A
Anonymous
Guest
Siku chache zilizopita tuliwasilisha malalamiko kuhusu changamoto tulizokuwa tunakumbana nazo katika eneo letu la kazi la BCEG Mbezi Beach, ikiwemo madai ya makato ya michango ya NSSF kutowasilishwa pamoja na masuala mengine ya ustawi wa wafanyakazi.
Hoja ya awali ~ Waziri wa Ujenzi na RC wa Dar tusaidieni Wafanyakazi BCEG Mbezi Beach tunakatwa NSSF lakini hazipelekwi
Leo, sisi na wenzetu tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa mamlaka husika kwa kuchukua hatua na kufanyia kazi malalamiko yetu. Tunafurahi kuona kuwa viongozi walilipa uzito suala hili, na hivi karibuni Mkuu wa Wilaya alifika katika eneo letu la kazi kwa ajili ya kufuatilia hali halisi.
Tangu ziara hiyo ifanyike, tumeshuhudia mabadiliko chanya katika mazingira ya kazi. Heshima kwa wafanyakazi imeongezeka, mawasiliano yameimarika, na hata mishahara imeanza kulipwa kwa wakati.
Tunatoa pongezi za pekee kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Maafisa Kazi (Labour Officers) kwa hatua walizochukua na kwa kusimamia haki za wafanyakazi. Tunatumaini usimamizi huu utaendelea ili kuhakikisha haki na ustawi wa wafanyakazi vinaendelea kulindwa.
Kwa niaba ya wafanyakazi, tunawashukuru wote waliohusika kusikiliza kilio chetu na kuchukua hatua stahiki hasa JAMIIFORUMS kwa kuwa ndio waliopaza sauti kilio chetu kikasikika. Ushirikiano huu umetupa matumaini na umetuthibitishia kuwa sauti za wananchi zinaposikilizwa, changamoto zinaweza kupatiwa ufumbuzi.