Wafugaji wa kuku unaweza tena inawezekana

Wafugaji wa kuku unaweza tena inawezekana

Hongereni sana, watanzania tuamke tuache kulalamika tukaze buti na Mungu atakuwa nasi

Sawa sawa mkuu. Pia kujiamini kwa kile unachofanya ni nguzo muhimu sana katika maendeleo. Wengi wanatawaliwa na mashaka na kutokujiamini.
 
jamani kuna anaefahamu dawa ya kuangamiza viroboto kwa kuku?

nimejaribu akheri powder lakini haifanyi kazi.

1.Jaribu kutazama muda ma matumizi 2. Waweza kuwapa ile ya kunywa hii ni kwa ajili ya minyoo na wadudu wakaao kwa ngozi ya kuku (keprpmec oral). Pendelea kutumia majivu kunyunyiza bandani/viota kila unapofanya usafi pamoja na hiyo kheri powder ama severin.

kila la kheri
 
hongera mm ss hv nakula mayai ya vifaranga ambavyo nimenunua kwa ss hv nataka kware na bata mzinga

Tunashukuru mkuu, Mungu ni mwema. Mayai unauza sasa au ni ya kula tu? Hivi kesho ndo unakuja kuchukua wale kware na mzinga?

All the best mkuu
 
Asante mkuu kwa taarifa hii muhimu. Hebu naomba unisaidie kujua kitu kimoja; hii glucose huwa inachanganywa na maji kwa kufuata vipimo gani? Naamanisha kiasi gani cha glucose kwa lita ngapi za maji?

Karibu sana mkuu. Glucose haina kipimo maalumu maana si dawa hiyo, ni kwa ajili ya kutia nguvu tu. Waweza kadiria tu i.e vijiko 2/3 vya chakula lita 10 za maji.
 
1.Jaribu kutazama muda ma matumizi 2. Waweza kuwapa ile ya kunywa hii ni kwa ajili ya minyoo na wadudu wakaao kwa ngozi ya kuku (keprpmec oral). Pendelea kutumia majivu kunyunyiza bandani/viota kila unapofanya usafi pamoja na hiyo kheri powder ama severin.

kila la kheri

Mimi walisumbua sana, nkaenda duka la pembejeo wakanambia ku2mia dawa ya kupulizia ufuta (ninja). Cc 2 kwa lita 1 ya maji... Pulizia banda lote wakati kuku hawapo bandani... Pulizia na kuku wenyewe afu nambie kama utasumbuka tena...
 
Washikadau,

Makala muhimu ya UFUGAJI wa KUKU kwa maendeleo binafsi na kwa taifa. Ni wakati wa kuthubutu na kuchukua hatua.
Karibu

Mkuu, inonekana uzi ni mzuri sana ila kuna limit ya kuona na kusoma kwa undani... Nasema hiv kwa 7bu kuna watu wengine cmu zetu haziwezi kufungua pdf. Je unanisaidiaje kwa hili?
 
Mkuu, inonekana uzi ni mzuri sana ila kuna limit ya kuona na kusoma kwa undani... Nasema hiv kwa 7bu kuna watu wengine cmu zetu haziwezi kufungua pdf. Je unanisaidiaje kwa hili?

Asante mkuu, ni pm email yako tukutumie
 
Habari mkuu! kama huto jail naomba unirushie ramani ya banda la kuku, litakalo weza kuwahifadhi kuku 200 tu wa kienyeji.
Natanguliza shukran.
 
Wakuu nimefanikiwa kupata vifaranga vya wiki 3,ili kuwaepusha na maambukizi kupitia maji ya kunywa,niwabadilishie maji ya kunywa kila baada ya muda gani?
 
Habari mkuu! kama huto jail naomba unirushie ramani ya banda la kuku, litakalo weza kuwahifadhi kuku 200 tu wa kienyeji.
Natanguliza shukran.

mkuu ukipata hiyo ramani nami naomba unipatie kupitia pm,shukrani
 
Wakuu nimefanikiwa kupata vifaranga vya wiki 3,ili kuwaepusha na maambukizi kupitia maji ya kunywa,niwabadilishie maji ya kunywa kila baada ya muda gani?

masaa 24 uoshe na sabuni. Ila mie naona huwa wanayachafua hivyo huwawekea asubuhi na jioni wakati nawawekea chakula. Jitaidi yasiingie uchafu ndio kinga ya uambukizo
 
Habari mkuu! kama huto jail naomba unirushie ramani ya banda la kuku, litakalo weza kuwahifadhi kuku 200 tu wa kienyeji.
Natanguliza shukran.

Kiongozi pH 7 , ni pm tujue utapa vipi hio ramani ya banda .
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom