KERO Wafanyakazi wa Elements Club (Masaki) kuweni na adabu. Mna madharau na kiburi

KERO Wafanyakazi wa Elements Club (Masaki) kuweni na adabu. Mna madharau na kiburi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Biashara huwa Kuna kupanda na kushuka, club element wasipofanya mapema reform ya wafanyakazi basi Ile club haishuki inaenda kudondoka na kufa kabisa

Nimeamua niandikie leo japo ni tukio lililonitokea mwezi Jana. Sio mara yao ya kwanza kunitreat unfairly imekuwa ni tabia yao.. Tulienda pale na rafiki angu saa tano usiku tukalipa buku ten ya kiingilio tukaenda moja kwa moja kukaa meza moja ilikuwa empty

Muhudumu akaja akasema hii meza reserved, tukamwambia tuonyeshe pa kukaa, akaja baunsa kututoa kwa nguvu mpaka nje, kuulizia nini shida wakasema sisi wasumbufu. Tukasema watusamehe hatukujua but walikataa

Hivi kuulizia tu tukae wapi tayari ni kosa? Yaani wana viburi, huduma mbovu wanathamini mastaa na matajiri tu mana hata ukienda na Gari ya IST au Vitz hupew parking, Walahi yule mmasai hakupi pa kupaki. Ila wakiona LC 300 hapo wanakupokea na magoti

Mbaya zaidi ukionekana umeenda na bodaboda au bajaji umekwisha, hatihati wasikuruhusu. Lile baunsa lenye upara why lisitoleweee mbona jeuri saana afu Lina miaka mingi kweli pale sijui wanalibembeleza la nini.

Unadharau walimu halafu unataka uonewe huruma, tafuta hela.
 
Unasema washamba lakini haujatembea ndugu yangu.Element haiwezi kufa ndugu yangu. Kuna hotel inaitwa Ledger Plaza Bahari Beach haina watu wengi lakini mpaka kesho ipo. Ndugu yangu sio kuwa na passport tu wanaikagua wanajua huyu mtu yupo level fulani. Usilazimishe kuruka hatua na kutaka kuishi level ambayo haujaifikia. Ukiona unaenda club na kiingilio kinakuuma badili club. Kwa ulichoandika level zako ni za kunywa liquor store (fremu zinazouza pombe). Huu ni ushauri ndugu yangu nilishawahi kuwa hapo ulipo. Wewe imekutokea Element mimi ilinitokea Hongera baa pale Ustawi. Baada ya hapo ndio nikaja kujua inabidi nikazane. Nashukuru Mungu sasa mambo yamebadilika. Mkuu usiumie wala kusikitika we komaa ndugu yangu.Hapo Element sio kwenu au kanisani kwamba ni lazima uende.
Umenikumbusha mbali enzi za hongera bar na ambience club
 
nikweli kabisa jamani mimi ijumaa nilienda na rafkiangu tulibolt bajaji tumefika pale wale walinzi walikua wanatuangalia kwa dharau sana na sio ELEMENT pekeake Club nyingi za masaki wana madharau sana wanamjudje mtu kwa mtu kwa muonekano sana mfano WAVUVI, TIPS,na 1245 oale pananikera kitu kimoja tu kwamba wao ukitaka kuingia club lazima uvae viatu virefu kwa mdada au raba kama ni mkaka bas uvae viatu vya kufunika why???? kwanini wanapangia watu kitu cha kuvaa???? yani hawaruhusu sandles why??? imagine mtu katoka mbali kaja kuhave fun hajui kama kuna mambo ya viatu nashangaa mtu anakataliwa kuingia serius kabisa bora wangemsikiliza kwakua ni mara yake ya kwanza then next time atavaa lakini walimtoaaa nilijiskia vibaya sana kwann????? wanaboa sana
Wanakeraaaaa
 
Back
Top Bottom