Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 34,954
- 80,256
Huu ni ukweli ambao ni members wachache wataweza kuusema hapa hapa JF kuhofia kutukanwa na kuchukiwa.
Hawa wafuasi hawaaminiki hata kidogo. Support yao mara nyingi imeishia hapa JF na X. Ikienda mbali basi labda IG na Club house.
Juzi wamemsifu Gwajima kwa ujasiri mitandaoni. Lakini sasa hivi Gwajima anapambana mwenyewe. Hawawezi kuingia barabarani na kusimamia wanachokiaminia.
Gwajima sasa kama ni kulala njaa au biashara zake kukwama anayapitia mwenyewe. Wao wanasombwa na kila episode inayotrend. Wameshamsahau Gwajima wapo na Iran na Israel.
Nadhani Mbowe aliligundua hili mapema akaamua kuwa opportunist.
Jiulize Lissu kakamatwa, wakanyimwa ruhusa ya kwenda mahakamani wakatishia wataenda. Wengi hawakwenda. Chama kimefungiwa wanailaumu serikali kumtumia Jaji kutoa hukumu. Lakini hawafanyi lolote. Wapo tu hapa kulalamika na kutishia.
Viongozi kibao kama Mzee Sumaye, Nyalandu walijaribu wakagundua wanajiumiza bure na familia zao.
Hata hii kampeni ya No reforms Oct hutawaona. Mtaji wa mabadiliko ni viongozi wanaopata support kutoka kwa wafuasi.