A
Anonymous
Guest
Kuna Wafanyakazi wa Shree Hindu Hospital Arusha ambao wamekuwa wakifanya kazi zao kama kawaida lakini wamekaa miezi miwili bila kulipwa mishahara.
Kinachotia wasiwasi zaidi ni kwamba wanapoulizia malipo yao, baadhi huambiwa, “kama hutaki kufanya kazi, acha kazi.” Hali hii inawaweka wafanyakazi katika mazingira magumu, kwani wana majukumu ya kifamilia, kodi, chakula na mahitaji mengine.
Tunaomba uongozi utoe maelezo ya wazi kuhusu sababu ya kuchelewa kwa mishahara na lini wafanyakazi watalipwa.
Tunaomba pia mamlaka zinazohusika na masuala ya ajira zifuatilie suala hili kwa usiri na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa.
Tunaomba suluhisho, si vitisho. Wafanyakazi wanaomba haki yao kulipwa kwa kazi ambayo tayari wameifanya.