Baba lao ofisi ya Utumishi kwa anuani ya katibu mkuu utumishi, utamaliza mwaka au na zaidi hujajibiwa barua. Nimeona ni kupoteza muda kumwandikia katibu mkuu utumishi barua. Ile ofisi ilitakiwa iwe kielelezo bora lakini ni kinyume chake. Mama lao PSSSF, tuko dunia ya digitali umewapelekea mahitaji yote, mwaka unakata unaambiwa wanashughulikia. Zile ni pesa zetu tulizideposit kama tunavyoweka pesa benki, kwanini ku-withdraw au kutoa iwe nongwa? Kama mwanzisha mada alivyosema ole wako umkute mwanamke, wana roho mbaya sijawahi ona. Halafu mnasema wanawake ni waadilifu?