Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Imekuwa ni kawaida kumsikia Rais Magufuli akitoa ahadi mbalimbali anapokuwa katika ziara nchini. Ahadi hizi ni za misaada na miradi mbalimbali ambayo utekelezaji wake utafanyika baada ya uchaguzi wa 2020.
KImsingi, unaweza kujiuliza, iweje Rais Magufuli atoe ahadi hizo wakati hatujui nani atakuwa raisi baada ya October 2020?
Hili linamaanishwa kwamba ahadi za Rais zinafanyika katika mintirafu kwamba kama akishinda uchaguzi ujao basi ndio atatekeleza ahadi hizo.
Kwa jinsi hiyo basi, wagombea wa Urais wa upande wa upinzani wana haki ya kutoa ahadi kama anazotoa Magufuli ambazo utekelezaji wake ni baada ya uchaguzi Mkuu. Kwa hiyo mtu kama Tundu Lissu, au Bernard Membe anaweza kwenda kwenye wilaya fulani na kuwaambia serikali itawatekelezea mradi huu mkubwa ma waji mwaka 2021, au tutawajengea hii barabara kiwango cha rami ili muweze kuunganishwa na mkoa fulani.
Wagombea Urais upande wa upinzani msisahau kutumia hiyo fursa ya kuahidi wilaya na mikoa miradi mikubwa ya maendeleo, kwa kuwa mna haki hiyo kama vile tu Magufuli, kwa kuwa hatujui nani atakuwa baada ya uchaguzi. Lakini la msingi ni kwamba yule atakaeshinda ndie atakuwa na uwezo wa kutekeleza ahadi anazotoa.