Wafanyabiashara wa Tanzania hawataki kabisa kulipa kodi, wana tatizo gani vichwani? Too much kulia lia

Kuna vilaza wamejaa kwenye ofisi za wakusanya kodi, wanadhani kutumia nguvu ndio dawa ya kusaidia mambo yaende.
Kuna nchi gani unaijua ambayo Kukusanya kodi huwa ni kumbembelezana? Taja moja tu! Iwe nchi ya maana, usiniambie Somalia.
 
Halafu kodi nyingi sana siyo za Wafanyabiashara.

Wao ni mawakala tu kwa niaba ya serikali lakini bado hawataki kulipa kodi mpaka kwa mbinde!

Mfano VAT, PAYE, n.k siyo hela zao lakini bado kulipa ni kwa shuruti [emoji848][emoji848][emoji848]

Bongo bahati nzuri.
Hata walipoambiwa kununua EFD ilibidi nguvu itumike! Hata VAT walikuwa wanadhani ni pesa yao! Kila biashara eti anatafuta msamaha wa kodi! Fallacy!
MOTTO ni fanya biashara, lipa Kodi hutaki kulipa kodi achana na biashara, hujakomaa.
 
Kama hiyo ndo Motto ya kufanya biashara, kwa nini wanalia-lia kila siku? Kodi kodi!
Soma message yangu #6. Usidhani kila anayefanyabiashara ni kutafuta kukwepa kodi. LIPA KODI kama mtu mwingine.
Usiotee moto kwa mbali, ingia ngoma ucheze.
Usiwe kama shabiki anayejua kupanga wachezaji uwanjani lakini yeye mwenyewe hata kupiga kiki na kufunga goli lililonmita 10 mbele yake hawezi.

Jibu wanalotka wafanyabiashara kwa kodi kandamizi ni kufunga biashara na kuhamisha mitaji, ili ninyi wajuaji mnaojua kulipa kodi mjaze hiyo nafasi.

Ukishafungua biashara yako niite nije kukupongeza.
 
Wafanya biashara wengi siyo waadilifu kabisa.
Siyo uadilifu tu, wengi hata ubwege uko kichwani.
Naangalia majibu ya thrd hii hadi unaona huruma. Yaani mtu anategemea kubembelezwa kulipa kodi! Nani akubebe? Mtu anasema anapata hasara, sasa hilo ni jukumua la TRA? Ukishabaki kwenye sekta hii ya biashara, wewe unategeneza faida. Kama unapata hasara na bado umo ndani, wewe ni bwege. HApo ndo mtu anakimbizana na TRA eti akwepe kodi, ndo iwe faida yake.
 
Kimsingi serikali inajiendesha kwa kulipa kodi..wananchi wanatakiwa waelimishwe tangu utotoni mashuleni instead ya kutuletea masomo ya kina kinjekitile ngware..bora somo ra biashara na kodi liwe lazima...kisha ziwepo sheria kali kwa yeyeote asiye fanya kazi na kutokulipa kodi...nchi hii tutaijenga wenyewe.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipe kodi vipi
1wakati hawatengenezi faida
2.Hakuna mazingira ya uwezeshaji
3.Serikali hamna wanachowafanyia mbali na kuonekana siku za kudai kodi
4.kodi ina viwango vikubwa inakaribiana kabisa na turnovers zao it's just like ukianzisha biashara serikali ndo inapata kula na kupunguza mtaji wako
5.Kuhusianisha biashara na mlengo wa kisiasa
6.Political insecurity(risks) ,yaani usipopendwa tu hata na diwani biashara yako inapigwa neno moja tu ,wanakuharibia reputation na kushuka mapato
7.utadai vipi kodi wakati mindset ya kiunyonge Tajiri yoyote ni mwizi ,mnyonyaji na mzurumaji wa taifa?(mhujumu uchimi)
8.Sheria nyingi za biashara zinaadhibu badala ya ku create room ya negotiation (resolution)
9.Mazingira ya ujasiamali mabovu
Ongezeeni wadau
Nikiangalia unayoyataja ni kama unajivisha makosa mwenyewe. Kama hali ndo ilivyo, aliyekuingiza ktk biashara ni nani? Eti mtu anatishia kuhamia Kenya, Kenya rubbish! Nenda ufanyebiashara, usilipe kodi, tutakupa hongera.

Acheni uzembe! Hata huyo naibu waziri aliyewasikiliza naye ana shida nyingine iliyompeleka. Waziri wake asimtume tena maana naona kama hana uelewa wa papo kwa papo. Anasubilia akasome kwenye internet, halafu aje na mifano ya Kenya, Uganda, Lebanoni, nk. Hapa ni TZ. soma sheria zetu zinasema nini, FINITO! Yaani mtu aingie ktk sekta halafu ndo adai kubadilishiwa sheria! Naibu umesoma hadi darasa la ngapi?
 
Kuna nchi gani unaijua ambayo Kukusanya kodi huwa ni kumbembelezana? Taja moja tu! Iwe nchi ya maana, usiniambie Somalia.

Wenzetu kodi ziko wazi. Tanzania mkusanya Kofi anakuja na makadirio anayoyafikiria yeye.
Kwasababu hiyo tumezalisha wala rushwa wakubwa. Ndio maana wanajisikia kufanya lolote sababu mlipa kodi eti analazimika kulipa kodi hata kama sio kodi stahiki.
Mlisomea wapi kukusanya kodi? Kwani lazima muwe nyinyi mnaofanya kazi mechanically? Kodi ni wajibu wetu sote kulipa. Ila watu wangapi wanalipa kodi inavyostahili Tanzania? Hizo hela za rushwa zinalipiwa wapi kodi?
 
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep
Tatizo makadirio hayafanyiki kiusahihi,na vilevile wengi wanafanya biashara kwakuchukua mikopo yenye riba kubwa kubwa ambayo ni matokeo ya usimamizi mbaya toka serikalini.Kingine ni serikali kua na irrational decisions nyingi,kwa mfano wamezuia malipo huko TARURA toka tarehe 20march,bila sababu za msingi,ni kama hawajui inawaadhiri vipi wafanyabiashara..wengine walitakiwa kurejesha mikopo,wengine wameshindwa kulipa mishahara wafanyakazi..nachomaanisha complex problems should be tackled by system approach techniques,sio kisiasa siasa!
 
Nikiangalia unayoyataja ni kama unajivisha makosa mwenyewe. Kama hali ndo ilivyo, aliyekuingiza ktk biashara ni nani? Eti mtu anatishia kuhamia Kenya, Kenya rubbish! Nenda ufanyebiashara, usilipe kodi, tutakupa hongera.

Acheni uzembe! Hata huyo naibu waziri aliyewasikiliza naye ana shida nyingine iliyompeleka. Waziri wake asimtume tena maana naona kama hana uelewa wa papo kwa papo. Anasubilia akasome kwenye internet, halafu aje na mifano ya Kenya, Uganda, Lebanoni, nk. Hapa ni TZ. soma sheria zetu zinasema nini, FINITO! Yaani mtu aingie ktk sekta halafu ndo adai kubadilishiwa sheria! Naibu umesoma hadi darasa la ngapi?
Wajinga ninyi.
Fungueni biashara ILI MLIPE KODI na ninyi.
Bla bla za kutojua kilichokuwepo kina kera.

Watu wanahamisha mitaji nyi mnafikiria vibiashara vya Mangi kwenye kona.
Wa,a hamuelewi kuwa 80% ya kodi ya Nchi inatokana na wafanyabiashara wa Dar es salaam, na wengi wako njiani kufunga biashara zao au wameshafunga.

Huko Zanzibar , Malawi, Zambia wanakaribishwa kwa mikkno miwili.
Kariokoo tulioyokuwa tunaifahamu sasa ni magofu.
Kadi sasa haipo pale.

Hakafu nyie vibulushuti msiojua hata kuuza kashata mnapiga nyeee, nyeee, nyeee!
 
Niko sokoni nina meza yangu tangu nimalize chuo kikuu. Hapa nalipa kodi ya maana kabisa! Bila hata kuzunguka kila kona nikilia lia bila sababu. Lipa kodi. Ukishindwa tafuta unakoona kodi haitakiwi.
Kwanza wewe sio mlipa Kodi halafu unakuja kuchanganya walipa Kodi (una TIN)
Hapo unalipa Ushuru tu wa Sokoni ili wasafishe wala hulipi wa Manis[aa/Halmashauri au Jiji, anapopita huyo Mama mkusanya Ushuru wa kila siku hichi kisenti ndio unahesabu Kodi
sasa sisi wenye TIN namba utatuweka wapi?
  • Chumba tu cha Biashara unalipia 30% ya Kodi ya mwenye nyumba na wanaongeza katika hiyo 30% ya mwenye nyumba uumlipie tena % kwa mapato yake
  • uje Biashara uliyoiingiza bado utakapouza 18%
  • Mashine ya EFD
  • Service Levy kwa kila mwezi kwa Manispaa iwawashie nyie taa za barabarani
  • 10,000 ya Usafi wa Taka kila mwezi
unachozungumzia na kujitapa ni USHURU
 
Namshauri Rais SSH azungumze na wafanyabiashara biashara awaambie wazi kuwa anashughulikia kero zao kuziondoa lakini wajibu wao wa kulipa kodi stahiki uko palepale bila kupepesa macho.

Voluntary compliance TZ iko chini sana.

Ni wazi kuwa kuna mahala hao jamaa nao hawajawajibika ipasavyo.
 
Eti kodi yenyewe ni 18% tu

Wewe hiyo rate unaiona ndogo?

Kama mzigo wako ni wa Millioni 100 kodi hapo ni million 18
 
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep
Hoja ya msingi ni kubambika kodi zisizolipa kwa kisingizio cha penality. Wafanyabiashara wanataka kulipa kodi halali iliyo kadiriwa kwa weledi na uhalisia. Fullstop
 
KIwango kiko ktk %age. Sasa wanaotishia kuhama asilimia yao ni kubwa kuliko wengine?
 
Kwanza wewe sio mlipa Kodi halafu unakuja kuchanganya walipa Kodi (una TIN)
Hapo unalipa Ushuru tu wa Sokoni ili wasafishe wala hulipi wa Manis[aa/Halmashauri au Jiji, anapopita huyo Mama mkusanya Ushuru wa kila siku hichi kisenti ndio unahesabu Kodi
sasa sisi wenye TIN namba utatuweka wapi?
  • Chumba tu cha Biashara unalipia 30% ya Kodi ya mwenye nyumba na wanaongeza katika hiyo 30% ya mwenye nyumba uumlipie tena % kwa mapato yake
  • uje Biashara uliyoiingiza bado utakapouza 18%
  • Mashine ya EFD
  • Service Levy kwa kila mwezi kwa Manispaa iwawashie nyie taa za barabarani
  • 10,000 ya Usafi wa Taka kila mwezi
unachozungumzia na kujitapa ni USHURU
Ndo hapo unashindwa kuelewa maana ya kodi. Hiyo ndo kodi inavyokwenda. Unalipa kwa jinsi unavyopata. Tatizo lako unataka usilipe kwa ksingizio cha ajira, nchi jilani, na bhla! bhla! kibao. Nikiuza chungwa zangu 50 kwa bei ya sh 200, siku inakwisha nikiwa na sh. 10000 na shilingi 1000 nimelipa ushuru wa soko. Wewe uza maua ya bilioni lakini kumbuka sheria inayosimamia biashara yako. Unataka kubadili sheria katikati ya mchezo? Ulianza biashara yako hukuijua kabla?

Naomba uniongezee mtaji, nifungue mashamba ya matunda na hapo ndo utajua ninavyojua sekta zisizo na mgogoro na TRA. Tusiishie kuhangaika na kutafuta lobbyists kutusaidia kufuta kodi za kisheria na kununua mafuta ya gari ya Naibu waziri wakati unajua sheria iko pale pale!
 
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep
Elimu ya kodi kwa wananchi bado haijawafikia,serikali ianzishe kabisa somo maalumu kuanzia O'level (kidato cha kwanza kuendelea), taifa haliwezi kusonga mbele kwa kujitegemea bila wananchi wake/wafanyabiashara kulipa Kodi inayotakiwa
 
Nimeona clip ya Naibu waziri wa Kilimo, Bashe na baadhi ya wakulima wa bustani pale Arusha, wakijieleza kwa kudeka sana, na kueleza eti kodi ni kubwa. Kodi yenyewe ni 18%. Huu ni uzembe ktk biashara na ni tatizo la mazoea.

Wakati mukilenga kumtisha rais, kumbukeni pia kuna maelezo ya kupanua wigo wa kodi, hivyo kama hamkuwa mukilipa kodi, lipeni. Anayekwenda Kenya wasikolipa kodi, aende! Mbona Kenya wanalipa kodi ya ardhi kubwaaa lakini wako kimya!

Mara ajira, mara hasara, visingizio viiingi! Wafugaji wanalipa, wasafirishaji wanalipa, waajiliwa wanalipa. Ninyi wakulima ndani ya viyoyozi hamtaki kwa tishio la kuhama, hameni Mbona wezi wanahamia wanakoruhusiwa kuiba! Too much demands!

It's useless to play lullabies for those who cannot sleep Hata biashara hujawahi fanya wewe even if kuuza chichili!!
 
Elimu ya mlipa kodi bado sana kwa wafanyabiashara. TRA walijisahau sana wakawa wanakusanya pesa bila kutoa taarifa na elimu wa watoa pesa.

Wakielewa makundi ya walipa na vigezo vya kuwa kwenye kila kundi watalipa bila matatizo.

Watanzania sio wabishi kwa vitu wanavyoelewa.
I love you Mama Dee
 
Ndo hapo unashindwa kuelewa maana ya kodi. Hiyo ndo kodi inavyokwenda. Unalipa kwa jinsi unavyopata. Tatizo lako unataka usilipe kwa ksingizio cha ajira, nchi jilani, na bhla! bhla! kibao. Nikiuza chungwa zangu 50 kwa bei ya sh 200, siku inakwisha nikiwa na sh. 10000 na shilingi 1000 nimelipa ushuru wa soko. Wewe uza maua ya bilioni lakini kumbuka sheria inayosimamia biashara yako. Unataka kubadili sheria katikati ya mchezo? Ulianza biashara yako hukuijua kabla?

Naomba uniongezee mtaji, nifungue mashamba ya matunda na hapo ndo utajua ninavyojua sekta zisizo na mgogoro na TRA. Tusiishie kuhangaika na kutafuta lobbyists kutusaidia kufuta kodi za kisheria na kununua mafuta ya gari ya Naibu waziri wakati unajua sheria iko pale pale!

Basi endeleeni kufunga baishara za watu na kuingia kwenye account za watu na kupora pesa zao ili mkusanye kodi nyingi.

Watu wanapigana vita zaidi ya miaka ishirini mwisho wanamaliza vita kwa kukaa mezani. Maguvu na ubabe haviajawahi kuleta maendeleo ya kweli kwenye Dunia ya kistaarabu.

Kwaheri Mwendazake.
 
Back
Top Bottom