KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa CATA MINE uliopo kijiji cha Kyabakari, Wilayani Butiama Mkoani Mara, jana wameandamana kwa mara nyingine kuelekea katika Ofisi za mgodi huo, kushinikiza mwekezaji kuwalipa malimbikizo ya mishahara yao pamoja na NSSF.
Wakiwa na mabango yenye jumbe Mbalimbali wafanyakazi hao zaidi ya 300 wamesema kuwa mpaka sasa hawajui hatma ya haki yao, kwani wamefanya jitihada zote za kufika hadi kwa Waziri wa Madini lakini hakuna kilichofanyiwa kazi.
Wamemuomba Rais Dkt. Samia kuingilia kati jambo hilo, kwani kwa muda mrefu wameachishwa kazi bila ya kulipwa mishahara yao, huku viongozi wa serikali akiwemo Waziri wakishindwa kutatua shida yao.
Mbele ya waandishi wa Habari, wafanyakazi hao wamesea kuwa wanadai zaidi ya miezi 20 mishahara yao huku wengine wakidai miezi nane, ambapo wamesema mwekezaji huyo hajawahi kuweka fedha zao NSSF tangu wameanza kazi.
“ Kila siku tukifuatilia tunawambiwa njoo kesho, njoo Kesho, maisha yetu kwa sasa magumu sana, tumeenda kwa viongozi wote wa serikali akiwemo Waziri wa Madini lakini imeshindakana, tunamuomba mama aingilie kati Jambo hili,” alisema Joshua Chamolo,
Aidha, walisema kuwa mgodi huo ulisimama kufanya kazi tangu mwezi Desemba 2023, ambapo baada ya shughuli zote kusimama hakuna taarifa yoyote ambayo ilitolewa kwao wala barua ya kusimamishwa kazi.
Soma Pia: Wafanyakazi mgodi wa CATA Mining Mara, waanza mgomo kushinikiza kulipwa mishahara, michango NSSF
Wanabainisha viongozi wote wa mgodi huo akiwemo mwekezaji hawaonekani eneo la mgodi, na wamehaingaika sana kuwapata na imeshindikana.