KERO Wafanyakazi wa CRDB tawi la Meru jijini Arusha jitahidini kutunza siri za taarifa za wateja wenu

KERO Wafanyakazi wa CRDB tawi la Meru jijini Arusha jitahidini kutunza siri za taarifa za wateja wenu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
D

DeletedMember281674

Guest
Hii imetokea siku ya Ijumaa tarehe 16 January 2026, Kuna jamaa aliingia kwenye hili TAWI, akiwa ameenda kupata huduma ya kuweka fedha katika akaunti zingine, lakini yule mteja Kila alichokuwa anafanya yule mteja wale wafanyakazi wa TAWI wakiwa makini sana kufuatilia baadae akatokea mfanyakazi Mmoja mdada mweupe hivi anaonekana umri umeenda akaanza kuropoka mbele ya wateja akiwaambia wafanyakazi wenzake tena kwa Sauti ya juu alisema nanukuu...Mteja mwenyewe nimeangalia akaunti zake (inaonekana huyo mteja ana akaunti zaidi ya Moja) nimekuta Hana hata hela, ni masikini tu kama sisi, huyu mtu Hana hata hela anatusumbua tu hapa, ni masikini tu kama sisi..."

Nilikuwa nimekaa kwenye mabenchi nikiwa kwenye foleni na mwenzangu Mmoja hivi tukaanza kuulizana tangu lini mfanyakazi wa benki akawa anafuatilia undani wa akaunti ya mtu kama ana Pesa au Hana, is it ethical???

Nashauri mtu anayehusika KUSIMAMIA nidhamu na maadili ya Watumishi wa benki ya CRDB afuatilie suala hili kupitia kwenye CCTV camera ambazo NAAMINI zinanasa mpaka Sauti, maana huyo mdada alikuwa anaongea hayo akiwa nyuma ya kaunta za cashier's namba 3 & 4 ilikuwa majira ya kati ya Saa 7:30 Mchana hadi Saa 8:30 Mchana, ili huyo Mtumishi achukuliwe hatua Kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa watumishi wengine kutokutoa taarifa za WATEJA wa benki yetu pendwa kwa watu wasiohusika au kuropoka kuhusu akaunti za watu zina kiasi gani. Kwanza ni suala AMBALO huyo mfanyakazi haimuhusu, kama akaunti ya mteja Ina fedha au Haina; au huyo mtu ana Pesa au Hana. Hayamuhusu hayo masuala, yeye anapaswa kutekeleza jukumu lake aliloajiriwa ikiwa ni pamoja na KUTUNZA SIRI ZA WATEJA.

Naomba kuwasilisha kero hii kwa Uongozi wa Benki ya CRDB.
 
Ndio maana matajiri wanatembea na mabodigadi au mguu wa kuku chini ya kiti cha gari

majangili wanaweza kujua una kiasi gani kwenye account kwa kutoa ofa ya savanna moja tu

Hatua za kinidhamu zinapaswa zichukuliwe Kwa huyu Mtumishi, wakifuatilia kupitia CCTV Camera watampata tu, anahatarisha hata uhai wateja wanaokuja kuhudumiwa katika hilo TAWI, anavujisha Siri wateja wanaweza kuvamiwa na wezi au majambazi wakadhurika au hata kupoteza hata Maisha, kutokana na huyu mfanyakazi wa CRDB TAWI la MERU JIJINI ARUSHA asiyekuwa na maadili
 
Kwa nini na wewe mteja huna hela lakini unajimwambafai na kuwasumbua wahudumu wa benki ukilazimisha upewe huduma first class? Hivi ulishawahi kukutana na maudhi ya wateja? Siungi mkono huo uropokaji wa huyo bidada lakini nawaza tu haiwezekani mama wa watu atoke tu na kuanza kuropoka, kuna shida mahali!
 
Pamoja na kwamba mkuu unatumia ID fake
Picha fake na zaidi ya yote hatufahamiani maana hatujawahi onana sehemu/mahali popote.

Nakiri pasina shaka wewe ni kada wa ccm. Ccm pekee ina watu kama wewe
 
CRDB vibaka ndani ya benki wameongezeka! Majid Nsekela kazi inamshinda?
 
lubajaro usikute mteja mwenyewe ndo wewe.

Unataka private services wakati akaunti hazina hela mzee. Sasa wao watachukuaje gharama zao.

Ungeingia mlango wa pembeni yake pale kwa raia wote, hakuna noma lolote mule. Unahudumia hata kama una jero kwa akaunti.
 
Si ndiyo hapo hata mimi nimeshangaa! Jamaa wanaingia kwa wateja wakubwa huku hana hela kwenye akaunti halafu anaanza kuwafokea wahudumu!
 
Ningekuwa ndiyo Mimi.Huyu mhudumu wa benk angekula makofi.
Utapiga makofi wangapi? Haya ni matatizo ya sehemu nyingi Bongo. Maskini wanadharau wenzao. Hata dukani utasikia ''mteja gani ananunua pisi moja''. Kwa kifupi ni tatizo la umaskini, mtu anajukuta anadharau wenzake.
 
lubajaro usikute mteja mwenyewe ndo wewe.

Unataka private services wakati akaunti hazina hela mzee. Sasa wao watachukuaje gharama zao.

Ungeingia mlango wa pembeni yake pale kwa raia wote, hakuna noma lolote mule. Unahudumia hata kama una jero kwa akaunti.
Hapana. Sikuwa Mimi.
 
Si ndiyo hapo hata mimi nimeshangaa! Jamaa wanaingia kwa wateja wakubwa huku hana hela kwenye akaunti halafu anaanza kuwafokea wahudumu!
Hapana sikuwa Mimi, ila sisi wateja tuliokuwa tumekaa kwenye viti tukisubiri namba zetu ziitwe tulijikuta tunaangaliana kwa mshangao kwa sababu benki siku zote kunakuwa na ukimya na faragha za WATEJA, lakini ukikuta Mtumishi wa benki anaropoka kwa wenzake hicho ndicho kilichotufanya tujiulize na tupate mshangao juu ya hilo.
 
Kwa nini na wewe mteja huna hela lakini unajimwambafai na kuwasumbua wahudumu wa benki ukilazimisha upewe huduma first class? Hivi ulishawahi kukutana na maudhi ya wateja? Siungi mkono huo uropokaji wa huyo bidada lakini nawaza tu haiwezekani mama wa watu atoke tu na kuanza kuropoka, kuna shida mahali!

Nafikiri hujaelewa hoja, mjadala huu unahusiana na uropokaji wa huyo dada kwa kutoa taarifa za account ya mteja ambaye hakuwa na hela katika akaunti zake, hii ndiyo hoja ya Msingi inayohitaji kujadiliwa hapa
 
Back
Top Bottom