Wagoma kujiunga form one kisa ugumu wa ajira

Mwanafunzi haendi shuleni kufeli
Mfumo baba mfumo unasema kuna pyramid hakuna hexagon au pentagon ni pyramid yaan chini mnaanza wengi alafu wanaofika kule juu ni wachache wengine wote wanafia njiani kwa hio KUFELI kupo

Unaweza ukaheshimiwa shuleni alafu ukaja kudharauliwa mtaani hii Dunia imekua ya kifala sana yaan ya kifala sana kipanga na John kisomo wa darasa fulani baada ya kumaliza chuo akifika mtaani anaonekana bwege tu km hana namna ya kukunja maokoto anasubiria mikeka itoke aitwe kwenye interview ambayo ni km Bahati nasibu kuitwa na kupata nafasi ni majaariwa
 
Kwahiyo miaka 7 yote wameambulia kuamini elimu ni kwa ajiri ya kuajiriwa!
Hata vijana wote waliohitimu wangekuwa mtaan bado elimu ina nafas yake katika utambuzi wa mambo.
Hawa wapelekwe kwa nguvu
Elimu haina mwisho,mi nadhani wakishapata ujuzi na wakijiajiri,nafikiri Kwa hapo baadae kama watahitaji kujiendeleza wanaweza fanya hivyo kuliko kupoteza muda na kuendelea kuwa mizigo kwa wazazi,ndugu na jamaa! Ukizingatia elimu yetu haimwandai mtu kujiajiri.
 
ao watoto wanauelewa mdogo tu. asa kama kila mtu akienda veta nan atafanya kazi hospitalin .akati kila mwaka mahospital na ofisi zinaongekeka .swala la ajira ni bahati tu af ni bora mtu
kuwa na elimu mana uwezi jua je serikali ikitoa ajira itakuwaje?
 
Kwahiyo miaka 7 yote wameambulia kuamini elimu ni kwa ajiri ya kuajiriwa!
Hata vijana wote waliohitimu wangekuwa mtaan bado elimu ina nafas yake katika utambuzi wa mambo.
Hawa wapelekwe kwa nguvu
Upo sahihi ila mimi nina maoni tofauti kidogo. Ni bora mzazi amsomeshe mtoto hadi kidato cha nne na ahakikishe ametoka shule walau anafahamu lugha ya kiingereza vizuri na kufaulu ni muhimu pia.

Baadaye ya hapo watoto washauriwe vitu vya kusomea. Kuna baadhi ya diploma na degree ni za kupuuza.

1. Political Science
2. Sociology
3. Procurement
4. Social welfare
5. Education
n.k

Hizo ni baadhi tu. Inabidi zitolewe kwenye vyuo vichache sana ili kuzalisha graduates wachache ili kupunguza chawa wa watawala.

Badala yake mtoto asomee diploma au certificate ya elimu ambayo anaweza kujiajiri.
1. Mechanical engineering/technician
2. Computer science/ IT
2. Pharmacy science
4. Electrical Engineering/ technician
5. Business & Accounts (diploma inatosha)
6. Agriculture
n.k
 
Kila mtu fundi unategemea itakuaje?
 
Kabisa mkuu.Wahindi wanasoma sana aisee.tusidanganyane hapa.
Wahindi wengi wanasoma vizuri elimu ya msingi tu na ordinary level. Wakikaribia 20 yrs hapo wanachomekwa kwenye biashara za wazazi. Wakishakaa kwenye mfumo wanaanza kufukuzia professional certifications kama uhasibu, ukandarasi n.k. Degree ni kitu wanatafta mwisho kabisa wakiwa tayari wana hela.
 
ao watoto wanauelewa mdogo tu. asa kama kila mtu akienda veta nan atafanya kazi hospitalin .akati kila mwaka mahospital na ofisi zinaongekeka .swala la ajira ni bahati tu af ni bora mtu
kuwa na elimu mana uwezi jua je serikali ikitoa ajira itakuwaje?
Ikitoa ajira ikasema inataka freshers na mwanao kashasota hadi miaka 30 hana ajira inakuwa imesaida nini? Kikubwa mi napambana wanangu wote waende Ulaya. Mission ni kuukimbia ukoloni mweusi wa CCM. Bora mwanangu akahangaike na maisha ulaya kuliko bongo humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…