Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Wagiriki nini kiliwakuta? Sasa hivi hamna tena Wagiriki wenye akili kama zamani?

Ahsante kwa kunijuza!
Ila ningependa kuuliza pia, historia inaonyesha kwamba upasuaji ulianzia misri, maana vifaa vya upasuaji vimegunduliwa huko!
Je wao walitumia nini wakati wa kufanya upasuaji?? Au ndio ilikua live bila ganzi, Ningependa kujua historia ya upasuaji maana sifahamu sana maswala ya utabibu
Ninavyotambua upasuaji ulianzia Japan na India. Wahindi walitumia pombe na bangi kumfanya mgonjwa alale. Mgonjwa alipewa pombe anywe kwenye chumba ambacho bangi iko kwenye kigae cha moto. Mara nyingi wagonjwa waliamua kabla upasuaji haujaisha.
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Huu udini sasa, yule wa kwetu hana akili?
 
Ninavyotambua upasuaji ulianzia Japan na India. Wahindi walitumia pombe na bangi kumfanya mgonjwa alale. Mgonjwa alipewa pombe anywe kwenye chumba ambacho bangi iko kwenye kigae cha moto. Mara nyingi wagonjwa waliamua kabla upasuaji haujaisha.
Hiyo njia ya pombe ilikua inatumika poa na jamii za kitanzania miaka ya nyuma (maybe kabla ya ukoloni?). Kama ni mzazi alinyweshwa pombe na nyingine wanampaka tumboni kisha upasuaji unafanyika...Ila hiyo ya bangi ndio naisikia, Labda waliigundua wajamaica😅

Nimegundua jamii nyingi duniani zilikua na utaratibu wake wa kufanya upasuaji! Ila kihistoria inaonyesha upasuaji wa misri ndio wa zamani zaidi
Surgical texts from ancient Egypt date back about 3500 years ago. Surgical operations were performed by priests, specialized in medical treatments similar to today
 
Heshima yako mkuu!
Kwa historia ulipaswa upewe PHD ya heshima ila nashangaa wamempatia mh Kasheku Musukuma wanawaacha watu wanaostahili.
Taifa letu halimtambui wala kumthamini mwenye kipaji na uwezo.
Ndio maana bungeni hupelekwa walevi kama pierre liquid ila watu wenye potential chanya kwa taifa hawaujui hata mlango wa bongo.
Mwenyewe si uliona Amber rutty kafanywa mgeni rasmi Kwenye shule moja hivi kama vile alichofanya ni kitu cha kujivunia!
 
Umemtaja Marco Polo umenikumbusha huyu jamaa na Silk road. Wachina wamemtemgenezea muvi nyingi sana..Ila Japan na England naziheshimu sana hizi nchi, ni visiwa tu ila mambo yake noma sana. Sasa hivi ndio wamepunguza makali
Japanese waliiconguer China na rest of Asia kwa Administration yao pamoja na technology

English people waliiconguer dunia kwaajili ya Administration, Education na Legal system yaani uongozi bora wa kisheria...effect yao ipo duniani kote mpaka dakika hii
 
Japanese waliiconguer China na rest of Asia kwa Administration yao pamoja na technology

English people waliiconguer dunia kwaajili ya Administration, Education na Legal system yaani uongozi bora wa kisheria...effect yao ipo duniani kote mpaka dakika hii
Naam hichi ndio kinafanya niheshimu sana hizi nchi mbili. Yaani kama waliambiana Mzungu achuke America/Africa halafu mjapan achukue Asia. Ilifika muda mjep anaanza kuingia ulaya, kanchi kadogo kamejawa na majanga ya asili ila mambo yake balaa sana
 
Naam hichi ndio kinafanya niheshimu sana hizi nchi mbili. Yaani kama waliambiana Mzungu achuke America/Africa halafu mjapan achukue Asia. Ilifika muda mjep anaanza kuingia ulaya, kanchi kadogo kamejawa na majanga ya asili ila mambo yake balaa sana
Wako Aggressive sana hao. Hawaamini kwenye kushindwa, hata wakikutana na nchi yenye Large population.
 
Ukifunua vitabu vya sekondari kila definition utaona inaanza "it's greek Word" hata lugha rasmi ya Binomial nomenclature ni Greek tuseme Biology na sayansi kwa ujumla lugha yake ni Kigiriki.

Kwanini?
Asiilimia 70% ya wanafalsafa, Wanasayansi, Wagunduzi wote wanatoka Ugiriki. Kwa ufupi Sayansi imeanzia Misri ya kale na kutapakaa ulaya hasa ugiriki huko ndiko ilikofanyiwa kazi vizuri wewe chunguza kila mwanafalsafa anatoka Ugiriki.

Ugiriki ya zamani ilikua imeundwa na miji ipatayo mia moja ambapo kila mji ulikua na utawala wake, Mji wa Athens na Sparta ndio ilikua miji mikubwa na yenye nguvu zaidi, japo miji hii mra nyingi ilikua inapigana kwa ajili ya kugombania ardhi lakini vilikua vimejiunga pamoja ili kujilinda na uvamizi wa kutoka nje.

Enzi hizo Ugiriki ilikua Ugiriki kweli kuna madume ya haja hasa (Alpha, Beta peoples) mwaka 480 BC Mfalme Leonidas wa Sparta aliongoza jeshi la wanaume 300 tu kupambana na mfalme Xerxes kutoka Persia mwenye jeshi la watu 10000+ lakini waliwachinja hasa richa ya uchache wao. Japo Leonidas aliahindwa ila alijitahidi kuziwia uvamiI huo ambapo baadae Mfalme Xerxes alikuja kuuwawa na mrithi wa leonidas Themistocles

✓✓Kumbuka mfalme Xerxes ndio mfalme aliyemuoa Ester wa kwenye biblia ambae ester alitumia penzi kuziwia kuuwawa kwa Wayahudi wotewaliokua Babeli. (Kaa kumbukumbu zangu zipo sawa) Wafalme wa Persia waliitwa Ahasuerus. (Ahusuhero).

Sasa waku nini kiliwapata hawa watu? Gunduzi zote zilizofanywa kwao haziwanufaishi. Nilitegemea Ugiriki iwe miongoni mwa Super power county ila hata G7 haipo sijui G20.

Nini kiliwatokea? Sasa hivi hamna tena watu wenye akili au??
Wamezidiwa ujanja na Wainglishi. Hawa jamaa ni hodari kwa propaganda na warubuni wazuri tu kwa kukufanya uone chao ni kizuri kuliko chako.
 
Ukiniambia nitaje Binaadamu watano wenye akili zaidi duniani nitataja hawa.
1. Imhotep
2.Leonado da Vinci
3. Yesu
4. Nikola Tesla
5. plato

Imhotep ndio baba wa gunduzi zote kunzia hesabu za Geometry, Upasuaji wa ubongo, pyramids na Maze Tombs zilizojengwa Misri katengeneza yeye. Huyu jamaa wagiriki wanamuabudu kama Mungu wa tiba na madawa maana alikua daktari wa kila kitu. Alikua Polymath kwelikweli kuliko hata Da'Vinci. Michoro yote ya Misri katengeneza yeye.
Mtume wetu SAW yuko namba ngapi yakhe
 
Wako Aggressive sana hao. Hawaamini kwenye kushindwa, hata wakikutana na nchi yenye Large population.
Halafu japanese wapo very Disciplined ndio maana wapo tofauti kwav mambo mengi na wanadamu wengine. Napenda sana stori zao za Samurai and so on
Toka vita ya pili iishe wapo zao bize na na masuala ya technology. Ila Kamikaze technique was so badass
Japan-is-an-awesome-country-facts-1.jpg
 
Yesu amefanya ugunduzi gani ambao mpaka sasa Dunia inajua.

Binafsi najua Yesu amepaishwa kwa kupewa ukuu

Ali- disobey kanuni ya Archemedes na sheria ya Flotation kwa kutembea juu ya maji panapo bahari ya Galilaya.

Mkuu Yesu ni mambo yote ndani ya yote. Ukimpata yeye umepata vyote(Munishi).
 
Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe.

kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hzamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watu wote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.

Asante mkuu Da’Vinci.

Ku instill imani kubwa kiasi hicho ndani ya mioyo ya watu ni zaidi ya vumbuzi nyingi za kuunganisha dots tu, hata kama zinaonekana kama ndio zinaiendesha dunia kwa mtazamo wa juu juu.
 
Asante kwa ufafanuzi Mzuri.
Lakini kulingana na sifa ulizi taja yesu naona mengi alifanya Mazingaombwe (Miujiza) wala hakuna ugunduzi alio ufanya. Maana angefanya ugunduzi mpaka sasa alichokuwa akifanya angeacha walau Formula ili na wengine wakifanye.

Je, kama yesu alifanya hayo yote na hakuna alio waachia urithi (kuendeleza) miujiza hiyo nitakuwa ninakosea kusema alikuwa Mbinafsi? NB: si kwamba nakufuru ila ni mawazo tu.

Hitimisho kulingana na Miujiza ya Yesu hatolinganishwa na watu wasio na miujiza kama akina Galilei Galileo, Newton, Aristottle, Faraday, Archimedes, n.k hivyo alipaswa kushindanishwa na watenda miujiza wenzake kama Ngh'wana Malunde (Wa kabila la kisukuma).

Mkuu Kasomi heshima kwako.
Mungu ni mwema.

Uvumbuzi wote wa kisayansi kwetu Africa ni miujiza.

Aeroplanes, computers, simu za viganjani, internet painkillers, antibiotics, chanjo,n.k n.k.

Yote ni miujiza tu kwetu sawasawa na kufufua wafu au kuponya wagonjwa kwa neno.

Hivyo twaweza mpima Yesu kwenye mzani mmoja na hao Newton, Galileo, etc na kum declare kuwa amewazidi.

Alafu inasemekana ujio wa Yesu ndio ulileta mabadilko kwenye jamii ambayo yaliibua hivyo vipaji vya hao wanasayansi wakuu na hili laweza kuwa sehemu ya jibu la swali la mkuu Da’Vinci yaani Wagiriki walipoteza ubunifu na umaarufu kwa sababu waling’ang’ania upagani wao wakati wenzao wakibadilika na kwenda na Ukristo.
 
Misri inapigiwa chapuo Sana kwenye huu hata kwenda nje swali alilouliza, wagiriki ndio wagunduzi wa mambo mengi ya sayansi mpaka siasa (democracy) ,hii ilitokana na utamaduni waliokuwa nao na dini kwani wagunduzi wengi kama sio wote walikuwa wanakaa maisha ya monastery au monks, industrial revolution nafikiri wao hawakujisumbua Sana na mabadiliko hayo ambayo yalianza kushape upya uchumi wa nchi zilizochangamkia hizo revolutions lakini bado wao wakaendelea kutumika kama wasomi wa Ku plan future ya nchi hizo, na hadi Sasa wanatumika.
 
Back
Top Bottom