Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Mimi nimekaa nchi za ulaya pia nimekaa ugiriki hakuna nchi watu wake jambo dogo tu badala ya kutukanana wao wenyewe Wanamtukana Mungu vibaya sana. wale wamelaaniwa wao na taifa lao.
 
Huyu jamaa alikua mtu mbadi sema tu hakuwa kwenye mainstream
Wanamkuza Thomas Edison wanamsahau Nikola Tesla kisa tu alikua sio raia wa marekani ukizingatia Edison alikua anatumia Ideas za Tesla maana kioindi hiko toka mwaka 1884 Tesla alikua kaajiliwa kwenye kampuni ya Thomas Edison. Hawakuishia tu kutumia ideas zake lakini pia wakati anafariki mwaka 1943FBI walichukua Docs zake zoote zikapelekwa kufanyiwa kazi.

Tumfahamu
NikolaTeslaAlizaliwa ulaya mashariki kwenye nchi ambayo leo ni Croatia/Serbia Tarehe 10 jully 1856 Kipindi ambacho kulikuwa na option mbili tu Kujiunga na Jeshi au dini. Baba yake alikuwa ni Mchungaji wa kanisa na mama yake alikuwa mama wa nyumbani. Alilazimishwa kujiunga na kanisa lakini alikataa hakuwa tayari. Mama yake kakuwahi kwenda shule lakini alikuwa na talent ya kushona na uwezo mkubwa wa kukariri mashahiri vitu vilivyomfanya mtoto Tesla kuvutiwa sana.Vitu hivi vilimfanya kuwa na uwezo wa kusovu hesabu ngumu za Calculs

Akiwa mtoto mdogo aliposoma kuhusu mapolomoko ya niagara marekani kichwani mwake aliona Gurudumu likizunguka katikati ya maji. Kwa immagination na meditation akajakuwa founder wa umeme wa maji miaka mingi baadae alipofika hilo eneo.
Kuna kipindi akiwa chuo alikuwa akisoma kuanzia saa tisa usiku hadi saa tano usiku mfululizo. Hadi siku moja akiwa nyumbani akakuta barua ya siri ya proffesor akimuandikia baba yake wamrudishe nyumbani maana akiendelea atafariki.
(Unzaweza kutafuta ukamsoma zaidi maisha yake coz sitaki tujadili kuhusu maisha yake)

Huyu jamaa alikua kichwa ukisikia kichwa kweli kichwa kavumbua vitu kama..

AC motor
Carbon button lamp
Death ray
Induction motor
Plasma globe
Plasma lamp
Polyphase system
Radio control
Resonant inductive coupling
Rotating magnetic field
Teleforce
Telegeodynamics
Teleoperation
Tesla coil
Tesla's Egg of Columbus
Tesla Experimental Station
Tesla's oscillator
Tesla turbine
Tesla valve
Torpedo
Vacuum variable capacitor
Violet ray
VTOL
Tesla Tower
Wireless power transfer
World Wireless System

Unajua kila mtu anapozaliwa hua anakua na Huruma,Upendo na Kujali kwa jumla tunaita Wema (Kindness ). Sasa huyu jamaa ndio alivyokua, alijua Dunia anayoishi ni kitanda cha Waridi( Bed of roses) kumbe sio, Dunia imejaa simba na mamba wakali wenye njaa ambao wako tayari kumtafuna mtu yoyote ili wao wajipatie manufaa. Mpango mkuu wa Nikola Tesla alikua anafanya kila uvumbuzi wake ili kumrahisishia binadam maisha bila kutegemea faida yoyote. Mfano mpango wake mkee alikua anataka Dunia nzima tupate umeme bure bila kupitisha mawaya mitaani wala nini yaani unafungwa tu mtambo ambao unawasha Umeme majumbani Wirelessly Dunia nzima.
Ila watu waliona huyu mbaya atawakosesha pesa Ukizingatia serikali ya Marekani ilikua imewekeza kiasi kikubwa kum-finance Raia mzawa Thomas Edison kwenye project hizo za umeme.

Kifo Chake na FBI.
Mwaka 1937 Nikola tesla alitoka kwenye chumba chake namba 3327 kilichoko kwenye hoteli ya new Yorker, akaelekea kanisani kisha maktaba hii ilikua ratiba yake ya kila siku. Wakati anavuka barabara aligongwa na taxi za enzi hizo na kurushwa pembeni, alivunjka mbavu tatu na kuumia kwnye uti wa mgongo. Bahati mbaya hakwenda ata kumuona daktari akatulia hivo hivo na maradhi yake inasemekana ajali hiyo ilimsababishia kua na matatizo ya kisaikolojia. Baada ya ajali hio tesla alitumia muda mwingi kukaa ndani ya chumba chake kilichopo ghoofa ya 33 chumba namba 3327 .


Nikola Tesla alikutwa amefariki ndani ya chumba chake na mfanyakazi wa hotel Tarehe 8 January 1943 saa 10:45 Pm.
Muhudu alimwita Daktari ambapo alikujua kuchunguza mwili na kutoa taarifa kua marehemu alikua muda mfupi tu uliopita, ikagundulika kua Kafariki kwa ugonjwa wa coronary thrombosis ambao unasababishwa a Damu kugandia kwenye mishipa ya kupitishia damu hivyo kupelekea Moyo kishindwa kusambaza damu mwili mzima

Punde tu baada ya kifo cha Nikola Tesla serikali ya marekani ilienda kuchukua Documents/Paper zote zilizokua zina maelekezo,Michoro na design ya project mbalimbali alizokua anazifanyia kazi. Kutokana na asili ya kazi za Tesla zilivyo Director wa FBI kipindi hiko J. Edgar Hoover alisema zile Documents zilikua Top Secret Maana ofisi inayoitwa "Office of Allien" ndio walipewa mamlaka ya kuchukua Documents zote zilizobakia za Tesla.

Serikali ilimwajili Injinia Dr. John G. Trump mjomba wake na raisi wa marekani wa sasa kupitia Karatasi zote zilizopatikana ili kuona kama zilikua zina thamani kiasi gani.
Mpwa wake Tesla aitwae Sava Kosanovic alijaribu kuomba serikali apewe vitu vilivyoachwa baadhi ya vitu binafsi alipewe vikapelekwa kwa familia , Kosanovic alienda mahalamani kutaka apewe na Files zote za mjomba wake baadae mno alishinda kesi akapewa haki ya kumiliki vitu vyote vya Tesla Documents/Files zoote. Files zote zilitumwa Belgrade, lakini kati ya files 80 zilifika files 60.

Ifike muda Huyu mtu apewe heahima yake stahiki kama ilivyo kwa Thomas Edison..
 
Angalau hapa nimejua Tesla alikuwa na akili. Sisemi kwamba Yesu hakuwa na akili, ila kutokana na Ukristu wangu, namuona alikuwa wa kawaida tu, ila umemuweka kuwa kati ya waliokuwa na akili sana duniani.
 
Angalau hapa nimejua Tesla alikuwa na akili. Sisemi kwamba Yesu hakuwa na akili, ila kutokana na Ukristu wangu, namuona alikuwa wa kawaida tu, ila umemuweka kuwa kati ya waliokuwa na akili sana duniani.
Tesla kasaidia sana kwenye masuala ya umeme. Wireless zote hizi kagundua yeye bila figisu za wafanya biashara leo hii tungekua tunatumia umeme wa wireless tena kwa ghalama kidogo.
Btw hiyo ni orodha yangu tu kutokana na muono na mapenzi yangu juu ya watu hao...
 

Yesu sio Mungu tena[emoji81][emoji81][emoji81][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Huyo yesu ana akili gn au kafanya kipi kumuona ana akili sana kushinda manabii wenzake
 
Wanajeshi wa ugiriki (Sparta) walijulikana kama Hoplites, ambapo hoplites walikua wanajeshi wenye ngao ya duara,mkuki na upanga mfupi wa chuma. Kwenye vita walikua wanatumia mfumo wa vita unaofahamika kama phalanx ambapo hoplites alikua anasima mbele ya mwenzake kisha anatumia ngao yake kujilinda na kumlinda mwenzake kama likitokea shambulio la mbele. Kama phalnx ikivunjika au adui akishambulia kutoka upande wa kushoto au kulia basi inakua hatarii zaidi kwa Hoplites
Mwanzoni mwa karne ya 5 BC nchi ya Persia ilikua inafanya uvamizi nchini ugiriki ,lakini jeshi lile la vile vimiji zaidi ya mia vilivyoungana kijeshi viliirudisha nyuma jeshi la Persian lilipotaka kuvamia katika vita inayojulikana kama Battle of Marathon ilikua mwaka 490 B.C chini ya mfalme Darius I wa Persia . Miaka kumi baadae mtoto wa Darius aitwae Xerxes I (519-465 B.C.), kwa mara ya pili alianzisha uvamizi nchini Ugiriki.

Chini ya mfalme Xerxes I, jeshi la Persian lilivamia ugiriki kupitia pwani ya mashariki akishirikiana na jeshi la maji la Persian lililokua linapita pwani. Ili kufika sehemu walipokua wanaeleka katika eneo linaloitwa Attica ambapo pia attica ilikua ni mji unaoongoozwa na Athens, Jeshi la Persia ilitakiwa lipite sehemu moja ya pwani inayoitwa Thermopylae (au “Hot Gates,” ilijulikana hivo kwakua ilikua karibu na chemichemi ya sulfur). Katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 480 B.C., Leonidas alikua anaongoza jeshi la wat 6,000 mpaka 7,000 kutoka miji mbalimbali iliyopo ugiriki ukijumuisha na wanajeshi 300 kutoka katika mji wake wa Sparta Aliongoza jeshi hilo kuziwia jeshi la Persia kupita ile sehemu inayoitwa Thermopylae.

Wananchi wa Sparta walikua na miungu yao walioiabudu, kulikua kuna mtu ambae alikua kama nabii wao ambae alikua anawapa maagizo wananchi kutoka kwa miungu hiyo. Kabla ya kwenda vitani Leonidas alienda kuonana na huyo nabii ili ampe maono kuhusu vita hiyo anayokwenda kupambana, nabii alimkataza kua asiiende atapoteza maisha ya wengi ni bora ajislimishe kwa jeshi la Persia, leonida alikata kata kata kua hataweza kujisalimiisha lazima akawaziwie pale kwenye hot gate, walimsihi sana na kumshauri lakini alikataa na kuituna miungo yake
Leonidas aliongoza jeshi lake hadi pale hotgate akiamini kua jeshi la Persia lazima lipitie pale alipambana nao na kuwaua wanajeshi wengi wa Persia kisha akajenga ukuta kwa kutumia maiti za wale wanajeshi.

Leonidas akiwa hajui kumbe jeshi lingine lilipita njia inayopita milimani hivyo wakatokezea nyuma ya jeshi la leonida, baada ya kugundua hilo makamanda walimshauri kua ni bora wajisalimishe maana washazungukwa ila Leonidas alikataa kabisa akasema sharia ya nchi ya Sparta hairuhusu kujisalimisha ni bora afe pale. Makamanda kutoka ile miji mbalimbali walichkua majeshi yao na kumuacha Leonidas akiwa na wanajeshi 300 tu!
Akiwa na wanajeshi 300 tu Leonidas alipambana na jeshi la zaidi ya watu 15000, mwisho alizidiiwa na kuuwawa..walimkata kichwa .
 
Angalia hii clip ya waafrika wa enzi hizo wakifanya surgery ya kichwa.
 
Kingine wagiriki walipenda Sana Ngono licha ya kua na maarifa ila ikija kwenye swala la kunyanduana walikua balaa Sana,mbaka Sasa ugiriki ndio Nchi inayoongoza Sana Kwa raia wake kufanya Ngono wakifuatiwa na warumi wa Italiano!
 
Watoto n wazuri Ila madume ni nothing hayajui mishe
 
Kuna muda huwa najiuliza elimu tunayosoma ndo inashida au sisi tunaofunza na kufunzwa ndo tunashida kama through archimedes principle and law of flotation watu wameunda meli na vitu vingi vinavyoelea, kwa nn sisi tunashindwa kufanya gunduzi kubwa na za kipekee zaidi duniani badala ya kuendelea kulalamika juu ya wakoloni na walivyotufanyia.
 
Aisee Kumbe inawezekana kuna Waafrika ambao wangeweza kugundua vitu vikubwa shida ni mifumo yetu kandamizi.
 
misri waligundua vimini na vitop...dada zangu mpoooo 😉 😉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…