Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Landcluser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso. Walikuwa wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo
Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Hanseketwa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe.
Kaimu Meneja wa Forodha wa TRA wa Tunduma, Omary Mnzava amewataja watumishi watano wa mamlaka hiyo kikosi kazi cha fast track waliofariki ajalini leo asubuhi Jumatatu mkoani humo ni Azari Shifonike ambaye ni dereva, Joel Mitondwa, Saidi Buddy, Fahad Hassan na Benard Mashingi.