Poultry Sayuni
Senior Member
- Sep 6, 2011
- 125
- 36
- Thread starter
-
- #21
Hongereni sana, watanzania tuamke tuache kulalamika tukaze buti na Mungu atakuwa nasi
jamani kuna anaefahamu dawa ya kuangamiza viroboto kwa kuku?
nimejaribu akheri powder lakini haifanyi kazi.
Mkuu Sayuni hapo kwako una ile mbegu ya kuku wa kienyeji aina ya Ching'wekwe ambayo inaaminika kuwa na asili ya kutaga mayai mengi zaidi?Asante!
hongera mm ss hv nakula mayai ya vifaranga ambavyo nimenunua kwa ss hv nataka kware na bata mzinga
Asante mkuu kwa taarifa hii muhimu. Hebu naomba unisaidie kujua kitu kimoja; hii glucose huwa inachanganywa na maji kwa kufuata vipimo gani? Naamanisha kiasi gani cha glucose kwa lita ngapi za maji?
Aisee hiyo mbegu hatuna, tunatazama pande mbili zaidi yaani mayai na nyama pia
1.Jaribu kutazama muda ma matumizi 2. Waweza kuwapa ile ya kunywa hii ni kwa ajili ya minyoo na wadudu wakaao kwa ngozi ya kuku (keprpmec oral). Pendelea kutumia majivu kunyunyiza bandani/viota kila unapofanya usafi pamoja na hiyo kheri powder ama severin.
kila la kheri
Washikadau,
Makala muhimu ya UFUGAJI wa KUKU kwa maendeleo binafsi na kwa taifa. Ni wakati wa kuthubutu na kuchukua hatua.
Karibu
Mkuu, inonekana uzi ni mzuri sana ila kuna limit ya kuona na kusoma kwa undani... Nasema hiv kwa 7bu kuna watu wengine cmu zetu haziwezi kufungua pdf. Je unanisaidiaje kwa hili?
Karibu mkuu. Umeshaandaa banda sasa ili tukuwekee oda yako kabisa!!!!
Habari mkuu! kama huto jail naomba unirushie ramani ya banda la kuku, litakalo weza kuwahifadhi kuku 200 tu wa kienyeji.
Natanguliza shukran.
Wakuu nimefanikiwa kupata vifaranga vya wiki 3,ili kuwaepusha na maambukizi kupitia maji ya kunywa,niwabadilishie maji ya kunywa kila baada ya muda gani?
masaa 24 uoshe na sabuni. Ila mie naona huwa wanayachafua hivyo huwawekea asubuhi na jioni wakati nawawekea chakula. Jitaidi yasiingie uchafu ndio kinga ya uambukizo
mkuu ukipata hiyo ramani nami naomba unipatie kupitia pm,shukrani
mkuu ukipata hiyo ramani nami naomba unipatie kupitia pm,shukrani