Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 761
- 6,985
Tukubali kwamba wapo watu katika Hali yakibinadamu wamedhalilika kutokana na namna walivyohudumu awamu ya tano na wanavyopaswa kuhudumu awamu ya sita. Watu hawa walijitwalia utukufu na heshima bandia kwa kinga iliyowekwa na awamu iliyopita ila sasa hivi kinga na heshima vimeondoka.
Kwa muktadha huo lazima watakosa murali wakufanya kazi maana hasira inayowaka miyoyoni mwao Ni kubwa. Baadhi watapretend lakini wengine watashindwa kabisa. Jambo jingine linalowaumiza ni kwamba walitumia muda mwingi kuzima furaha za viongozi wenzao, wakawakatia mawasiliano nakuacha kabisa kushirikiana nao kwa kile walichoaminishwa niwakwamishaji. Leo hii wale waliotengwa wanafuraha hata kama awajateuliwa maana wamerejeshewa Uhuru wao.
Watu wafuatao wamewatesa viongozi na wananchi na sidhani kama wapo tayari kufanya kazi katika awamu ya sita, watu hao baadhi ni Hawa hapa
1. Palamagamba Kabudi - Huyu bwana kitendo cha kuambiwa hadharani kwamba alivuruga Wizara ya Katiba na baadaye kuvuruga mahusiano ya kimataifa kimemtia doa kubwa sana. Kitendo cha kuambiwa alishawishi tubishane na makampuni ya madini kimemvua nguo na kumkumbusha maneno ya Tundu Lissu kwamba taarifa za maprofesa zilikuwa rubbish.
Huyu mtu aliiona nyota yake iking'aa na kujisifu ametolewa jalalani, naamini nyota imezimwa na kwa namna yoyote anapaswa kupewa likizo kwa kipindi flani arudi normal.
Hakuna namna Kabudi atasaidia Taifa liwe na sheria za haki kwa sababu sheria mbovu katunga yeye then kapeleka Bunge la Ndugai kwa ajili ya kupitishwa tu si vinginevyo, Leo anaanza kukubali changes zinazozingatia haki?
Lakini pia ipo hoja ya Katiba mpya, nawaza Kabudi anaanzaje kutusaidia kupata katiba mpya akiwa ni mshauri mkuu wa Rais kwenye sheria?
Inshort Mhe. Rais amezungumza kuhusu katiba ila hakuna namna ambavyo wasimamizi wa sheria alioweka wanaweza kutupatia sheria nzuri kwa sababu wao ndio walioziharibu na wana kiburi za elimu na madaraka.
2. Humphrey Polepole - Huyu kijana ni msomi mzuri na ana makaratasi mazuri ila hana chembe ya uzalendo. Si kiongozi anayeiona nchi bali ni kiongozi anayeona mfumo unaomletea maslahi na mfumo huo ni chama Tawala. Mabadiliko yaliyotokea ghafla yamemfanya ashindwe kumpongeza au kusema chochote kuhusu utendaji wa Awamu ya sita. Kwa kifupi huyu atokaa akubaliane na Rais aliyepo kimtazamo na kimantiki, alishaaminishwa neema inakuja juu yake leo kitumbua kimeingia mchanga. Ana hasira kali isiyoonekana kwa macho
3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali - Kati ya watu wanaopaswa kubeba la ama za mifumo mibaya ya Kodi na sheria kandamizi ni mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hakuwahi kuisaidia nchi na watu wake bali kipindi chote amejikiti kukisaidia chama Cha mapinduzi kutimiza agenda zake. Nafasi hii inahitaji kuwa na mtu anayeliona Taifa kuliko kuiona familia yake,madaraka na chama Cha siasa. Alisaidia kuivuga nchi kimfumo na nivigumu Leo kumpelekea mabadiliko ya sheria au agenda yakatiba akatenda haki. Inshort kwa usomi wake nakiburi cha madaraka hatoweza kukubali kula matapishi yake.
4. DPP - Kati ya Watumishi waliotumia ofisi vibaya tangu kuundwa kwa Taifa la Tanzania ni Biswalo Mganga. Ametia majeraha Taifa na nafsi za watu akitumiwa kutimiza matakwa ya chama na mwenyekiti akiacha pembeni maslahi ya Taifa. Leo hii Magereza yamejaa watu ambao kwa miaka awasikilizwi kesi zao kwa sababu hawana kesi Bali DPP na genge lake walielekezana huyu aozee ndani. Ametesa watu kwa kuwanyima dhamana, ameshindwa kabisa kusimamia haki na Sasa bado yupo ofisini akisubiriwa aanze kutenda haki! No
5. Spika wa Bunge - Huyu ndiyo mwenye agenda za chama. Kinachojadiliwa na kupitishwa bungeni si agenga au hoja za Taifa Bali ni agenda za chama. Kwa kipindi chote cha uongozi wake sheria kandamizi zinazojadiliwa leo mitaani zimepitishwa. Haiwezekani Bunge lipitushe sheria kandamizi bila mkono wa spika. Huyu pia nikikwazo na tukumbuke alivyokuwa anaishi awamu iliyopita si atakavyopraise awamu hii. Ana hasira moyoni tusimwamini kwenye reform ya Taifa letu.
6. Jaji Mkuu na timu yake - Tunajua wazi kwamba muhimili wa mahakama umejichimbia serikalini. Tunafahamu kwamba wapo watu wamenyimwa dhamana na mahakama na mahakama haijawahi hata siku moja kukemea, tunafahamu namna mahakama ilivyotoa uhamuzi kuhusu wasimamizi wa uchaguzi na kesi nyingine za kisiasa. Majaji na mahakimu hawa walioshindwa kujisimamia Leo hii si rahisi wakalisaidia Taifa haki itebdeke. Lazima tukwame.
Hawa watu ukiniambia wanaweza wakasaidia kutekelezwa kwa maelekezo ya jana ya Mhe. Rais tukawa na Taifa lenye amani ntakataa. Tutaendelea kubaki kuwa Taifa lenye utulivu hadi hapo watu wa aina hii watakapoondolewa na tukapata watu neutral kwenye utumishi wa Umma, bunge na mahakama.
Kuendelea kuamini watumishi wa Umma wanatakiwa kutumikia chama cha mapinduzi na si kulitumikia Taifa tutaendelea kusubiri mbadilishano wa Awamu usio na tija kwa Taifa.
Mama fanya mabadiliko ya mfumo mzima, ruhusu katiba inayokubalika kisha 2025 ng'atuka tuachie Taifa lenye nidhamu na historia itakukumbuka wewe na familia yako. Hakuna kiongozi wa kitaifa amemwahi kukumbukwa kwakusimamia maslahi ya chama chake Bali anakumbukwa kwa kusimamia maslahi ya Taifa.