Wameivuruga Kenya kwa njia ipi jombaa, na hata fomu zao za kugombea hawajaziwasilisha kwa tume huru ya IEBC? Wapiga kura nao wamechanganyikiwa kivipi, wakati hata siku ya kupiga kura haijawadia? Mbona unataka kuwavuruga watanzania wenzako na hizi hadithi zako hizi za kujitungia? Ambazo hata sisi wakenya tunazisikia kwa mara ya kwanza kutoka kwako. Wagombea huru wamekuwepo tangia uchaguzi mkuu wa 2013. Tena kupata hiyo fomu ya kuwania, kwa mgombea yeyote yule huwa kuna hela ambayo lazima ulipe.
Kilifi County.
Raia wamegoma kutoa vivuli vya IDs zao kwa wagombea binafsi ili wapeleke IEBC kama ushahidi wa udhamini, kisa na mkasa hawawaamini wagombea binafsi.
Trans Nzoia County.
Mjini Kitale, wagombea binafsi wanalalamikia sheria ya IEBC inawakandamiza kwa malipo makubwa ya kuomba kugombea alafu jina lako linaenda kutupwa na IEBC, 2017 walilipishwa Kshs. 20,000 na sasa 2022 Kshs. 30,000. Mgombea binafsi akitaka kumuwekea pingamizi mgombea yeyote (binafsi au wa chama) ada ya kuweka pingamizi ni kubwa. Pia kupinga matokeo ya kura Mahakamani ada ni kubwa kiasi ambacho wagombea binafsi wengi hawawezi kumudu na bado mlalamikiwa (respondent) akishinda anaweza kudai fidia kubwa ya kusumbuliwa na kesi Mahakamani inayofunguliwa na mgombea binafsi. Hoja ni kwamba kama dhana ya ugombea binafsi ni haki ya kiraia (civic right) basi isiwekewe vikwazo vingi maana wao hawapewi ela na chama wala ruzuku ya serikali bali wanajitegemea toka mifukoni mwao wenyewe.
Mount Kenya County.
Ambako ndiko pana ushabiki na shughuli nyingi za kisiasa za uchaguzi na ndiyo eneo lenye kura nyingi Kenya nzima, sasa tangu siku tano nyuma, pamevamiwa na wagombea wa vyama vikubwa kutongoza kura. Watu hawawendi mashambani wanategeshea wagombea kupata chochote maana kipindi hiki ndiyo msimu wa pesa katika eneo hilo. Eneo la Mount Kenya lina wagombea binafsi kibao. Eneo hilo lina vyama 10 vikubwa na vidogovidogo zaidi ya 10. PNU ya Kibaki ilipata kura nyingi za Wakikuyu kwenye eneo hilo 2007.
Busia County.
Wagombea binafsi wanavizia wagombea wa vyama wanapofanya mikutano ya ndani wanapiga simu kwenye vyombo vya dola kuja kuwakamata na kuzuia mikutano.
Kwa mujibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Kenya, vigezo vya kugombea urais Kenya ni:
1. Awe raia wa Kenya kwa kuzaliwa.
2. Awe ana sifa za kugombea ubunge (Katiba ya Kenya inamtaka rais kuwa Mbunge wa Jimbo)
3. Awe amesajiliwa na chama cha siasa kinachogombea au awe mgombea binafsi.
4. Awe na angalao wapigakura 2000 toka kila county kwa idadi kubwa ya counties.
Umri wa kugombea urais Kenya:
1. Umri wa chini ni miaka 18 (hapa pana shida), Tz ni miaka 40. Marekebisho ya Katiba ya Kenya 2010 yalifuta umri wa chini wa kugombea urais wa miaka 35.
2. Bunge la Kenya lilisema ukomo wa umri wa kugombea urais wa miaka 70 unabagua wananchi.
Nafikiri unaishi Migingo wewe (No roads, no airport, no railway, no beach, no telecom towers, no cable telecoms, no everything except fish and HIV)