Pre GE2025 Wafanyakazi wa Tanzania badilikeni. Hakuna wa kuwasaidia zaidi ya kadi yako ya kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa hiyo hapa unataka kusema kuwa wafanyakazi hawafanyi kazi kwa bidii ndio maana hawaongezewi mishahara?
suala sio nataka kusema,
ni bayana bidii itakupa faida na maslahi bora zaidi na hutakua na sense ya kivivu ya manunguniko na malalamiko bali kuchapa kazi na kusonga mbele 🐒

hayo ya kwahiyo sijui hivi sijui vile yabaki tu kwa wavivu wanaoweza kurubuniwa kwasabb ya uvivu na tamaa zao 🐒
 
Siku hazigandi !
Mambo yanaenda yanabadilika !
Dhulma huwa nayo ina mwisho wake !!
 
Mimi nasema watumishi wabamizwe tu tena safi sana akili zitawakaa kupitia shida wametumika sana ktk maisha yao ya kitumishi wametumiwa sana na ccm kiasi kwamba imefikia hatua ccm inafanya itakavyo kwa kuwatumia watumishi na wala haiwaogopi na ccm imetumia vizur sana mwanya wa njaa ya watumishi kuwa hadaa na vijisent kidogo kisha wanawahujum wagombea wengine sasa ngoja nao waisome namba akili zitawakaa mdogomdogo
 
KARMA itawazawadia Cardiovascular 🫀 Diseases wale wote wenye Kufanya Dhulma !!
 
WAFANYAKAZI wa Tanganyika hawana UJANJA huo inawezekana hata hata anayewatesa hawamjui
Mbunge anaongezewa mshahara wa mamilioni lakini kumwongezea Mfanyakazi 50,000/= ETI mpaka Uchumi wetu uwe VUMILIVU
 
Wabunge na mawaziri wakistaafu tiyari wamejiwekeza kwa mamishahara na maposho makubwa wanayolipana lkn sisi makabwela tukidhulumiwa kikokotoo tutaishi vipi uzeeni wetu!!
 
Silaha kubwa kabisa ya wanyakazi ni migomo. Tatizo ni mfumo wa kimabavu na rushwa ambao hauruhusu hilo kutokea.
Pamoja na hayo, wafanya kazi wana nafuu ukilinganisha na wakulima ambao wako hoi bin taabani.
Bei za mazao, usafiri, pembejeo na utaalaam ni kitendawili. Acha basi wanavokamuliwa ushuru njiani na sokoni.
Mtu anayeendeshwa kwenye V8 anatakiwa ajihoji hali hali ya wananchi wa kawaida ambao hata chai wameisahau, wengi hata kiporo ni shida. Hawajui supu au mtori wao ni nguna tu na mboga dhaifu mwaka mzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…