KERO Wafanyabiashara wamechoka kuwekewa taka mbele ya maduka Eneo la Darajani, Vikokotoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest

Wafanyabiashara wa eneo la Darajani, Vikokotoni wanaendelea kukumbwa na changamoto kubwa ya ukusanyaji wa taka mbele ya maduka yao.

Licha ya kulipa pesa za taka kwa Manispaa kupitia tozo zinazojumuishwa kwenye leseni za biashara, taka zinaendelea kuachwa mbele ya maduka baada ya wafagiaji kufagia. Leo nilipopita katika eneo hilo, karibu njia nzima ilikuwa imejaa vifungu vya taka ambavyo havijazolewa.

Hali hii ni endelevu mana karibia siku nne au Zaidi wafagiaji wanafagia bila kuzoa taka. Hali hii inalazimisha wafanyabiashara kujigharamia tena kwa kuwalipa watu binafsi kila siku kuja kuwazolea taka hizo mbele ya maduka yao.

Kwa hali ilivyo sasa, wafanyabiashara wanabeba mzigo wa kulipia huduma ya usafi mara mbili. Mara ya kwanza kupitia pesa wanazokatwa kwa lazima na Manispaa kwenye leseni ya biashara, na mara ya pili kwa kuwalipa watu watakaokuja kuwazolea taka kila siku taka zikiachwa mbele ya duka.

Ni muhimu mamlaka husika kuchukua hatua za haraka ili kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa taka na kuhakikisha huduma ambayo wafanyabiashara wanalipia inatolewa kwa ufanisi.
 
Halmashauri ya mjini Maghribi watafanyia kazi suala Hilo, jambon dogo sana hilo
 
Halmashauri ya Mji Mkongwe unasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…