Uchaguzi 2020 Wagombea wa Urais kutoka upinzani kimsingi wanaruhusiwa kutoa ahadi za miradi na misaada mbalimbali nchini, kama anavyofanya Magufuli

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Imekuwa ni kawaida kumsikia Rais Magufuli akitoa ahadi mbalimbali anapokuwa katika ziara nchini. Ahadi hizi ni za misaada na miradi mbalimbali ambayo utekelezaji wake utafanyika baada ya uchaguzi wa 2020.

KImsingi, unaweza kujiuliza, iweje Rais Magufuli atoe ahadi hizo wakati hatujui nani atakuwa raisi baada ya October 2020?

Hili linamaanishwa kwamba ahadi za Rais zinafanyika katika mintirafu kwamba kama akishinda uchaguzi ujao basi ndio atatekeleza ahadi hizo.

Kwa jinsi hiyo basi, wagombea wa Urais wa upande wa upinzani wana haki ya kutoa ahadi kama anazotoa Magufuli ambazo utekelezaji wake ni baada ya uchaguzi Mkuu. Kwa hiyo mtu kama Tundu Lissu, au Bernard Membe anaweza kwenda kwenye wilaya fulani na kuwaambia serikali itawatekelezea mradi huu mkubwa ma waji mwaka 2021, au tutawajengea hii barabara kiwango cha rami ili muweze kuunganishwa na mkoa fulani.

Wagombea Urais upande wa upinzani msisahau kutumia hiyo fursa ya kuahidi wilaya na mikoa miradi mikubwa ya maendeleo, kwa kuwa mna haki hiyo kama vile tu Magufuli, kwa kuwa hatujui nani atakuwa baada ya uchaguzi. Lakini la msingi ni kwamba yule atakaeshinda ndie atakuwa na uwezo wa kutekeleza ahadi anazotoa.
 
Muda wa kampeni bado, hata fomu ya kugombea hajachukua. Kwa sasa yeye ni Rais wa JMT, na sio mgombea mpaka pale tume ya uchaguzi itakapo ridhia kama yeye ni mgombea.
 
Sheria ya vyama vya siasa inasemaje? huyu anatoa rushwa ya waziwazi na kama kungekuwa na tume huru ya uchaguzi tayari huyu hana sifa tena lakini kwa vile NEC na ofisi ya msajili wa vyama ni machina ya CCM hatuna namna zaidia ya kuumia moyoni.
Mkuu kutoa rushwa ni pale Magufuli kama mgombea uraisi anatoa fedha taslimu kwa jumuia au taasisi, fedha ambazo hazikuwa katika mipango ya maendeleo iliyoainishwa kabla hata hatawa mgombea. Lakini ahadi za miradi sio rushwa, kwa kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa kupitishwa na katika taaisii za serikali pamoja na BUnge. Hivyo ahadi hizo zinaweza kutolewa na wagombeaji wa upinzani pia
 
Siyo kweli ngoja watoe upinzani uone msajili wa CCM atakavyo komaa
 
Hapana Mkuu. KUja juu kwa Msajiri wa vyama hakufanyi hili lisiwe kweli. Yule ni mtu wa kuhurumiwa tu.

Umewahi kufanya mchezo wa kutupa kitu mbali halafu mbwa wako anakimbia kukichukua anakurudishia kwa furaha na kukutaka ukitupe tena aende kukuletea? UKielewa hilo utaelewa mengineyo!
 
Tumhurumie aendelee kuharibu nchi?
 
Tumhurumie aendelee kuharibu nchi?
Hapana, tumhurumie kwa kuwa yeye anatumwa tu, hana la kufanya. Kumuondoa yeye hakutaondoa tatizo. Ukimwangalia kwa makini utaona mara nyingine anatoa maagizo huku anataka kulia!
 
Wewe nae unajiona una akili timamu? Au chizi asiyejitambua? Unakiri rais Magufuli anatoa ahadi kama rais. Na mantiki hiyo unakiri ndie rais wa JMT. Sasa hao wapinzani uchwara unataka watoe ahadi au misaada kama akina nani? Au unadhani JPM anatoa msaada kama rais wa JMT 2020-2025? Na urais wa 2015-2020 unajua unakoma lini kwq mujibu wa katiba ya JMT?
 
Yaani huelewi kabisa! Tatizo watu wenye vichwa vigumu kuelewa ndio mnaopiga kelele kuliko wengine!
 
Mkuu kutoa rushwa ni pale Magufuli kama mgombea uraisi anatoa fedha taslimu kwa jumuia au taasisi, fedha ambazo hazikuwa katika mipango ya maendeleo iliyoainishwa kabla hata hatawa mgombea. Lakini ahadi za miradi sio rushwa, kwa kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa kupitishwa na katika taaisii za serikali pamoja na BUnge. Hivyo ahadi hizo zinaweza kutolewa na wagombeaji wa upinzani pia
Kununua jogoo kwa laki ni nini, acha upumbafu kwani miaka yote mitano alikuwa hayaoni majogoo. Dawa ni spana tu ahadi tunapokea na spana tunazipiga😂😂
 
Attachments

  • EemJU_XXsAAfO8q.jpeg
    EemJU_XXsAAfO8q.jpeg
    10.3 KB · Views: 3
Yaani huelewi kabisa! Tatizo watu wenye vichwa vigumu kuelewa ndio mnaopiga kelele kuliko wengine!
Sielewi nini we bichwa maji? Sema urais wa 2015-2020 unakoma lini kwa mujibu wa katiba ya JMT? Kwa nini unahoji maswali ya kipuuzi na kipumbavu wakati rais anatekeleza majukumu yake!
 
Okay. Kwa hiyo kwa kuwa Uraisi wa JPM bado hawezi kuwa na hatia ya kutoa rushwa kwa sasa baada ya kupitishwa kuwa mgombea wa CCM?

Na Lissu na Membe je, wanaweza kutuhumiwa kutoa rushwa kwa sasa wakigawa fedha?

Na kama JPM anajua kuna uchaguzi unakuja na hajui kama atapita, anaweza kutoa ahadi ya kutoa fedha au kuwajengea watu mwaka 2021?

Vitu vingine sio lazima uwe na PhD ya Chemistry kuvielewa
 
Kununua jogoo kwa laki ni nini, acha upumbafu kwani miaka yote mitano alikuwa hayaoni majogoo. Dawa ni spana tu ahadi tunapokea na spana tunazipiga😂😂
KUnunua jogoo kwa laki sio tatizo, kwa sababu inawezekana kabisa ilikuwa ni katika suala la uchangishaji. Kwani hujaona minada ya ushangishaji watu wananua vitu mara 10 ya bei yake? Hiyo ni kufanya tukio lifurahishe. Sasa huyo mtu aliyemuuzia JPM jogoo ilikuwa katika mazingira gani?

Believe me, mio sio blind supporter wa Magufuli au mtu yeyeote, so huwa napenda nisimamie ukweli
 
Wewe nae unajiona una akili timamu? Au chizi asiyejitambua? Unakiri rais Magufuli anatoa ahadi kama rais. Na mantiki hiyo unakiri ndie rais wa JMT. Sasa hao wapinzani uchwara unataka watoe ahadi au misaada kama akina nani? Au unadhani JPM anatoa msaada kama rais wa JMT 2020-2025? Na urais wa 2015-2020 unajua unakoma lini kwq mujibu wa katiba ya JMT?
Halafu wewe kidudu kibaya, huelewi kuwa nimesema JPM hawezi kutoa ahadi kama raisi ikiwa utekelezaji wa hiyo ahadi utafanyika nje ya October 2020? Kwa sasa JPM hana madaraka ya uraisi beyond October 2020. Chochote anachoahidi kupita kipindi hicho ni rushwa ya uchaguzi. Na kama anaruhusiwa kufanya hizo ahadi basi wagombea wa uraisi wa upinzani wanaruhusiwa.

Kwa nini huelewi logiki ndogo kama hizi?
 
Mkuu kutoa rushwa ni pale Magufuli kama mgombea uraisi anatoa fedha taslimu kwa jumuia au taasisi, fedha ambazo hazikuwa katika mipango ya maendeleo iliyoainishwa kabla hata hatawa mgombea. Lakini ahadi za miradi sio rushwa, kwa kuwa miradi hiyo itatekelezwa kwa kupitishwa na katika taaisii za serikali pamoja na BUnge. Hivyo ahadi hizo zinaweza kutolewa na wagombeaji wa upinzani pia
Kwa hiyo ile Laki 1 aliyotoa kwa babu wa jogoo na 5m aliyotoa kwa shule unakubali ni rushwa?
 
Halafu wewe kidudu kibaya, huelewi kuwa nimesema JPM hawezi kutoa ahadi kama raisi ikiwa utekelezaji wa hiyo ahadi utafanyika nje ya October 2020? Kwa sasa JPM hana madaraka ya uraisi beyond October 2020. Chochote anachoahidi kupita kipindi hicho ni rushwa ya uchaguzi. Na kama anaruhusiwa kufanya hizo ahadi basi wagombea wa uraisi wa upinzani wanaruhusiwa.

Kwa nini huelewi logiki ndogo kama hizi?
Hiyo ya kumzuia rais aliyepo madarakani asitoe ahadi ambayo haiwezi kutekelezwa baada ya Oktoba ni kwa mujibu wa Ibara gani ya katiba ya JMT? Au sheria gani? Na hiyo ya kutaka wagombea wa upinzani kutoa ahadi kabla hata kampeni kuanza ni kwa mujibu wa ibara gani? Au mkichwa hakuna?
 
Kwa hiyo ile Laki 1 aliyotoa kwa babu wa jogoo na 5m aliyotoa kwa shule unakubali ni rushwa?
Kununua jogoo toka kwa babu sioni kama rushwa.

Kutoa milioni tano kwa shule, kama hakukuwa na mchango uliohusisha watu zaidi ya Magufuli kunakuwa na mazingira ya rushwa, hasa kama wanaofaidika na msaada ni wapiga kura.

Kwa hiyo kwa sasa JPM anapaswa kujiepusha na matendo ya kutoa fedha taslimu kwa walengwa ambao ni wapiga kura ikiwa mazingira ya kutoa hizo pesa hayahusishi jumuia kwa ujumla bali anatoa yeye peke yake. Utoaji wa fedha kama huo una mazingira ya rushwa.
 
Back
Top Bottom