Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Wafuasi wa Askofu Mwaikali wasusa ibada Mbeya

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
29,909
Reaction score
32,414
Screenshot_20220619-115148.png

Mbeya. Baadhi ya waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde usharika wa Ruanda, wanaomuunga mkono Askofu Edward Mwaikali aliyeondolewa katika kanisa hilo, wamesusia ibada kwa kile kinachoendelea juu ya mgogoro katika kanisa hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Askofu Mwaikali ambaye sasa ametangaza kuhamia Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki (KKAM), kukabidhi baadhi ya mali za kanisa hilo.

Katika ibada ya leo Jumapili Juni 19, kanisani hapo iliendeshwa na Askofu mstaafu, Dk Israel Peter Mwakyolile ambaye amesisitiza kutubu akisema kuwa wachungaji wametenda dhambi kubwa na waathirika ni waamini ambao hawana hatia.

"Mungu atusamehe sana, Dk Mwaikali na sisi wengine, wachungaji wametenda dhambi kubwa badala ya kutengeneza wamebomoa kwani tumepoteza watu wengi tunaporudi nyumbani tutafakari upya," amesema Dk Mwakyolile ambaye ametokwa na chozi wakati akizungumza madhabauni.

Mwananchi ambayo ilikuwa kanisani hapo, imeshuhudia makundi ya waamini wakiwa baadhi wamekaa kwenye viti nje ya kanisa wengine wakiwa wamesimama kwa makundi makundi wakionekana kupanga mipango yao.

Pia kama haitoshi, wapo ambao walifika kanisani hapo lakini ni kama hawakuelewa mwenendo na kuamua kuondoka kabla ya ibada kumalizika.

Source:mwananchi digital
 
Unahubirije Amani huku unanoa Jambia?

Waumini huwajua sana Viongozi wao na ukiona kwny Nyumba ya Ibada kuna Mgogoro Jua kuna tatizo la msingi ambalo wengi huhubiri kusameheana badala ya kutibu chanzo cha mgogoro


misikiti na Makanisa yenye vyanzo vya Mapato ni kitalu cha ufisadi na ingependeza sana CAG aruhusiwe 'kupita pita'
Mahubiri yanasema tusameheane waamini hawataki kusamehe wanasusa
 
Nyinyi KKT maaskofu wenu na viongozi wengine wa kiroho wasiwe wanaoa.

Askofu anafamilia na amepanga kusomesha watoto wake ulaya na kumnunulia mama watoto gari ya pili nyinyi mnamfukuza. Ni ngumu kukubali sababu hapo anaiwazia familia na pengine anashawishiwa na mama watoto kutokubali kufukuzwa ili aendelee kuitwa mama askofu.

Ni mtazamo tu lakini, Oneni kwa wenzenu Roman Catholic ni amani tu.
 
Hao wananchi wanaomfuata huyo Mwaikali walifuata nini huko kanisani ambapo huyo Mwaikali hayupo?

Si wangeenda kwenye hilo kanisa alipohamia? Wawaache wengine wasali kwa amani?
Namimi nimejiuliza wanafuata nini huko,kwanini wasimfuate Mwaikali wao huko alipo?wanatafuta kuleta vurugu tu
 
Back
Top Bottom