Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mpaka sasa haijakuwa wazi sana juu ya kilichotokea pale kiongozi wa Wagner, Prigozhin alipofanya uasi na kuelekea kama kutaka kuipindua serikali ya Urusi.
Nchi rafiki za Ukraine zilionenaka kufurahia tukio lile japokuwa wachache walitilia mashaka mtiririko mzima wa matukio.Jambo lililowashangaza wengi ni makubaliano ya ghafla ya kumpeleka kiongozi huyo uhamishoni nchini Belarus ambaye ni mshirika mkubwa na jirani na Urusi.
Pamoja na zawadi hiyo aliyopewa Rrogozhin baada ya uasi bado akaongezewa kupelekewa askari wa vikosi vyake na baadae silaha na pesa.
Belarus pia ni jirani na nchi ya Poland ambayo nayo ni mshirika mkubwa na mjumbe wa jumuiya ya NATO. Nchi hiyo vile vile ni njia kubwa ya kupitishia silaha zinazotolewa kama sadaka na zinazonunua Ukraine kwa ajili ya kuendesha vita hivyo na Urusi.
Kabla hata miezi miwili kufika tayari vikosi vya Wagner vimeonekana kwenye mpaka wa Poland na Belarus na hapo juzi helkopta za Wagner zimelalamikiwa na Poland kwamba zimeingia ndani ya maeneo ya mipaka yake.
Harakati hizo za kuongezeka harakati za Wagner inavyoonekana zimeanza kuishtua Poland mbapo sasa imeanza kutoa kauli za kupingana na mipango ya Ukraine katika vita vyake ambazo nyengine Poland imesema zinafanyika bila kushauriana nao.