Wafanyakazi wenzangu wananifanyia figisu nifukuzwe kazi

Wafanyakazi wenzangu wananifanyia figisu nifukuzwe kazi

komaa kaza kabisa..niliwahi kukutana na changamoto kama hizo.....unakuta boss anakuelewa kwa sababu ya uzuri wa vyeti vyako lakini wafanyakazi wenzio hawakukubali.....komaaaaaaaa ikiwezekana shtua sigara kubwa kabla hujaingia kazini😂😂😂
Vipi kamanda hio inasave?
 
Changamoto kazini ni kawaida sana.. la msingi umatakiww kujua mbinu za kukabiliana nazo au kuishi nazo. Kushindwa kwako itakuwa ushindi kwao.. kuwa imara songa mbele.
Ndio natafuta mbinu za kukwepa vitimbwi Mana sio Mara moja.
 
Kazi ipo hapo .Mi badala ya kufundishwa kazi nilikua nabebeshwa mikaa na mikungu ya ndizi mpaka nikatoka mbio mwenyewe.Nachokushauri komaaa nao hao.
 
Mkuu kazini hyo kawaida kila mtu anahisi unataka kuchukua nafasi yake hapo unachotakiwa uwe makini sana na kinachofanyika
Asante sana, Kama vile umeiona . Yani mtu anadhani umekuja kuchukua nafasi yake kumbe sio kabisa
 
Kazi ipo hapo .Mi badala ya kufundishwa kazi nilikua nabebeshwa mikaa na mikungu ya ndizi mpaka nikatoka mbio mwenyewe.Nachokushauri komaaa nao hao.
Ndio natafuta mbinu nikwepe vizingiti, ikiwezekana nisiwe kwenye mawazo yao kabisa.
 
Vipi kamanda hio inasave?
Acha hizo mkuu.. omba ushauri ila sio kila ushauri uutumie.

Usile ganja kama hujawahi kutumia, utahaibu kazi za watu na watapata sababu ya kukuvurugia ajira yako.
 
Hiyo ni kawaida katika maofisi ya kibongo, hasa ofisi zenye fursa za hela.

Inaonekana kuna watu pale wanaona labda utachukua nafasi zao.

Cha kufanya:

Uwe mpole sana. Kama ni mjuaji acha kabisa mpaka utakapoizoea ofisi halafu unaonesha makucha.

Unatakiwa kuchagua moja kati ya haya, la sivyo unaweza hata kuuliwa:

1. Ushikilie dini yako kikamilifu.
au
2. Uende kwa mganga kujizindika. Huku kuna dawa unajizindika, yaani ukirudi kila mfanyakazi anakuona wewe ni mtu mzuri.

Ukiendelea kutulia bila kuchukua hatua, utakuja kurudi hapa na kuleta uzi wa kutimuliwa kazi au umeacha kazi.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru kwa ushauri
 
Habarizenu humu!

Baada ya salamu,naomba niwasilishe changamoto ilionifanya niandike leo, mimi nimuajiriwa kwenye organization ABC, kwa bahati mbaya bado sijakabidhiwa kazi rasmi yaani nipo kwenye kipindi Cha mafunzo, shida iko hapa.

Eneo lakazi nimekuta wafanyakazi wazoefu tu was muda, Kuna baadhi niwazuri was nyoyo lakini wengi e wanakunja kimafanikio, Yani Kuna wengine kabisa nawaona wananitengenezea njia ilimradi niharibikiwe, bosi anione nuksi.

Mda mwingine nipo na mkufunzi wangu wa kazi Mara ghafla anapatwa na hasira, bila sababu, kwa bahati iliyo nzuri wanaonifanyia haya nimewafahamu, tatizo nikuruka vitimbwi vyao ndio nimeshindwa.

Naombeni msaada wenu, mwenzenu kazi bado naihitaji lakini changamoto ndio hio nawezaje kukwepa hivi vizingiti vyao.

Karibuni:
Mara nyingi ukiwa huna tatizo na utendaji katika majukumu yako (kazi zako), huhitaji kuwa na wasiwasi na majungu ya wengine. Labda bosi wako awe hajitambui/hajuwi uongozi. Maeneo ya kazi wanaangalia productivity (maana ndiyo existence ya kampuni), na sio nani anasema nini. Piga kazi kwa weledi, na bosi akibaini hilo, atawazibia pamba masikio wale wote wanaochonga juu yako; hiyo ndio silaha yako.
 
Tatizo boss akiwazibia masikio, wanaweza hata kumuua! Binadamu wa sasa maofisini ni hatari sana!

Kuna ofisi hawaachi maji mezani, kila mtu anatembea nayo mkononi au ananunua maji madogo madogo ya kunywa mara moja.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nilishawai kupata changamoto kama hii ofisini hile ofisi walikuwa wananichukia sijapata ona uzuri nilikuwa the best kwa Boss walifanya kila vibwanga Mimi nikakaza mwisho wa siku walikoma wenyewe na kazi iliwashinda

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom