Zanzibar 2020 Wagombea wa CCM Pemba wana haya ya kunena


Hiyo ndio sababu waliyosema hao walioenguliwa au unasema wewe ??
 


Unao ushahidi wa hichi unachokisema ???
 
Kuna tofauti kati ya Unguja na Pemba. Huu mfano ulioutoa ni kutoka Unguja sio Pemba.
Amandla....
 
Ingekuwa hawajakata rufaa wasingesema wanasubiri maamuzi ya Tume. Na kama wanachama wa vyama pinzani wamesema kuwa wao hawajaweka mapingamizi basi pingamizi hizo zimewekwa na wasimamizi wa uchaguzi au zimewekwa kwa kutumia fomu za kughushi. Wanachofanya wanachama/wapenzi wa chama cha ACT-WAZALENDO ni kutoa tahadhari kwa taasisi yenye mamlaka ni kuwa hawatakubali kuenguliwa kwa kuonewa. Kama wataenguliwa itakuwa ni wajibu wa NEC kuifahamisha na kuihakikishia jamii kuwa uamuzi wao uliongozwa na sheria na taratibu zilizopo na sio vinginevyo.

Amandla...
 
what are you talking about, unaambiwa wameenguliwa kwa barua za wagombea wa ccm ambao wamekuja kukana, wewe unataka ku assume huenda kulikuwa na sababu zingine, kuwa ccm hakufanyi uwe na akili zaidi kuliko kuwa opposition, nchi yetu sote mitazamo tu ndio tofauti, arghh!
 
Jifunzeni kujaza fomu vizuri.
 
Sipendi malalamishi we ukijua mpuuzi fulani kahusika kumuengua mtu wetu tafuteni ni mtu Kijiji gani mnaenda kumuengua mama yake au baba yake huko atokako uone Kama watapokea maelekezo ya kingese haya
Hapana mkuu, wazazi tusiwahusishe tutakuwa tunawaonea maana kwa Pemba si aghalabu kumkuta mzazi yuko upinzani. Dawa ni kuwagusa wao wenyewe ama watoto wao au wake zao na hapo baada ya kuwakosa wenyewe! Wakikatwa vichwa wasimamizi wawili watatu haki ya nani hawatakubali kupokea maelekezo ya kijingakijinga!
 
Unao ushahidi wa hichi unachokisema ???
Hujui kuwa Magufuli na Lipumba waliwekewa pingamizi na Lissu; kuhusu hizo taarifa nilizoweka zimetoka kwa wasimamizi wa uchaguzi Zanzibar na wakatoa na majina ya waliopitishwa kugombea. Mpaka sasa ni kumi tu ambao hawakukidhi matakwa ya sheria, na mmoja aliyekuwa amewekewa pingamizi yeye amelipangua. Hiyo ndiyo lugha waliyotumia, sasa kama Maalim anajua wameonewa basi atueleze sababu alizaoabiwa kuhusu kuenguliwa kwao; siyo kupiga kelele tu. Wasimamizi wa uchaguzi wamesema tu kuwa hawakukidhi matakwa ya sheria, kwa hiyo sote hatujui ni sheria zipi hawakukidhi.

Hiyo ndio sababu waliyosema hao walioenguliwa au unasema wewe ??

Kwa vile tumeambia ni kutokukidhi sheria, sababu zipo nyingi; hapo nilikuwa natoa mfano tu ambao Maalim anaweza kutuarifu, nimetumia mfano wa uraia siyo kwamba ndiyo sababu iliyotumika kwa sababu mpaka sasa pande zote mbili hazijasema zaidi ya tamko hilo la wasimamizi wa uchaguzi, na malalamiko ya ACT
 
Wewe jifanye kujua! Hivi unawajua Wapemba wewe?
 
Kuna tofauti kati ya Unguja na Pemba. Huu mfano ulioutoa ni kutoka Unguja sio Pemba.
Amandla....
Basi kama matokeo ya pemba hayajatangazwa; kwa nini kuwe na kelele? Pale waliandika matokeo ya awali, yaani bado kuna mengine yanakuja lakini kelele zimekuwa nyingi sana. Taarifa kamili zikija tutazijadili lakini siyo kuongea speculations tu.
 


Maendeleo hayana vyama!
 
Wewe jifanye kujua! Hivi unawajua Wapemba wewe?
ni walalamikaji sana hata pasipo na sababu? Katika makosa makubwa kwa viongozi ni kuwaaminisha watu wako kuwa wao wanaonewa tu. Bbaadaye wanaweza kukata tamaa kujishughulisha na lolote wakiamini wanaonewa tu au kujikua wankuwa wavunjifu wa sheria pas na sababu ya maana.
 
Waambie watu wako kwa Pemba wanacheza na moto.
 
Basi kama matokeo ya pemba hayajatangazwa; kwa nini kuwe na kelele? Pale waliandika matokeo ya awali, yaani bado kuna mengine yanakuja lakini kelele zimekuwa nyingi sana. Taarifa kamili zikija tutazijadili lakini siyo kuongea speculations tu.
Sio speculations. Wasimamizi wa uchaguzi Pemba wameishatoa maamuzi yao kuhusu nani anastahili kugombea ubunge na nani hastahili. Katika maeneo mengi wasimamizi hao wameamua kuwa wagombea wa ACT-Wazalendo hawastahili na ACT-Wazalendo wamekata rufaa kupinga maamuzi hayo. Ni haki yao kuufahamisha umma kuwa wamekata rufaa na mategemeo yao kuwa haki itatendeka. Kuwataka wasilalamikie maamuzi yaliyofanyika hadi yote yatoke ni kama kumwambia mtu asilalamike mtu anapomkata kidole bali asubiri mpaka pale atakapomkata kichwa.

Amandla...
 


Tume inadanganya haina uhalali wa kuendesha uchaguzi.
Uchaguzi uhairishwe iundwe tume nyingine huru.
 
Mgombea hana kosa lolote, unamuengua mtu kwa uhuni tu. Halafu eti aliyeenguliwa aanze kupoteza muda wa kukata rufaa. Huo ujinga Watanzania tuukatae.

Tume ni jukumu lao kuhakikisha wasimamizi ni watu thabiti, wenye hekima, dhamira njema na uwezo. Wameyaweka mashetani kuwa wasimamizi wa uchaguzi, na wanajua ni shetani. Hayo mashetani hayakemewi, hayaonywi, hayazuiwi, hayaondolewi wala kuadhibiwa. Yanaachwa yafanye mambo yote ya ushetani kwa uhuru, halafu eti wagombea wapoteze muda wao kukatia rufaa maamuzi ya kishetani yaliyofanywa na hawa wakala wa shetani. HAPANA.

Kama Tume haitaki kuwaondoa mashetani kusimamia uchaguzi, wananchi wayaondoe haya mashetani kwa namna yoyote inayowezekana. Tutaendelea kuruhusu watu waendawazimu kuichezea haki ya wananchi wetu mpaka lini?

Wananchi wayaadhibu vikali haya mashetani yanayovuruga haki za wapiga kura. Kumwadhibu mhalifu, ni kazi takatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tume inadanganya mchana kweupe je siku ya kuhesabu kura Usiku si ndio balaa .haina uhalali wa kuendesha uchaguzi.
Uchaguzi uhairishwe iundwe tume nyingine huru.
 
Kwa vyovyote hakuna sababu zozote. Uchaguzi haujaanza kufanyika leo kwenye awamu hii. Kwa ujumla huu utawala ni utawala wa shetani.

Kwani walifanya nini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa? Hao wagombea na hivi vyama vya siasa vimetua leo toka Jupiter?

Kama awamu zote watu hujaza fomu na kugombea, kwa nini leo watu wote wadakwe na upumbavu kiasi cha kushindwa kujaza fomu.

Wajinga wengi wamejaa CCM, kwa nini hakuna hata mmoja toka CCM aliyeenguliwa? Kwa nini mambo mengi ya hovyo yametokea awamu hii?

Kwa sasa inaonekana Taifa lipo chini ya laana. Mtawala akilaanika, Taifa hulaanika pia. Kuna mabaya yanatokota kuliandama Taifa kutokana na watawala ambao ni mawakala wa shetani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna hoja ya kuwaengua wagombea wa upinzani tu. Usiamini kuwa hata huku bara, kuwaengua wagombea 95% wa upinzani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, kulikuwa na sababu za msingi.

Huwezi kumwondoa Rais Magufuli kwenye haya maovu yote. Lazima ndiye mhusika mkuu kwa 100%. Uchaguzi haujaanza kufanyika leo, kwa nini mambo yote ya hovyo kuhusiana na uchaguzi, haki za watu, uhuru wa watu, uhuru wa vyombo vya habari, yote yatokee kwenye utawala wake tu?

Lakini zingatia pia kauli zake zile za ajabu ajabu za kuwaagiza wasimamizi wa uchaguzi wasiwatangaze washindi wagombea kupitia vyama vya upinzani, hata kama wameshinda!! Hivi Taifa hili limewahi kuwa na kiongozi aliyewahi kutoa kauli kama hiyo?

Kwa hiyo tunajua chanzo cha haya maovu yote. Kila mmoja anajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…