Wagonjwa wa Corona wadaiwa kuvunja geti hospitali ya Amana na kutoroka. Mwananyamala waleta vurugu wakitaka waruhusiwe

Serikali imeshindwa kumanage corona nchini cha msingi wagonjwa waachiwe warudi nyumbani na haina haja ya kuwapima watu wengine wala kuwaweka karantini. Warudi makwao wakajifukize tu maana serikali haijaleta korona.
 
Kama uzi huu umejaa uongo, IGP kashapewa maagizo. Mtashughulikiwa.
 


hivi Rais Magufuli hana washauri hashauriki ama?
 
Wanajaribu kuficha kinyesi chumbani ila wanaumbuliwa na harufu

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Makonda kimyaaa.

Yani hii issue itakuwa out of their hands. Na ni kwa sababu ya ukaidi wa magufuli.
Dar es salam intakiwa ifungwe
Hao wa mwananyamala wameleta shida kufungiwa!!? ndio iwe Dar yote tafakari?!
 
Hii habari imerushwa na ITV katika habari za Hivi punde.
Mkuu wa wilaya amekiri kuwa ni kweli vurugu za wagonjwa kutaka kutoka hospitali na kurudi makwao zimetokea
 
Na jamaa yangu yupo karibu na Amana anasema wagonjwa hakuna kilichokua kinaendelea walio kua taaban hakuna oxygen manesi wanawapea dawa dirishani wengine wanaombwa pesa wakanunuliwe dawa wameona bora wakajitibu nyumbani hakuna kinachoendelea hospital

Wamefika getini walinzi wakataka kuwazui wakawaambia tunawaambukiza walinzi wakakimbia na wao wakatoka

Ukweli ni aibu kwa serekali mi najiuliza inamana hawa wahudumu wa afya wakati wenzetu wanahangaika huku hawakuwekwa semina namana ya kuwahudumia hawa wagonjwa

Mpaka inafikia hatua ya wagonjwa kutoroka walikua wananyanyapaliwa wanaogopwa na wahudumu ukweli sielewi kama serekali walijipanga

Najiuliza Wazir mwenye zamana anatosha kweli kwa haya yanayotokea
Ninacho fikir ni kwamba inawezekana hata wahudum wa afya wakawa hawana vitendea kazi inatisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msanii Pierre Likwidi aongoza wagonjwa wa CORONA Amana Hospital Kuvunja geti na kukimbia. Wagonjwa wote wa Corona wamekimbia toka hospitalini hapo na kuingia mtaani.

Inasemekana hali ni mbaya watu wamekuwa wakifya na kuhachwa hali iliyopelekea wagonjwa wengine kuamua kukimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…