Hiki kisa cha kweli huko uingereza karne kadhaa. Kuna jamaa alipata mapacha na mama yao kufa. Wakawa wanalelewa na na nanny. Jamaa alikuwa na mbwa nimesahau breed alikuwa muaminifu kweli huyu mbwa. Na ikatokea hakai mbali na hawa mapacha. Mara zote hako nao.
Kuna siku aliondoka akamwacha mbwa na nany. Ila yule nany alitoka. Jamaa kurudi nyumbani akakuta kitanda cha watoto kimeanguka na mashuka yamezagaa yana damu na mbwa wake akimkodolea macho kwa ghazabu akachukua upanga na kumchoma mbwa wake huku mbwa akimtazama kwa huruma machoni akifa.
Baada ya hapo kugeuka akasikia madogo wakilia na pembeni bonge la mbwa mwitu wolf limekufa.
Jamaa alilia kwa sauti na kujuta kwa nini alimuua mbwa wake. Alimzika nakuweka mnara kwenye kaburi la mbwa hadi leo lipo. Kati ya wales skotlend sina uhakika
Sky Eclat