wakuu hebu tusaidiane.
waganga na wachawi ni wakala/agents wa ibilisi/shetani
kwanini wanapingana
mchawi anakuroga ufe, mganga anakutibu usife
cc rakims
ccmshanajr
walker water
Wanachezewa Mchezo smart bila wao kujua. Ni wachawi wa Higher rank au waganga wa higher rank ndio wanajua game nzima ya mchezo.
Ila walio wengi wanajua kuna ka uadui fulani baina yao, ni kama unavyoona Simba na Yanga, huku chini washabiki wanachukulia hayo mambo serious,lakn walio top wanaona ni mbinu ya mchezo.
Mchawi ni nani?? Mganga ni nani??
Mchawi ni mharibifu tu, mafunzo yake na mind yake imekuwa conditioned kuujenga ufalme wa giza kwa njia ya kuharibu , kufunga na kuvuruga. Haijalishi nguvu zake au maagano yake, tools zao zote zinafanya kazi hiyo. Huyu namchukulia kama RUNGU.
Upande wa Mganga huyu ni mharibifu na mtengenezaji. Yaani mchawi aliye ongezewa maarifa ya kutibu pia. Neno kutibu sio lazima limaanishe kuweka Huru. Huyu ni kama Nyundo inayo weza kugonga na kuchomoa misumari.
Hawa jamaa wana bargain, wanatengeneza madili, kwamba huyu usimponyeshe, huyu tuachie wa kwetu, tutakupa fedha etc . Sametimes waganga wenye maarifa hutumiwa na wachawi kufanya uchawi na kuroga. Huko ni ktk kucheza game yao kuwa yenye kuwachangamsha.
Ikifika ktk mambo halisi ya kuugusa utawala wao, wote wanafanya kitu kimoja. Hufanya vikao vya usiku, hupewa assignment ya kuleta matokeo fulani.
Si unao simba na yanga ikifika ktk jambo la Nchi, wanaitwa na mamlaka kuu na wanacheza pamoja tena fresh kabisa.
Unapo enda kwa mganga, huko unasajiliwa kama hospital wanavyo kusajili, isipokuwa tu waganga wanachukua Adress zako za Rohoni ,wakipewa assignment kukuhusu au wakitaka fedha ay kitu kwako wanakuchangamsha tu.
Msihadaike, hakuna mwema kati yao, wanakuhamisha tu office ya kifungo na umiliki, MUNGU ndio true healer na Savior.