Wagoma kujiunga form one kisa ugumu wa ajira

Wagoma kujiunga form one kisa ugumu wa ajira

Inabidi tuanze kuishi kama wahindi. Asilimia kubwa ya wahindi wanawapeleka watoto shule ili wajue kusoma na kuandika tu na wakishafika umri wa miaka zaidi ya kumi, wanawaandaa kuja ku take care biashara zilizoanzishwa na wazazi wao
Huu ni uongo,
Jamaa wana bachelor zao kibao,
Kina Mo wana bachelor, Jamaa wa lake ana bachelor, watoto wa Bakhresa wote wana bachelor, usiamini kuwa wahindi hawasomi,
 
Mtoto: Fulani yule anaimba Muziki maarufu sana anajulikana mpaka huko duniani amesoma?

Baba: Hajasoma kaishia tu hapo form 4

Mtoto: Anafanya kazi gani?

Baba: Ni mwanamziki mkubwa tu anapanda mpaka Ndege anakesha angani km mwanasiasa

Mtoto: Kwa hio Mimi Shule naenda kufanya nini?

Baba: Unaenda kusogeza umri wa kuishi na kuongeza ujuzi Ila ukimaliza inabidi utafute ujuzi mwingine wa ziada ndio utengeneze Pesa

Mtoto: Ndio hivyo tu?

Baba: Ndio

Mtoto: Sasa km ni hivyo kuna haja gani ya Mimi kusoma ikiwa Ajira zenyewe za kulenga kwa manati?

Baba: Hakuna haja kuna mambo mengi ya kufanya ushaambiwa pamoja na elimu ya darasani uwe na ujuzi wa ziada

Mtoto: Sasa huo ujuzi wa ziada unapatikana wapi?

Baba: Mtaa ndio kuna ujuzi wa ziada

Mtoto: Kwa hio kipi bora kupata ujuzi wa ziada mtaani na kutengeneza Pesa au kwenda kusogeza miaka?

Baba: Pata ujuzi wa ziada utengeneze Pesa hatuwezi wote kua wanasiasa hatuwezi wote kua mainjinia hatuwezi wote kua madaktari na marubani na walimu

Mtoto: Kwa hio sasa nafanyaje?

Baba: Angalia ujuzi unaouweza mtaani jifunze tengeneza Pesa hakuna muda wa kusubiri maisha yanakwenda kasi sana unaweza upate A zote darasani na ukaishia mtaani usipate kazi yoyote huko juu na hauna ujuzi wa ziada

Mtoto: Basi Mimi ntabaki mtaani tu hakuna haja ya kwenda form 1 ntaenda kujifunza ufundi cherehani hapo kwa Mama Joy

Baba: Sawa umeamua Jambo zuri Ila zingatia kua na ujuzi wa ziada ndio nazungumzia ujuzi wa ziada zingatia ujuzi wa ziada

Mtoto: Sawa ujuzi wa ziada hata ufundi cherehani ni ujuzi wa ziada

Baba: Ndio utakuja kua dizaina mzuri wa nguo kuliko kwenda kuparangana miaka minne wakimaliza wewe watakua wateja wako unawashonea nguo

Mtoto: Sawa ni Jambo zuri
 
Baadhi ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamegoma kuripoti shuleni kwa kigezo kuwa wenzao waliomaliza kidato cha nne, sita na chuo kikuu wapo mitaani bila ajira.

Wanafunzi hao wamesema hali hiyo imewakatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari badala yake kuamua kutafuta shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo mafunzo ya ufundi.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mmoja wa wazazi wa watoto ambao hawajaripoti shuleni, mkazi wa Kata ya Turwa wilayani Tarime mkoani Mara, Elizabeth Charles amesema binti yake alikataa kuandikishwa na kutaka apelekwe chuo cha ufundi cherehani kutokana na wahitimu wengi kuwa mitaani bila kazi maalum.
Hili nalo nendeni mkalitizame
 
Sasa huoni tuta kuwa na scarcity ya wasomi miaka ya mbeleni kama madaktar, mainjinia, walimu n.k
iko hivi, wanafunzi wasome kile ambacho watakitumikia bila kukwamishwa na mitihani ya necta, yaani mwanafunzi anasoma pcb kuanzia form one mpaka chuo kikuu anatunikia cheti cha kuhitimu na kisha kwenda kufanya kazi aliyoisomea. Mtindo wa sasa wa kusoma unakutana na mtihani wa form fou au six unafeli kwa alama kidogo tu unarudi nyumbani huku umejaza maarifa mengi kichwani yasiyokusaidia kuajiriwa. Wahitimu wa vyuo vikuu tu ndio bado wa uhakika wa kuajiriwa tofauti na hawa walioishia form four na six kwa dhana ile ya kufeli mtihani na kukosa sifa za kuajiriwa kwa cheti chenye alama za kutambuliwa. Mwanafunzi haendi shuleni kufeli watunga sera walijue hilo. Watu wanaenda shule kupata stadi na maarifa ya kufanya shughuli zao na za umma.
 
Baadhi ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamegoma kuripoti shuleni kwa kigezo kuwa wenzao waliomaliza kidato cha nne, sita na chuo kikuu wapo mitaani bila ajira.

Wanafunzi hao wamesema hali hiyo imewakatisha tamaa ya kuendelea na masomo ya sekondari badala yake kuamua kutafuta shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo mafunzo ya ufundi.

Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe, mmoja wa wazazi wa watoto ambao hawajaripoti shuleni, mkazi wa Kata ya Turwa wilayani Tarime mkoani Mara, Elizabeth Charles amesema binti yake alikataa kuandikishwa na kutaka apelekwe chuo cha ufundi cherehani kutokana na wahitimu wengi kuwa mitaani bila kazi maalum.
Shule waache tu iwapo wanasoma kwa ajili ya ajira
 
Back
Top Bottom