Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umeonaUtasikia hiki dar 3000😅😅😅
Vipi upatikanaji wa hela za kununulia hivyo vyakula? Unaweza kumwambia mshikaji una buku ya karibu hapo akakupa?Sijaona mkoa wenye vitu cheap kama Mbeya huku gharama ya maisha ipo chini compared to other regions
Na tofari ni bure kabisa. Tope tu pale kwa mama John nyumba inaenda.Ndoa maana wanaitwa green city.ni mkoa uliobarikiwa kuwa na mvua nyingi,mazao mengi ya kila namna.ukiishi Mbeya ukashindwa kujenga basi nenda kwa mganga.hata bidhaa za ujenzi bado ni chini.
Japo kaongeza chumvi ila ni kweli ukienda maeneo vinakolimwa viazi chips za 2000 ni zaidi ya sinia,😂hapa umezidisha mashudu
Usiwashtue wakatuletea mabalaa, wao wanaamini utafutaji hela Mbeya ni mgumu 😀, wakati huko huko Dsm kuna watu wanalipwa hela ya mahindi ya kuchoma UyoleTunamwambia mje Mbeya
Mnajidai kung'ang'ana Dsm
Mtakuja kufa njaa.
Hapo kamaanisha mtindi, Tukuyu hiyo elfu 10 ni lita 10Maziwa lita 5 kwa elfu kumi ni ghali sana
Chips 2500? Hiyo si chips yai na mayai matatu! Kwanza ni sehemu gani huko uliuziwa kwa hiyo bei? Parachichi Mbeya bei inaanzia 300, maziwa ni 1000 kwa lita eneo analokaa hiyo 10k ni mtindi, maisha sio ghali mbeya ila ni kweli kwasasa Wakenya wapo wengi kwenye parachichi kama ambavyo wapemba wapo wengi kwenye ndizi na viazi.1.Dar wali 1500 unapata yule mama anauza
2.Maziwa sawa na Dar to lita 5 ni elfu kumi
3.Chips mbeya bei yake sawa na Dar tu 2500 ,nimetoka uko juzi
4.kuna mwingine anadai eti wali kuku ni shilingi elfu 3 muongo ,nimepuyanga maeneo yote kuanzia mafiati,kabwe,mwanjelwa,sai mama john ,uyole hakuna kitu kama hicho maisha kwa sasa hata mbeya yameanza kuwa juu kutokana na muingiliano wa wageni umekua mkubwa pia wageni wengi hasa wakenya wanaenda mashambani kununua mazao,kwa sasa parachichi limepaa sana bei yake sawa na Dar tu shilingi 500
Kabwe ndiyo karibu na kwa mama John eeeh?Nipo KABWE saa 7:42 pm Tarehe 6.3.2025 Hapa MBEYA, Sasa Hivi... Maisha ya MBEYA ni Poa sana kwa Upande wa Chakul 1
Pagumu mzeeVipi upatikanaji wa hela za kununulia hivyo vyakula? Unaweza kumwambia mshikaji una buku ya karibu hapo akakupa?
mbona hapo bei zimepanda mkuu?Niko mkoa wa mbeya hasa shughuli zangu zilizonileta nazifanyia mbeya mjini na Tukuyu.
Hizi bei ndogo za vyakula wanazouza zimenifanya nijiulize hawa watu faida wnazipataje.
Mfano
Kande la mahindi mabichi na maharage wanauza sh 500,wakati dar mara ya mwisho kula kande niliuziwa 2,000/=
Wali nyama bei ni 1,500/= Dar ni 3,000/=
Wali maharage ni 1,000/= wakt dar ni 2,000/=
Chips kavu bei ni 1,000/= za kushiba wanakuambia 1,500/= hizo za kushiba mwanaume wa dar hawezi kuzimaliza coz ni sahani inajaa fully.
Kitimoto kilo ni elfu 9,wakt Dar nimeacha 12,000/=
Parachichi kubwa ni 500/=
Viazi mviringo debe ni elfu 9.
Michele debe ni elfu 35.
Mahindi debe ni elfu 12.
Nyama ya ng'ombe nimeona hapo uyole bucha flani wameandika kilo ni elfu 7 wakt dar bei nimeacha ni elfu 12
Supu ya ng'ombe na ndizi tatu ni 1,500/=
Kichane cha ndizi mbivu ni elfu 1.
Maziwa lita 5 ni elfu 10
Mafuta ya alizeti lita 5 ni elfu 25
Hawa watu faida wanazipataje?
NdioKabwe ndiyo karibu na kwa mama John eeeh?
Chunya kila kitu bei ghali, hadi wadada wanaojiuza kule kuna hela ukimpa anakuona takataka wakati hela hiyo hiyo ukimpa msichana hapa mjini anaona ameokota buziDar ya wapi hiyo wali nyama 3,000 nipajue vizuri ili siku nikiwa na ziara nitoke home nikiwa nimeshiba?
Actually ni kweli Mbeya kuna gharama nafuu za vyakula ila kwa Dar maeneo mengi regular bei za msosi ni 1,500.
Hapo hapo Mbeya ukisema ushuke wilaya ya Chunya utashangaa bei ya chakula ilivyokuwa ghali.