Yeah ipo tofauti. Mganga maana yake ni tabibu, Doctor. Hao matabibu wanatoa tiba kwa mtindo tofauti tofauti.
1.Wale waliosomea, MD na wanatumia vifaa na njia zinazo kubalika na mifumo, ktk mitaala mbalimbali.. Kumbuka Tiba inayotolewa humu yaweza kuwa ni Extractions au mavuno ya vitu vya asili viliwekwa ktk dosage na mtindo mbalimbali ya kitaalamu, chemikali za kutengenez, mionzi n.k
2. Kuna wale wa asili, tiba mbadala. Hawa sasa wengi wanatumia elimu walizo jifunza kutoka ktk tamaduni, kuwa miziz flan au gome fulani au njia fulani inaweza kutibu kitu fulani. Hao ukifatilia dawa zao na ukizichek pia sayansi inaweza thibitisha. Wanaweza kukutaka ukapimwe kisha uende kwao ukiwa na hakika na ugonjwa gani. Tiba zao sio za kiimani,ingawa kuna wengine wanaongozw na imani,lakin ukifatilia dawa zao unawez pata Uthibitisho wa kisayansi..
3. Kuna kundi hili la mwisho, ambalo tiba zina ambatana na imani, vipimo vya ugonjwa ni ramli, tunguri. Tiba zao ni imani, huamini sana ktk chanzo cha magonjwa kuwa ni nguvu za giza . Humu pia wanachangany na mifumo ya tiba ya number mbili. Ila vyanzo vya kujua shida, ugonjwa hadi tiba yatokana Mapepo ya utambuzi.
Unaumwa kichwa, unachanjwa Chale,unapakwa dawa au unafukizwa wanasema umepona . Na unaondoka umepona kulingana imani yako , lakin ndio kuna kukamatwa nafsi yako.