Wafanyabiashara weusi Tanzania, pelekeni watoto India wasome shahada za family business ili mkifa biashara zisife

Kwahiyo pia unataka kila Mtanzania azae watoto 8 kama Bakhressa??

Kama una mtoto mmoja au wawili wakasoma Finance na Business Admistration za UDSM au UDOM na sio hiyo family business ya India wao hawawezi kutengeneza Admistration structure na kwenye mapungufu wakahire watu wa kuziba hizo nafasi??

Pia unataka kusema hakuna watoto wa kiafrika (Kitanzania) waliofanikiwa kwa kuendesha biashara za familia??

Mkuu shida kubwa ya waafrika na wabongo wengi ni kutohusisha watoto kwenye biashara, na sio watoto tu mpaka mke wakati mwingine hajui chochote kuhusu biashara ya mmewe wala account zina pesa ngapi. Anashirikishwa tu kusign fomu za mikopo za benki..
 
Ukweli mchungu
 
Mie katika pilika pilika zangu za kusaka tonge...nimegundua kitu kimoja kikubwa!

Watanzania wengi biashara zetu ni za uchuuzi tu...yaan unachukua biashara area 1unapeleka area 2!faida ndo unaendeshea maisha...

Ni watz wachache Sana wenye business kubwa au kampuni kbs!sijui umeelewa! Shida inakuja hapo!.tumekuwa wachuuzi zaidi..! Ngumu Sana kumpeleka mtoto akapate elimu nje!

Na hao wenye makampuni weusi ndo Kama unavyosema!😔!
Naamini Kama Kuna takwimu basi wenye firms zao hawazid 2%!
Nchi yetu bado Ina umaskini Sana!..tumetopea!
 
Mzee Ekenywa..
Kutoka EKENYWA ENT CLINIC hadi EKENYWA SPECIALISED HOSPITAL..
Baba alikuwa Daktari bingwa kwa Kinywa na Meno na akafungua hospitali pale Magomeni Mwembechai na Mtoto Dr Emmanuel naye kabobea kwenye Fani ya baba yake hivyo anasimamia hospitali vizuri kabisa...
Pili Kairuki Memorial Hospital ni Family Business..
Baba alikuwa Daktari na watoto na ni Madaktari...!
 
Kwanini Family Business za Wahindi na waarabu zinafanikiwa..?
Kubwa ni Kuwa
Wenzetu wanajenga Biashara katika Misingi ya Ujuzi....
Hivyo mtoto naye Hurithi ujuzi wa wazazi katika mfumo rasmi au usio rasmi..
Pili katika vipindi vya likizo watoto hupata muda mwingi wa kukaa kwenye biashara za Familia zao na kuanza kupata uzoefu wangali bado wadogo...
Hivyo kwa utaratibu huo hurithishana ujuzi vizazi na vizazi...
 
Kweli kabisa, ukimshirikisha mwanao kwenye biashara zako tangu awali itamjengea uzoefu mapema na kufahamika vizuri na washirika wenzako wa biashara, hivyo hatashindwa kuiendeleza.
 
Hazipanuki walivyoaacha wazazi wao ziko hivyo hivyo!!! No New addition!!!!
 
Better to Maintain rather than to DIE...
You are right somehow even though as time goes on stiff competition and New business entrants can kick out the business that doesn't grow!!!!
 
Biashara ni wito na maono, kama nimefanikiwa kuwasomesha basi wakatafute vyao, mi nilifundishwa na nani?

Wacha biashara ife!
 
KiufupI Wazee wa Kiafrika wanapenda kuona watoto wakiteseka. Wanapokufa lazima watu wagawane sababu hakuna anayejua kuendesha biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…