Litakuwa jambo la kusikitisha, kuliko kushangaza ikitokea kwamba Lissu karopok a tu juu ya jambo la namna hii.Msitegemee Lissu ataropoka jambo zito kama hili pasipo kuwa na ushahidi na huenda hata picha za alichokisema teyari anazo sambamba na ushahidi mwingine.
Ikibainika kuwa hivyo ndivyo, atakuwa ameweka uharibifu mkubwa sana kwake binafsi na kwa chama chake.
Hata sioni kabisa faida inayoweza kutokana na habari ya aina hii, kama ni ya kutungwa tu.
Na kwa upande wa pili, ikibainika kwamba kuna ukweli ndani ya habari hii, Magufuli atakuwa ameweka historia mbaya sana ndani ya nchi hii. Hata habari za hii miradi mikubwa inayoendelea, na uigizaji wake wa "uzalendo na kuwajali wanyonge" yatakuwa hayana maana kubwa tena katika 'legacy' yake ndogo aliyokuwa amabaki nayo.
Na kwa upande wa Samia, sasa ndiyo tutajua kwamba kumbe na yeye anatembelea mlemle, kwa kujua yanayoweza kutendwa na mwenye madaraka makubwa kama yeye ndani ya nchi.
Huu mkataba wa Bandari utakuwa ndiyo chanzo cha kufanya yaleyale yaliyofanywa na mtangulizi wake.
Hivi Dotto yuko wapi siku hizi. Kama Samia alijua alishiriki kufanya haya, halafu asimguse kabisa, hicho ni kielelezo tosha kwa ushiriki wa Samia katika mambo haya.