Zanzibar 2020 Wagombea wa CCM Pemba wana haya ya kunena

Jambo la muhimu sasa ni kuhakikisha hao wagombea wa CCM wanabeba mshahara wa dhambi za CCM na wasimamizi wao wa uchaguzi. Maana ukweli ni kuwa ushetani wote unaofanywa na tume ni kwaajili ya kuhakikisha hao wagombea wa CCM wanapita bila kupingwa.

Sasa njia sahihi ni kudili na hao waliopitishwa bila kupingwa.

Wapiga kura wasiingie kwenye mtego wa kusema kuwa wagombea wa CCM hawahusiki, hata wakawatenga na uovu. Hao ndio wawe victims wa kwanza wa uonevu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria hizi zimewekwa kulinda masilahi ya CCM kwahiyo dawa ni watu kufanya maamuzi magumu na wapemba watawaonyesha.
 
We jamaa acha kusumbua watu fuatilia vizuri social media ujuwe kinachozungumzwa. Maalim alisema waliwaengua 18 baadae nane wakabaki 10. Na juzi wameshamtoa mmoja hivyo sasa bado 9.
 
Huyu Kichuguu pamoja na kuwa amepata exposure kwa kuishi miongoni mwa nchi zilizostaarabika, jamaa bado ni kiazi sana.

Niliwahi kujadili naye hapa issue ya Lissu kufanya kampeni kabla ya muda nikajiridhisha kuwa uelewa wake ni mdogo na leo naona anarudia upupu huo huo hapa, anachojua yeye ni kunakili vifungu vya sheria asivyoelewa hata tafsiri yake.
Mbaya zaidi eti anaamini hii tume na ccm wanaweza kutenda haki.

Ukitazama tangu mchakato wa uchaguzi uanze utagundua kuwa haya hayatokei kwa bahati mbaya. Issue ya mapingamizi inakuja baada ya plan zingine kufeli.

Ilianza kwa kuwanyima fomu wagombea, ikafatiwa na kukataa kuzipokea fomu wanaporejesha, kuwateka wagombea, kuwabambika kesi zisizo na dhamana ili wasirejeshe fomu na baada ya yote haya kufeli kwa baadhi ya wagombea, plan ya mwisho imekuwa ni mapingamizi.
 
Basi kama matokeo ya pemba hayajatangazwa; kwa nini kuwe na kelele? Pale waliandika matokeo ya awali, yaani bado kuna mengine yanakuja lakini kelele zimekuwa nyingi sana. Taarifa kamili zikija tutazijadili lakini siyo kuongea speculations tu.
Mwenendo na historia ya CCM kwenye uchaguzi inafahamika. Hulka ya Rais Magufuli kwenye masuala ya demokrasia, uhuru wa watu na haki za raia inafahamika.

Bila kusimama kidete, ukasubiria haki kwenye utawala wa awamu hii, ni sawa na kusubiria embe chini ya mchongoma.

Jambo la muhimu ni kutoa amri kwa Tume, ndani ya siku 5, wagombea wote nchi nzima wawe wamerudishwa isipokuwa wale waliojiondoa wenyewe. Nje ya hapo hakuna uchaguzi. Ujinga na primitivity iliyoletwa na utawala wa awamu hii, tuukatae kwa nguvu zetu zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakuona unapata tabu sana kutetea hizi mambo. Barua ya/ za waliodaiwa kuweka pingamizi zipo na wamekanusha kuweka hayo mapingamizi, ila wewe unasema huenda kuna sababu ingine. Hiyo sababu ingine unayodhani huenda ikawepo ni ipi??
 
Kwahiyo tume unaijua vizuri na hizo habari za Zanzibar Leo ndio unazisimamia? Kwamba mapungufu ya kisheria yamejitokeza kwa wagombea upinzani tu kama ilivyokua bara?
Tatizo anachagua upande mi namsoma muda mrefu sana, ni mtu aliyejipambanua na katika kujipambanua anasahau sio yeye mwenye macho na masikio ya kufahamu yanayojiri Zanzibar.
 
Hiyo hoja ya kudai huenda kulikua na sababu nyingine ndo amejikita nayo. Nimemuuliza hiyo sababu ingine ni ipi ilihali hao wanaodaiwa kuweka pingamizi wamekataa tena kwa maandishi? Kutetea hizi mambo inabidi uwe na akili za pwagu
 
Mkuu nakuona unapata tabu sana kutetea hizi mambo. Barua ya/ za waliodaiwa kuweka pingamizi zipo na wamekanusha kuweka hayo mapingamizi, ila wewe unasema huenda kuna sababu ingine. Hiyo sababu ingine unayodhani huenda ikawepo ni ipi??
Huyu Kichuguu ni wa kumpuuza tu muacheni aandike ujinga wake yamkini analipwa kwa alifanyalo.

Mgombea anataarifiwa na tume kuwa amewekewa pingamizi na mgombea fulani ambaye naye anakana kuweka pingamizi tena kwa barua then yeye anatueleza upumbavu kuwa inawezekana kuna sababu nyingine. Yaani tume yenyewe imetoa hiyo taarifa kisha yeye anajaribu kutuaminisha vinginevyo.

Mtu anayenukuu taarifa kutoka Zanzibar leo kama credible source ya kucross check integrity ya taarifa iliyoanzia ccm ni moja kwa moja hajielewi. Kwa maneno mengine haelewi hilo gazeti mmiliki wake ni nani. Sasa mtu wa namna hii anapaswa kupuuzwa tu.
 
"Makosa makubwa ya kiuongozi ni kuwaaminisha watu wanaonewa"... mkuu mbona mambo yako wazi hivi wenye makosa yanayopelekea kuenguliwa ni opposition tu? Kwamba kati ya wagombea wote bara na visiwani opposition ndo wenye dosari.

Sasa kama wenye dhamana ambao ni tume ndo walalamikiwa wakuu na viongozi wa opposition wanaona hili kuna ubaya gani wakiwaambia wafuasi wao? Ati wewe unadai ni makosa kuwaaminisha watu wanaonewa, enyi watetezi wa mfumo kandamizi kuweni na roho ya ubinadamu huku duniani tunapita tu.
 


Wewe unafanya kazi tume mkuu? Taarifa au majibu ya NEC/ZEC umeisikia na kuiona?

Kitu nakubaliana na wewe ni wanasiasa wetu kuwa makini na kufuatilia mambo kabla ya kuyatolea taarifa.

Tatizo ni hapo tume inapokua haiaminiki.
 
Na hao wanaokata wagombea wawe makini maana kama wanaenda kinyume na sheria na wenzao siyo wajinga watakusanya ushahidi baada ya uchaguzi waonekane walioshinda hawakushinda kihalali ije igeukie kwao, siku zote kabla hujafanya maamuzi unatakiwa uangalie Kama upo sahihi.
 
Fact.
 
Ni wakupuuzwa hakika.
 
nani kaweka hayo mapingamizi
 
Gazeti Zanzibar leo ni gazeti la CCM, wengi wetu tunalifahamu. Ni gazeti la mrengo fulani... ulitegemea liandike nini?
 
Ni wakupuuzwa hakika.
Mtu anayejaribu kujifanya anatetea haki kwa kutumia sheria mbovu ni mpumbavu tu, kama ni muumini wa haki angewashauri hao ccm kwanza walete katiba ya maana inayoweka misingi ya haki.

Jitu linahangaika kutetea tume ambayo imeteuliwa na ccm tena kwa kuweka makada ambao kwa uwazi wamewahi kuomba ridhaa za kugombea kwa tiketi ya ccm. Ccm hiyo hiyo ambayo at a certain point ni miongoni mwa wagombea kwenye chaguzi zinazo simamiwa na tume hiyo hiyo utarajie watende haki.

Magufuli alitamka hadharani kuwa awape gari, awalipe mishahara kisha wamtangaze mpinzani kashinda?

Haya yanayotokea unaona ni wasimamizi wa uchaguzi wanajaribu kujihakikishia ajira zao kwa kuhakikisha wanawaengua wapinzani mapema kabisa ili kutii agizo la Magu.
Kichuguu
 
No, mama yake au baba yake kwa kweli no, Wao sio waliotenda kosa na hawahusiki...tusiende huko jamani!
Hata me sipendi tufike huko, ila kuna kila dalili tukafika. Nadhani ni wakati muafaka hata hao ndugu zao wawasihi ili kunusuru usalama wao, muda ni sasa hawa watu wakichoka hatutaweza kuwawekea mpaka wa visasi vyao.

Cha ajabu taifa lina wanaojiita wazee, viongozi wa kiroho nk wote wapo kimya wakishuhudia nchi ikivurugwa badala yake wamekazana kuhubiri amani bila kuwaasa watawala kutenda haki.
 
Na kwa nini iwe "huenda..."? Kwani mambo haya si inabidi yawekwe wazi kwa mujibu wa sheria? Hio ficha ficha maana yake nini?
 
Amejikita kukosoa dosari za upinzani na kwamba wafuate sheria nilimuuliza katika wagombea wote bara na visiwani mbona ni opposition ndo wanaonekana kukosea na hatimae kuenguliwa?

Rejea uchaguzi wa serikalini za mitaa, haya yanayojitokeza sasa ndo yaleyale ya 2019 kwenye serikali za mitaa. Kihistoria kila tunapofanya chaguzi kuna upuuzi fulani unafanywa na tume, na kuna hawa wanaojitoa akili kuona makosa ya upande mmoja ni aibu kubwa hii.

Huyu ni wakupuuzwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…