Wafanyabiashara wa vyakula wa mkoa wa mbeya faida wanazipataje?

Wafanyabiashara wa vyakula wa mkoa wa mbeya faida wanazipataje?

Isenye

Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
97
Reaction score
628
Niko mkoa wa mbeya hasa shughuli zangu zilizonileta nazifanyia mbeya mjini na Tukuyu.

Hizi bei ndogo za vyakula wanazouza zimenifanya nijiulize hawa watu faida wnazipataje.
Mfano

Kande la mahindi mabichi na maharage wanauza sh 500,wakati dar mara ya mwisho kula kande niliuziwa 2,000/=

Wali nyama bei ni 1,500/= Dar ni 3,000/=

Wali maharage ni 1,000/= wakt dar ni 2,000/=

Chips kavu bei ni 1,000/= za kushiba wanakuambia 1,500/= hizo za kushiba mwanaume wa dar hawezi kuzimaliza coz ni sahani inajaa fully.

Kitimoto kilo ni elfu 9,wakt Dar nimeacha 12,000/=
Parachichi kubwa ni 500/=
Viazi mviringo debe ni elfu 9.
Michele debe ni elfu 35.
Mahindi debe ni elfu 12.

Nyama ya ng'ombe nimeona hapo uyole bucha flani wameandika kilo ni elfu 7 wakt dar bei nimeacha ni elfu 12
Supu ya ng'ombe na ndizi tatu ni 1,500/=

Kichane cha ndizi mbivu ni elfu 1.
Maziwa lita 5 ni elfu 10
Mafuta ya alizeti lita 5 ni elfu 25
Hawa watu faida wanazipataje?
 
Najamaa yangu aliendaga mbeya miaka fulani hivi.

Jamaa ndio ilikua first time kutimba mbeya, amefika jioni akatoka kwenda kula chips, akaagiza chipsi za buku 2.

Alipofika alikuta vijana watatu, kila mmoja yupo bize na mambo yake, aliposema tu nipe chipsi za buku 2 unaambiwa kila mtu akaacha alichokua anafanya wakaanza kumtazama jamaa huku wanaongea kilugha.

Mzigo ulivyokuja jamaa akasema hii sio oda yangu.

PIA SOMA:

Mimi pia naishi Mbeya huwa wananishangaza sana lakini bei ya mazao sokoni ipo chini.
Niko mkoa wa mbeya hasa shughuli zangu zilizonileta nazifanyia mbeya mjini na Tukuyu.

Hizi bei ndogo za vyakula wanazouza zimenifanya nijiulize hawa watu faida wnazipataje.
Mfano

Kande la mahindi mabichi na maharage wanauza sh 500,wakati dar mara ya mwisho kula kande niliuziwa 2,000/=

Wali nyama bei ni 1,500/= Dar ni 3,000/=

Wali maharage ni 1,000/= wakt dar ni 2,000/=

Chips kavu bei ni 1,000/= za kushiba wanakuambia 1,500/= hizo za kushiba mwanaume wa dar hawezi kuzimaliza coz ni sahani inajaa fully.

Kitimoto kilo ni elfu 9,wakt Dar nimeacha 12,000/=
Parachichi kubwa ni 500/=
Viazi mviringo debe ni elfu 9.
Michele debe ni elfu 35.
Mahindi debe ni elfu 12.

Nyama ya ng'ombe nimeona hapo uyole bucha flani wameandika kilo ni elfu 7 wakt dar bei nimeacha ni elfu 12
Supu ya ng'ombe na ndizi tatu ni 1,500/=

Kichane cha ndizi mbivu ni elfu 1.
Maziwa lita 5 ni elfu 10
Mafuta ya alizeti lita 5 ni elfu 25
Hawa watu faida wanazipataje?
 
Dar ya wapi hiyo wali nyama 3,000 nipajue vizuri ili siku nikiwa na ziara nitoke home nikiwa nimeshiba?

Actually ni kweli Mbeya kuna gharama nafuu za vyakula ila kwa Dar maeneo mengi regular bei za msosi ni 1,500.

Hapo hapo Mbeya ukisema ushuke wilaya ya Chunya utashangaa bei ya chakula ilivyokuwa ghali.
 
Nilinunua chips kavu za buku jero mbeya wakanijazia chips kwenye ndoo kubwa ya lita 20, huku jamaa ananiambia kiongozi samahani viazi vimetuishia naomba tukuuzie kwa 500 tu hizi badala ya buku jero
 
Back
Top Bottom