Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

Wafugaji wa mbwa kibiashara au ulinzi tukutane hapa

kapicha mkuu
Welchcorgipembroke.JPG
 
GT shukran kwa huu uzi. Am a dog enthuast. Kuna huyu mbwa wanadai ni mpole na mjinga Labrador. Yani hata intruder akingia ndani atamsindikiza. Ni breed inayoendana na retrievers
mkuu najua wewe unaishi na jamii inayojali mbwa kuliko hata viongozi wa bongo wanavyojali watu wao, nimeishi na Wascandnavia nikiri ndio walioniambukiza ugonjwa wa kupenda mbwa hasa wa Dk, hebu tupe uzoefu wako mkuu
 
Hawa Koko kwa ajili ya kama alarm tu si unajua koko akiona mtu lazima abweke so ni njia nzuri ya kustukia wezi.....Ngoja nizichange nije kufuga hao GS niachane na KOKOBANGA NYE NYE NYE.
dah GT iyo mijibwa koko inakulindia magunia ya mkaa huko minjingu? Halafu mioga na ina mikwara kwa kubweka yani hata ukiinama kufunga kamba za viatu zinatimua wakidhani unaokota mawe kuwarushia
 
dah GT iyo mijibwa koko inakulindia magunia ya mkaa huko minjingu? Halafu mioga na ina mikwara kwa kubweka yani hata ukiinama kufunga kamba za viatu zinatimua wakidhani unaokota mawe kuwarushia
Hahahaaaaaa Mzee wa KOPENIHAGENI 😀😀😀😀😀 Naifuga kwa ajili ya kama kutishia watu na Alarm ya kukustua kama kuna watu wamekuja au kuiba magunia ya mkaa.
 
mkuu najua wewe unaishi na jamii inayojali mbwa kuliko hata viongozi wa bongo wanavyojali watu wao, nimeishi na Wascandnavia nikiri ndio walioniambukiza ugonjwa wa kupenda mbwa hasa wa Dk, hebu tupe uzoefu wako mkuu
Mkuu mbwa huku ni mwanafamilia. Ana hadi kitambulisho. Ila kati ya vitu wazungu wamekosea ni viwili tu ni kushabikia ushoga na kumtukuza mbwa. Siyo vizuri mbwa kulala naye kukaa naye ndani. Napenda mbwa lakini kumtukuza kiasi hicho hapana.

Kuna huyu the biggest dog the great dane yani jibwa kubwa sana ni german breed
 
gd ni bonge la mnyama, naweza kusema ni cross ya gs.
mkuu wenzetu wsmezidisha upendo sana kwa dogs
 
gd ni bonge la mnyama, naweza kusema ni cross ya gs.
mkuu wenzetu wsmezidisha upendo sana kwa dogs
kuna dogo flani mwafrika kutoka italy nilikutana naye siku flani mtaani akiniomba nimfanyie konekshen ya kubeba boksi. Tukapoteleana. Baada ya muda nikawa namuona akiwatoa out mbwa wawili golden ritriever siku nyingine nikamuona wakiwa na mmama wa kizungu na mijibwa yao nikajichekea tu nikasema dogo tayari kashawekwa ndani
 
ikiwa ataonyesha upendo kwa madog tayari ameula
 
Ngoja niwape kisa kilimtokea family friend mmoja mwaka 2015 msimu wa xmass na mwaka mpya.

Jamaa alikuwa na GS wako nane. Kawaida huwapa msosi kila siku usiku mida ya saa 4 baada ya watu wote kuingia ndani maana ni wakali mno. Na zoezi la chakula kuna shamba boy huwa ndie anawahudumia mbwa.

Sasa shamba boy xmass alienda kwao kula sikukuu. Na family friend yeye ni mtu wa tungi sana huwa anakesha baa na wajomba zangu.

Siku shamba boy alipoondoka jamaa akawa amelewa zake akarudi home akapitiwa akalala (mbwa hawakupewa chakula kama kawaida).

Akaamka asubuhi akaandaa msosi vizuri akafungulia banda la kwanza. (Amewagawa katika mabanda mawili wanne wanne).

Baada ya kufungua banda la kwanza mbwa mmoja akaanza kumkoromea kwa hasira sana kisha akamrudia, wale wengine watatu nao wakamrukia wakaanza kumrarua kwa hasira, wale wengine ndani nao wakapandwa na wazimu mpaka wakavunja banda wakaungana na wenzao.

Mke wa jamaa ni mayowe tu kwa dirishani anashuhudia mumuwe anavyotafunwa bila kuwa na lakufanya. Watoto vilio mpaka majirani wakasogea karibu.

Bahati nzuri kuna mtoto wa jirani ni rafiki wa shamba boy na mara nyingi wakiwa wanalisha mbwa wanakuwa wote hivyo wale mbwa wamemzoea sana.

Basi dogo ndio kuingia pale akawatuliza mbwa na jamaa kukimbizwa hospital ambapo alilazwa miezi mitatu akiwa hana fahamu.

Kusema ukweli yule jamaa kama angekuwa kapuku wala asingepona kwa shambulio lile. Pesa ilimuokoa.

Baada ya kurudi uraiani alikuwa amefungwa POP miguuni wala kutembea bila magongo hawezi. Aliwatandika risasi mbwa wote na mpaka sasa sijui kama anafuga tena.

Mbwa ni Loyal Friend kuliko hata binadamu lakini ni hatari sana pia.

Wafugaji tuzingatie Terms and Conditions

[emoji190] [emoji240]
Asante kwa story lakini naomba ukaulize upya type ya mbwa wake. GS hawana hizo tabia na thats only reason nawafuga na siyo upuuzi wa pitbull,doberman na ma rottlewellers.
 
Hiki kisa cha kweli huko uingereza karne kadhaa. Kuna jamaa alipata mapacha na mama yao kufa. Wakawa wanalelewa na na nanny. Jamaa alikuwa na mbwa nimesahau breed alikuwa muaminifu kweli huyu mbwa. Na ikatokea hakai mbali na hawa mapacha. Mara zote hako nao.

Kuna siku aliondoka akamwacha mbwa na nany. Ila yule nany alitoka. Jamaa kurudi nyumbani akakuta kitanda cha watoto kimeanguka na mashuka yamezagaa yana damu na mbwa wake akimkodolea macho kwa ghazabu akachukua upanga na kumchoma mbwa wake huku mbwa akimtazama kwa huruma machoni akifa.

Baada ya hapo kugeuka akasikia madogo wakilia na pembeni bonge la mbwa mwitu wolf limekufa.

Jamaa alilia kwa sauti na kujuta kwa nini alimuua mbwa wake. Alimzika nakuweka mnara kwenye kaburi la mbwa hadi leo lipo. Kati ya wales skotlend sina uhakika

Sky Eclat
 
Back
Top Bottom