Wafanyabiashara wa vyakula wa mkoa wa mbeya faida wanazipataje?

Wafanyabiashara wa vyakula wa mkoa wa mbeya faida wanazipataje?

Niko mkoa wa mbeya hasa shughuli zangu zilizonileta nazifanyia mbeya mjini na Tukuyu.

Hizi bei ndogo za vyakula wanazouza zimenifanya nijiulize hawa watu faida wnazipataje.
Mfano

Kande la mahindi mabichi na maharage wanauza sh 500,wakati dar mara ya mwisho kula kande niliuziwa 2,000/=

Wali nyama bei ni 1,500/= Dar ni 3,000/=

Wali maharage ni 1,000/= wakt dar ni 2,000/=

Chips kavu bei ni 1,000/= za kushiba wanakuambia 1,500/= hizo za kushiba mwanaume wa dar hawezi kuzimaliza coz ni sahani inajaa fully.

Kitimoto kilo ni elfu 9,wakt Dar nimeacha 12,000/=
Parachichi kubwa ni 500/=
Viazi mviringo debe ni elfu 9.
Michele debe ni elfu 35.
Mahindi debe ni elfu 12.

Nyama ya ng'ombe nimeona hapo uyole bucha flani wameandika kilo ni elfu 7 wakt dar bei nimeacha ni elfu 12
Supu ya ng'ombe na ndizi tatu ni 1,500/=

Kichane cha ndizi mbivu ni elfu 1.
Maziwa lita 5 ni elfu 10
Mafuta ya alizeti lita 5 ni elfu 25
Hawa watu faida wanazipataje?
Ndoa maana wanaitwa green city.ni mkoa uliobarikiwa kuwa na mvua nyingi,mazao mengi ya kila namna.ukiishi Mbeya ukashindwa kujenga basi nenda kwa mganga.hata bidhaa za ujenzi bado ni chini.
 
Umenikumbusha mwaka fulani hivi tulienda Mbeya kwa ajili ya Semina tulikaa kama wiki 2 hivi aisee tulienjoy sana.
Kwenye mambo ya msosi mimi nilikuwa napenda kuagiza wali na kuku wa kienyeji pande la nguvu na vipande vya parachichi wanaweka kwa juu ya wali bure kwa bei ya 3000.
Kitu kingine kilichokuwa kinanipa mshangao ilikuwa tukienda bar kwa ajili ya burudani unakuta bili inakuja jumla elfu 5 tu halafu saa ya kulipa muhudumu anapokea hela kwa ishara ya kupiga magoti kisha anatoa sauti ya unyenyekevu ya Kinyakyusa"Na kesho mje tena"
 
Mfuko wa Cement, Sukari, na Chupa za Maji, Uhai, Kilimanjaro au Juice ya Pakti ya Azam ni bei gani ? Bila kusahau average Kodi ya Pango wanalouzia bidhaa zao.
 
Tukuyu mbeya ukifika hapo ni kama upo tu jikoni misosi kibao na kale kabaridi kana support mambo mengi!
 
Niko mkoa wa mbeya hasa shughuli zangu zilizonileta nazifanyia mbeya mjini na Tukuyu.

Hizi bei ndogo za vyakula wanazouza zimenifanya nijiulize hawa watu faida wnazipataje.
Mfano

Kande la mahindi mabichi na maharage wanauza sh 500,wakati dar mara ya mwisho kula kande niliuziwa 2,000/=

Wali nyama bei ni 1,500/= Dar ni 3,000/=

Wali maharage ni 1,000/= wakt dar ni 2,000/=

Chips kavu bei ni 1,000/= za kushiba wanakuambia 1,500/= hizo za kushiba mwanaume wa dar hawezi kuzimaliza coz ni sahani inajaa fully.

Kitimoto kilo ni elfu 9,wakt Dar nimeacha 12,000/=
Parachichi kubwa ni 500/=
Viazi mviringo debe ni elfu 9.
Michele debe ni elfu 35.
Mahindi debe ni elfu 12.

Nyama ya ng'ombe nimeona hapo uyole bucha flani wameandika kilo ni elfu 7 wakt dar bei nimeacha ni elfu 12
Supu ya ng'ombe na ndizi tatu ni 1,500/=

Kichane cha ndizi mbivu ni elfu 1.
Maziwa lita 5 ni elfu 10
Mafuta ya alizeti lita 5 ni elfu 25
Hawa watu faida wanazipataje?
Dar ni dar na Mbeya ni.mbeya Acha ushamba
 
Taburalaza wanauza bei ya vitu vya viwandani wakti mada iliyopo ni bei ya vyakula.
 
Najamaa yangu aliendaga mbeya miaka fulani hivi.

Jamaa ndio ilikua first time kutimba mbeya, amefika jioni akatoka kwenda kula chips, akaagiza chipsi za buku 2.

Alipofika alikuta vijana watatu, kila mmoja yupo bize na mambo yake, aliposema tu nipe chipsi za buku 2 unaambiwa kila mtu akaacha alichokua anafanya wakaanza kumtazama jamaa huku wanaongea kilugha.

Mzigo ulivyokuja jamaa akasema hii sio oda yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ndio mana wanyakyusa wanene. Labda kama hajakulia huko au ana_maintain figa
 
Nilinunua chips kavu za buku jero mbeya wakanijazia chips kwenye ndoo kubwa ya lita 20, huku jamaa ananiambia kiongozi samahani viazi vimetuishia naomba tukuuzie kwa 500 tu hizi badala ya buku jero
Uongoooo 🤣🤣🤣🤣
 
Kuna supply kubwa ya vyakula vya shambani, wanazalisha sana maeneo hayo na hivitoki mbali hivyo gharama za usafiri na uhifadhi zinapungua.

Wengine hawanunui bali wanaagiza tu kijijini kwao.

Hapo anayeumia ni mkulima analaliwa sana
 
Najamaa yangu aliendaga mbeya miaka fulani hivi.

Jamaa ndio ilikua first time kutimba mbeya, amefika jioni akatoka kwenda kula chips, akaagiza chipsi za buku 2.

Alipofika alikuta vijana watatu, kila mmoja yupo bize na mambo yake, aliposema tu nipe chipsi za buku 2 unaambiwa kila mtu akaacha alichokua anafanya wakaanza kumtazama jamaa huku wanaongea kilugha.

Mzigo ulivyokuja jamaa akasema hii sio oda yangu.
dah umenichekesha sana mkuu😂😂
 
Back
Top Bottom