Kenya 2022 Wagombea Binafsi Waivuruga Kenya

Kenya 2022 General Election
Kenya pia watachujwa wabakie kumi. Hao wagombea 50 wa urais ujue saini zao bado hazijaidhinishwa na tume ya uchaguzi.
Ndio nashangaa na mihemko ya hawa wenzetu kuhusu huu uchaguzi. Watu wapo excited sana, hata zaidi ya wakenya. 😀 Yaani wanaotufunza kuhusu ugombea binafsi, hawajaushuhudia wao wenyewe kwenye nchi yao. Wakati nchini Kenya huu ndio utakuwa uchaguzi mkuu wa tatu, ambapo kumekuwepo na wagombea binafsi.
 
You sound logical comrade, though wengine wanaweza kuwasha moto kwa wanaharakati wa haki za binadamu kwamba wanabaguliwa na kudai katiba inayoweza kuwatetea na hapo itazuka agenda mpya na mjadala mpya. Ila umenishawishi.
 
Kenya pia watachujwa wabakie kumi. Hao wagombea 50 wa urais ujue saini zao bado hazijaidhinishwa na tume ya uchaguzi.
Issue siyo kuchujwa na wala hiyo haiwapi shida kwa sababu wanajuwa rais ni Raila kwamba wao hata wangepewa kujifua kwa miaka 100 hawawezi kuupata urais.

Issue ni kwamba baada ya kuchujwa wanaenda kusumbua/kutapeli wenye vyama kwamba wawape ela ili wawape wapigakura ambao ni wafuasi wao, au waingie mkataba kwamba wakitoa wapigakura basi mgombea urais au ubunge au u-gavana akishinda aje awape vyeo, so bado tatizo liko palepale.

Dawa labda iwe ni kufuta kabisa hoja ya ugombea binafsi.
 
Nisaidie kupata contacts za Ramogi Tv Kisumu.
Vipi boss, mbona unajinukuu na kujiomba contacts? 😀 Anyway, Ramogi Tv haipo Kisumu, ni mali ya Royal Media Services(RMS) ya SK. Macharia na wanamiliki Stesheni zingine za Tv na Radio km. Citizen, Inooro, n.k, n.k. Ofisi za RMS zipo jijini Nairobi.
Wewe ni mwanamuziki wa ngoma za Ohangla? Nazipenda sana jombaa, sanasana za Emma Jalamo.
 
Lakini ugombea binafsi una tatizo gani? Mbona Wakenya hawajalalamika? Vyama pia vina matatizo yao. Vyama vya Kenya havina demokrasia na kuna kitu kinaitwa direct ticket. Yaani kwa mfano ukiwa rafiki ya Ruto au Raila unapewa cheti bila kufanya nomination yaani hakuna uchaguzi wa chama utakaofanyika ili kumchagua mshindi. Sasa ikiwa hata kuna watu wanashinda katika uchaguzi wa chama na aliyekuwa namba mbili ndiye anayepewa cheti na aliyeshinda kukosa kupewa cheti unategemea huyo aliyeshinda asigombee kama mgombea binafsi ilhali kwenye ground watu wanampenda? Vyama vya Kenya pia vina udikteta mwingi sana na ndio maana kuna umuhimu wa ugombea binafsi.
 
Kilifi County.
Raia wamegoma kutoa vivuli vya IDs zao kwa wagombea binafsi ili wapeleke IEBC kama ushahidi wa udhamini, kisa na mkasa hawawaamini wagombea binafsi.

Trans Nzoia County.
Mjini Kitale, wagombea binafsi wanalalamikia sheria ya IEBC inawakandamiza kwa malipo makubwa ya kuomba kugombea alafu jina lako linaenda kutupwa na IEBC, 2017 walilipishwa Kshs. 20,000 na sasa 2022 Kshs. 30,000. Mgombea binafsi akitaka kumuwekea pingamizi mgombea yeyote (binafsi au wa chama) ada ya kuweka pingamizi ni kubwa. Pia kupinga matokeo ya kura Mahakamani ada ni kubwa kiasi ambacho wagombea binafsi wengi hawawezi kumudu na bado mlalamikiwa (respondent) akishinda anaweza kudai fidia kubwa ya kusumbuliwa na kesi Mahakamani inayofunguliwa na mgombea binafsi. Hoja ni kwamba kama dhana ya ugombea binafsi ni haki ya kiraia (civic right) basi isiwekewe vikwazo vingi maana wao hawapewi ela na chama wala ruzuku ya serikali bali wanajitegemea toka mifukoni mwao wenyewe.

Mount Kenya County.
Ambako ndiko pana ushabiki na shughuli nyingi za kisiasa za uchaguzi na ndiyo eneo lenye kura nyingi Kenya nzima, sasa tangu siku tano nyuma, pamevamiwa na wagombea wa vyama vikubwa kutongoza kura. Watu hawawendi mashambani wanategeshea wagombea kupata chochote maana kipindi hiki ndiyo msimu wa pesa katika eneo hilo. Eneo la Mount Kenya lina wagombea binafsi kibao. Eneo hilo lina vyama 10 vikubwa na vidogovidogo zaidi ya 10. PNU ya Kibaki ilipata kura nyingi za Wakikuyu kwenye eneo hilo 2007.

Busia County.
Wagombea binafsi wanavizia wagombea wa vyama wanapofanya mikutano ya ndani wanapiga simu kwenye vyombo vya dola kuja kuwakamata na kuzuia mikutano.

Kwa mujibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Kenya, vigezo vya kugombea urais Kenya ni:
1. Awe raia wa Kenya kwa kuzaliwa.
2. Awe ana sifa za kugombea ubunge (Katiba ya Kenya inamtaka rais kuwa Mbunge wa Jimbo)
3. Awe amesajiliwa na chama cha siasa kinachogombea au awe mgombea binafsi.
4. Awe na angalao wapigakura 2000 toka kila county kwa idadi kubwa ya counties.

Umri wa kugombea urais Kenya:
1. Umri wa chini ni miaka 18 (hapa pana shida), Tz ni miaka 40. Marekebisho ya Katiba ya Kenya 2010 yalifuta umri wa chini wa kugombea urais wa miaka 35.

2. Bunge la Kenya lilisema ukomo wa umri wa kugombea urais wa miaka 70 unabagua wananchi.

Nafikiri unaishi Migingo wewe (No roads, no airport, no railway, no beach, no telecom towers, no cable telecoms, no everything except fish and HIV)
 
Uko vizuri Tony254.

Hata hapa Tz vyama vya upinzani vinafanya uchaguzi wa ndani wa geresha tu kumpata mgombea lakini wanakuwa wanaye tayari. Tena ni walewale miaka yote tangu 1995.

CCM pia kura ya maoni siyo kigezo cha kupata tiketi ya kupeperusha bendera, ni geresha inayoua chama na kudororesha demokrasia kwa kutengeneza mitandao/makundi.

Kenya, baraza la mawaziri linajulikana kabla ya kura kupigwa kwa sababu ifuatayo:

Mwenye idadi kubwa ya wapigakura/wafuasi, ili apewe nafasi kwenye coalition na ahadi ya uteuzi kwenye serikali mpya, sharti apewe idadi ya kura za yeye kuleta kwenye coalition, kinyume na hapo yeyote ambaye chama chake kitapata idadi hiyo ya kura popote nchini ambaye yuko kwenye coalition ndiye atapewa cheo hicho. Hapa ndipo Musalia Mudavadi ameingia kingi kwa Ruto. Ali Hassan Joho Gavana wa Mombasa County naye ameahidiwa na Azimio nafasi ya Waziri wa Ardhi akileta idadi fulani ya kura. Ni vivyo hivyo kwa wote walio kwenye coalitions.
 
Wewe ni ndondocha wa wapi?
 
Source ya hizi habari zako iko wapi ili tujisomee wenyewe? Kwenye jukwaa hili huo ndio huwa utamaduni, mada huwa zinaambatana na 'sources', au 'references'.
Kwahivyo hayo uliyoyaandika hapo, ndio yanadhibitisha kwamba ugombea binafsi unaivuruga Kenya na kwamba haufai? Umeueka kwenye ratili na ugombea binafsi kwenye nchi ipi hiyo ukanda huu, kwa mfano? Alafu huko kwenu Migingo na sijui HIV kunahusiana vipi na maswali niliyoyauliza, kwenye hiyo comment yangu uliyoinukuu?
 
Kenya pia watachujwa wabakie kumi. Hao wagombea 50 wa urais ujue saini zao bado hazijaidhinishwa na tume ya uchaguzi.
Exactly.

Concept ya ugombea binafsi ni haki ya msingi, nchi hazitakiwi kusema kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi, halafu zikamlazimisha mtu kuwa na chama ili awe kiongozi.

That's basically giving a right by the right hand and taking it back by the left.

Sasa kama mimi sioni chama ninachokubaliana nacho, na nataka kuwa kiongozi, hapo si nanyimwa haki yangu ya kikatiba?

This is what is happenning in Tanzania.

Kwa sababu CCM, the ruling party, inaogopa watu wakiwa na nafasi ya ugombea binafsi, hawatakihitaji chama na watakipinga.

Na ndiyo maana kuna mkakati wa kuichafua hii dhana ya ugombea binafsi ionekane mbaya.

Wakati changamoto zake zinaweza kuw amanaged vizuri tu.
 
You sound logical comrade, though wengine wanaweza kuwasha moto kwa wanaharakati wa haki za binadamu kwamba wanabaguliwa na kudai katiba inayoweza kuwatetea na hapo itazuka agenda mpya na mjadala mpya. Ila umenishawishi.
Mtu anayeshindwa kupata wadhamini 20,000 kila mkoa ni kama vile amepewa nafasi ya kushiriki kura za maoni kwa wananchi akashindwa kupata kura za kutosha.

Hapo hata kulalamikia haki za binadamu hana msingi.
 
Sasa kama mimi sioni chama ninachokubaliana nacho, na nataka kuwa kiongozi, hapo si nanyimwa haki yangu ya kikatiba?
Ndiyo maana Kenya wali-review Katiba ili itoe haki kwa wote kwamba kugombea urais uwe na umri wa 18 na ruksa kuzidi miaka 70 iliyokuwepo awali.
 
Ndiyo maana Kenya wali-review Katiba ili itoe haki kwa wote kwamba kugombea urais uwe na umri wa 18 na ruksa kuzidi miaka 70 iliyokuwepo awali.
Naam, ndiyo inavyotakiwa hivyo.

Sasa hivi kuna watu wako CCM au vyama vya upinzani, si kwa sababu wanavikubali vyama hivyo, bali kwa sababu hawawezi kugombea uongozi bila ya kuwa na chama.
 
Hizo sababu zote ulizoorodhesha si sababu za kusimamisha mfumo tunaotumia wa kumpa mtu yeyote Yule Uhuru wa Kuwania urais.

Kama hizo ulizotoa hapo ndo sababu basi mbona Tanzania msiamue Tu kugeuza Tz iwe Kingdom ambapo familia moja inaongoza Taifa na iwe hakuna uchaguzi kila baada ya miaka 5 manake hio system ni rahisi zaidi kuliko demokrasia.

Alafu kama hujui, kuna Sheria kadhaa ambazo zimewekwa kuzulia kila mtu Kuwania kiti cha urais, Mbali na msajili wa vyama kuna polisi kupitia DCI, DPP, NIS wote lazima wakuchunguze waseme hawana kesi na wewe na haujawahi kuhukumiwa na mahakama.

Alafu kupewa tiketi ya urais na IEBC lazima watu elfu mbili kutoka zaidi 50% ya county zote 47 za Kenya wawe wametia saini kwamba wangependa wewe uwe mgombea wa Rais ... Kama hautapata saini hizo utanyimwa tiketi.... Kuna visheria vidogo vidogo vyengine kama hivyo ambayo inafanya iwe vigumu Kwa mwendazimu yeyote kupewa tiketi ya Kuwania urais. Kwahivyo usishangae kusikia hio list ya wanaotaka Kuwania urais imepunguzwa Kwa asilimia kubwa kwasababu wagombea walishindwa kupata saini hizo.


Anyway, Katiba yetu bado changa kwahivyo ni vizuri ipimwe na tujue mipaka yake... Hivi unajua kule marekani Katiba Yao inaruhusu mtu yeyote kuwania urais kama independent candidate lakini hakuna mtu amejaribu kufanya hivyo ndani ya nusu Karne? Kila siku ni Democrats VS republicans kwasababu Katiba Yao imekomaa, imepimwa ikajaribiwa Hadi vikatosha ndani ya miaka 400 Hadi kila mtu anajua bila kupitia republican au democrats basi hautashinda chochote..
 
Ikiwa hivyo hua president ana join side yenye anataka (mara nyingi yenye wabunge wengi na interest sawa) na kutengeneza serikali ya makubaliano na kuteua baadhi ya viongozi wa juu wa serikali kutoka kwa hicho chama so anaendelea kama kawaida.
Hii wakitaka mda wiwote wanaswitch side na inabidi uchaguzi mkuu uitishwe kila baada ya miezi 3 kama israel,,
Kwa nchi zetu hatuwezi hii,,
 
Uasin Gishu county mechi kali Buzeki(independent) vs Bii(UDA). Buzeki is no push over ,fierce battle na Mandago last election (nilidhani atakuwa chaguo la UDA 2022 UG governer)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…