Kunguru wa Manzese
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 12,729
- 18,119
Kuwa kidaka chozi raha sana lazima utafune
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kakoge maji ya bahari mkuuduh mbona hizo bahati sisi hatuzipati
Ni wiki sasa Maryam ananipigia simu kila siku kila mara akidai anafarijika sana kuongea na mimi baada ya mpenzi wake wa muda mrefu kumtenda. Amekuwa akidai sauti yangu na maneno yangu yaliyojaa hekima na busara yanamtia faraja sana, yaani yanampunguzia machungu ya kutendwa.
Basi kwa siku huchukua takribani saa 1 nikiongea naye kwenye simu mambo mbalimbali ya kijamii,mahusiano na biashara na kidogo sana siasa. Kuchat ndio usiseme kidogo tu sms. Maryam anasema mimi ni mcheshi na mtu mwenye huruma,kitu ambacho mpenzi wake anakosa.
Wewe ndugu msomaji usiwaze ujinga kutaka kunihukumu, mimi sio mpenzi wa Maryam. Kifupi nimegeuka kuwa baba mchungaji wa Maryam.
Majanga yaliyomkuta sio mada, mada ni uwepo wa vijana maridadi tunaofariji wanawake waliotendwa na wanaume wao. Hakika tunafanya kazi ya Mungu na kitabibu kwa wakati mmoja. Taabu ya kazi hii ni pale shetani anapochochea na kukufitina. Hapa ndipo wanawake wengi hutamani kutulipa kwa kazi nzuri tuliyofanya. Hujikuta tunalipwa mapenzi bila kutumia jitihada zozote. Msukumo mkubwa hutokana na hao kina dada tunaowafariji, kutaka faraja kubwa zaidi.
Mtihani mzito kabisa ni pale unapojipa jukumu la kufariji mke wa mtu. Hili ni bomu la nyuklia. Na mimi nasema acha kufariji mke wa mtu labda tu awe ndugu yako na inajulikana hivyo.
Nasema hivyo kwa sababu mfariji wao nilitaka kuingizwa kwenye mtego. Huyu mfarijiwa alifunguka kila kitu ila akaficha kama ni mke wa mtu. Kumbe mumewe mkorofi haishi naye,yupo mkoa jirani. Ikabidi kabla ya kuendelea kumfariji nimchunguze kwanza. Kumbe wakati namfuatilia na mumewe ananifuatilia. Nikanasua mtego.
Kwa wafariji wenzangu mtaniunga mkono kwa kazi nzuri tunayofanya. Wafarijiwa mtakubali zaidi.