Pre GE2025 Wafuasi CHADEMA wavamia nyumbani kwa Mbowe kumlazimisha achukue Fomu ya kugombea Uenyekiti

Pre GE2025 Wafuasi CHADEMA wavamia nyumbani kwa Mbowe kumlazimisha achukue Fomu ya kugombea Uenyekiti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama kweli Mbowe anataka kulinda heshima yake na ushawishi angeachana na habari za kuendelea kuwa mwenyekiti wa hicho chama.

Ikiwa Tundulissu atakubali kumuachia Mbowe uenyekiti wa Chadema kutakuwa hakuna sababu yeye kuendelea Kuwa Chadema.

Machaguo ni mawili kukiua chama Kwa kumrudisha Mbowe au kumpatia Lissu hiyo nafasi ya uenyekiti.

Sioni sababu zozote za Muhimu za Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti.
Kwa kuwa Chama ni cha Baba Mkwe wake, haoni ulazima wa kumkabidhi mtu wa Kuja (Lissu) kukiongoza

Ni hakika anapoteza ushawishi wake wote alioujenga Kwa miaka yote 20 ya Uenyekiti wake
 
Kundi kubwa la vijana wamejazana Nyumbani Kwa Freeman Mbowe mikocheni

Baadhi ya majirani wamepiga Simu polisi Ili kuomba Ulinzi wa Makazi yao

Niko hapa Chato ngoja nielekee nikashuhudie kinachojiri 🐼

==

Mamia ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, wakimtaka achukue fomu kwaajili ya kutetea nafasi yake ya uenyekiti.

View attachment 3179505
View attachment 3179513View attachment 3179514View attachment 3179516
Nani anawalipa hawa!

Kuna cyndicate kubwa inataka kuvuruga amani na utulivu wa nchi sasa naona.

Kwanini nguvu wanazozitumia sasa wasizitumie kwenye sanduku la kura, kama chama hicho ni cha kidemokrasia kweli!
 
Siasa za maji taka za Mbowe hizi, hawa ni bodaboda waliolipwa mafuta 20k na posho 20k kila mmoja na kuandamana kwenda kwa Mbowe, ukicheki kwa makini ni tukio la kupangwa, sbb 99% ni bodaboda na 1% wapiga picha, hakuna wanachama hapo wa Chadema hata mmoja, hao ni bodaboda, hizi ni siasa za kushindwa, ni siasa maji taka, na aibu kubwa kwa Mbowe, mwaka huu Mbowe hana ujanja tena mbele ya Lissu, kabananishwa..!!

Hii ni aibu kubwa kwa Mbowe..!! Mwenyekiti anaekaa madarakani miaka na miaka na hataki kuachia madaraka, huu ni udikteta mbaya sana..!! CCM ndio Chama Bora cha Siasa duniani..!!
 
Huu upuuzi unaondelea ni Mbowe mwenyewe anayeweza kuukomesha vinginevyo atabakia na chawa tu wenye akili wote wataondoka.
Sisi tulishaona siku nyingi inashangaza hadi leo bado kuwa wancdm aisee?
 
IMG-20241218-WA0074.jpg

Kwa mara ya kwanza katika historia ya vyama vingi nchini Tanzània Mwenyekiti wa Chama kikuu Cha Upinzani nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe Freeman Mbowe aungwa mkono na Wafuasi toka Chama tawala Cha CCM pamoja na Wafuasi toka Chama chake Cha CHADEMA.

Freeman Mbowe anaungwa mkono na kundi kubwa toka Chama tawala Cha CCM hata hivyo sababu ya kukubalika kwake bado haijawekwa bayana japo baadhi ya watu wanasema Freeman ni mtu wa watu wote bila kujali Itikadi za vyama vyao.

Hapa Jamii Forum Wafuasi wa CCM hawajabaki nyuma katika kumtete Mwenyekiti huyo aliyedumu madarakani kwa zaidi ya miongo Mitatu akianzia na Uenyekiti wa BAVICHA Taifa mwaka 1993.

Hizi ni baadhi ya Nyuzi za Wanachama wa CCM wakimnadi Mwenyekiti wa mioyo yao Bw Freeman Mbowe

1. Kuelekea 2025 - Tundu Lissu hana karama ya kuongoza chama kikubwa kama CHADEMA, msifanye makosa ya kumpa Uenyekiti
 
Aisee huyu jamaa atawapasua vichwa. sasa naamini Mbowe ni Agent wa CCM. rejea Simulizi ile pendwa.
Kwenye ile simulizi yoga alimtaja huyo Mwamba pamoja na Chama chake, kwamba kinatumiwa na CCM katika kufanya Siasa zake ndiyo maana vinagharamiwa na hao madon wa Chama tawala

Kwahiyo imelazimika Mfumo kuingilia kati ili Lissu asipewe Uenyekiti, maana ana misimamo ambayo Mwenyekiti wake hana
 
Kwa kuwa Chama ni cha Baba Mkwe wake, haoni ulazima wa kumkabidhi mtu wa Kuja (Lissu) kukiongoza

Ni hakika anapoteza ushawishi wake wote alioujenga Kwa miaka yote 20 ya Uenyekiti wake

Ahhh! Inafikirisha Sana 🤗🤗🤗 kiukweli .

Kama ni hivyo ni bora tukose wote Kama Alivyofanya Maalim Seif Kwa CUF.
 
Kundi kubwa la vijana wamejazana Nyumbani Kwa Freeman Mbowe mikocheni

Baadhi ya majirani wamepiga Simu polisi Ili kuomba Ulinzi wa Makazi yao

Niko hapa Chato ngoja nielekee nikashuhudie kinachojiri 🐼

==

Mamia ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe, wakimtaka achukue fomu kwaajili ya kutetea nafasi yake ya uenyekiti.

View attachment 3179505
View attachment 3179513View attachment 3179514View attachment 3179516

kiukweli Lissu anaweza kabisa kuwa Mwenyekiti wa Chadema. Hilo halina shaka ....!

Ila kwa siasa za Tanzania kwa sasa .... Mbowe bado anatosha zaidi.

Siasa kali au za kiharakati zinaweza kuiangusha Chadema kwa kasi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom