo wako sijui tetesi sio kweli nitamtetea maana tushaenda hapo na tukaona anavyoivisha.

Ila hizi ndizi tatizo lake zikishatolewa kwenye mashine haziwi na utamu wake tena ule wa asili sukari i apungua.
 
Hili jambo lipo siku nyingi na lilianzishwa na wachina, siku hizi zile ndizi nzuri toka mikoani hazipo, zipo hizi zinazouzwa kwa mafungu na zina rangi ya njano na kijani zikiwa zimekatwa toka kwenye mkungu.
 
Hii nimewahi kuisikia. Duh nitakuwa mhanga wa kwanza maana mimi nikila wali lazima ndizi mbivu iwepo.
Nasikia ni zile za rangi ya kama njano sijui
SIo kweli.

Kuna jamaa Ubungo maziwa pale ana mashine kupuliza joto kafunga kwenye kontena anavundika ukipeleka ziko mbichi unapigiwa hesabu kesho yake unaenda chukua mbivu zako.

Hakuna cha dawa wala nini, nimeshuhudia kwa macho yangu anavyofanya
 
Uwongo ni uwongo ni uwongo! Nawatetea mara tatu.

Iko hivi:

Kuna jamaa mmoja pale ubungo maziwa ana contena za futi 40 kama nne kaziwek pamoja.

Hizi kontena kavuta umeme ka isa halali wa 3face na kafunga mota (mashine ya kupuliza joto) kama AC. Ndani ya kontena zote.

Mle ndani huyu bwana ananunuaga ndizi mikoani kote kwenye masoko, ameajiri vijana wengi sana kazi yao ni kukata hizi ndizi vichane vichane na kuzipanga ndani kwenye kontena mle hadi zinajaa mwanzo mwisho chini hadi juu, haya mashine alofunga yana geji (asilimia anazoseti kupiliza joto ndani mle )akipanda ndizi mbichi leo jioni akiwasha kesho yake zote zimeiva pamoja haijalishi zimekomaa au hazijakomaa vizuri zote zinaiva kiwango sawa.

Jamaa kwa sasa ana magari bodaboda toyo hadi vikirikuu vya kusuply mzigo wake sehemu mbali mbali.

Hata wewe ukienda kununulia hapo u aruhusiwa au kupeleka ndizi zako unapigiwa mahesabu ya garama kuivisha.

Hivyo huyu jamaa kwa sasa soko amelipatia na anaendelea.

Huu uwongo wako sijui tetesi sio kweli nitamtetea maana tushaenda hapo na tukaona anavyoivisha.

Ila hizi ndizi tatizo lake zikishatolewa kwenye mashine haziwi na utamu wake tena ule wa asili sukari i apungua.
Mkuu samahani unaweza nipatia namba zake
 
Nyie mnaimba iyena iyena huku mnasubiria kujulishwa mnachowekewa?
Hivi unajua juisi za embe za ile kampuni ni nini mnawekewa?
Mnafikiri mnawekewa maembe?
Hujajibu swali kajitatakia kivipi? Unaweza kusema watu wasinywe juisi za madukani, wasile mbivu za sokoni,Je mchele, nyama, samaki ,maharage, unga, maziwa ambavyo na wewe pia pengine unatumia una uhakika viko salama?
 
Back
Top Bottom