SoC03 Wafungwa kabla ya kutoka gerezani waandaliwe kisaikolojia

SoC03 Wafungwa kabla ya kutoka gerezani waandaliwe kisaikolojia

Stories of Change - 2023 Competition

FIKRA NASAHA

Member
Joined
May 22, 2023
Posts
14
Reaction score
47
wkg.jpg

Ni Kupunguza Wimbi la Kurejea Kwenye Uhalifu

Kila Mwaka, Tunaposheherekea Sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania), Ambaye Pia ni Amiri Jeshi Mkuu, Hutoa Msamaha wa Wafungwa, Kwa Idadi Inayopendekezwa na Magereza, Nchi Nzima Ikiwa Pia Sehemu ya Kupunguza Msongamano wa Wafungwa Magerezani.

Idadi ya wafungwa wanao samehewa inaweza kuwa kubwa au ndogo. Wanaonufaika na msamaha wa Rais ni pamoja na wale waliokuwa wakitumikia kifungo kisichozidi mwaka mmoja na wale ambao wamekuwa wakitumikia vifungo vya muda mrefu lakini wamebakiza muda usiozidi mwaka mmoja kumaliza vifungo vyao au ni wagonjwa.

SWALI la kujiuliza, je hao wafungwa, wametayarishwa kuja kukabiliana na hali halisi ya kimaisha uku uraiani, baada ya kukaa miaka kadhaa huko Magerezani?

Kama vile askari wanaotoka vitani, kabla ya kuja uraiani, kwanza upitia kwenye vipimo vya kisaikolojia ili kuondokana na ile hali ya Post-traumatic stress disorder (PTSD), ili kuwawezesha waweze kuishi vyema na raia na kuondoa ile hali ya woga, dhiki na mashaka na mihemko ya kiakili na kuwapunguzia kama si kuwaondolea kabisa zile kumbukumbu mbaya walizopitia vitani.

Matayarisho hayo uwawezesha askari, kukabiliana na maisha ya uraiani kwa amani na kuepuka kufanya uhalifu au hata kuwadhuru raia kutokana na matatizo ya kiakili walioyapata vitani.

Hata kwa wafungwa haswa wale wa muda mrefu na wale ambao uhalifu wao ulitokana na kudhuru watu wengine kama vile mauwaji na ubakaji na jinai zingine. Hao wote baada ya kutumikia kifungo kwa muda mrefu, ujikuta wanakuwa wageni na maisha ya uraiani.

Ukizingatia kwamba jela nyingi Kiafrika, zimejaa uonevu na kuoneana haswa miongoni mwa wafungwa wenyewe kwa wenyewe na kesi zingine zinaripotiwa kuwa baadhi ya wafungwa wananyanyaswa kingono, mapigano baina ya wafungwa, na vitendo vingine vya ukatili ni kawaida katika magereza mengi.

Lakini hali hii sio tu kwa wafungwa hata walinzi wao (askari Magereza) hufanya kazi katika mazingira yenye dhiki kubwa ambayo inapelekea kuongeza uwezekano wa wafungwa kuteswa bila ya sababu za msingi.

Na haswa wafungwa wa kike, wapo katika hatari kubwa ya kushambuliwa kingono na walinzi wa Magereza.

Wengi wao (wafungwa) hata kutembelewa na ndugu, jamaa na marafiki ni kwa nadra sana, kiufupi wafungwa wengi wanakuwa wametengwa na jamii kwa asilimia kubwa sana. Kutengwa huku kunaweza kuongeza hatari ya mfungwa kukosa afya ya akili kama vile unyogovu na wasiwasi (depression and anxiety).

Hali hii upelekea wafungwa wengi kuathirika kisaikolojia (kimwili na kiakili) na kujikuta wanabadilika kitabia. Na kupelekea wengi wao kuona kuwa wametengwa na jamii kutokana na makosa waliyo yafanya uko nyuma, na hii uwapelekea wengi wao kukosa subra na hata kuwapelekea kutumia nguvu kupata kile wanacho kitaka na hata kurudia tena kufanya jinai (makosa waliyo yafanya kabla ya kwenda jela) kwao uona ni jambo la kawaida.

Takwimu za kimataifa zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wafungwa waliotoka jela, ukamatwa tena ndani ya miaka mitatu, kama si miezi michache tu.

Ushauri unaotakiwa kufuatwa ni kuwatumia Wataalam wa afya ya akili (A mental health professional) kuwasaidia wale wote waliotoka jela.
Mtaalam anaweza kusaidia wafungwa kurudi tena katika jamii (Uraiani) na kurejesha tena uhusiano mzuri kati ya na ndugu, jamii, marafiki pamoja na familia husika.

Bila ya kusahau kuwapa elimu ya kimaisha na hata ujuzi wa ujasiliamali, ili wanapotoka basi waweze kujitegemea na wafatiliwe mienendo yao kwa hao wafungwa kufanyiwa rokoo kila wiki au kila mwezi na kujuwa maendeleo yao, kitabia huko uraiani.

Bila ya kuwaandaa hao wafungwa, tusishangae kusikia wengi wao wamerejea kufanya jinai na uhalifu ule ule au zaidi ya ule na kurejeshwa tena Magerezani.​
 
Upvote 3
umeandika vyema kabisa lakini ukipata muda mzuri pata wasaa wa kuongea na hao wafungwa wenyewe wakupe sababu za wao kurudi jela mara kwa mara

pili hakuna unyanyasaji wa kingono kwa wafungw wa kike maana magereza yao wanahudumiwa na askari wa kike tu kuanzia ulinzi mpaka huduma zote za ndani

askari wa kiume hawaruhusiwi kulinda gereza la wanawake wala kutembea na mfungwa kike na hata kumsimamia kazi mfungwa wa kike analindwa na kusimamiwa na askari wa kike tu
 
Tumalize kwanza la bandari kiongozi
 
Back
Top Bottom