Wagonjwa wa Corona wadaiwa kuvunja geti hospitali ya Amana na kutoroka. Mwananyamala waleta vurugu wakitaka waruhusiwe

Wagonjwa wa Corona wadaiwa kuvunja geti hospitali ya Amana na kutoroka. Mwananyamala waleta vurugu wakitaka waruhusiwe

Serikali imeshindwa kabisa kufanya chochote na huu ugonjwa....nafikiri sababu ni mind set ya kipindi cha nyuma ya kutokusaidia watu wa maafa kwa kudema kwamba either wamesababisha wenyewe au wamejiweka kwenye mazingira ya kudhurika....


Janga hili limekuja kivingine na limekuta serikali inafanya ujanja ujanja tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kunatakiwa kuwe na infection control oficer katika kila wilaya, majukumu yake.
Kuhakikisha Kuna vifaa vya kutosha katika eneo lake.
Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wote wilayani kwake. Mafunzo yarudiwe kila mwaka.
 
Kunatakiwa kuwe na infection control oficer katika kila wilaya, majukumu yake.
Kuhakikisha Kuna vifaa vya kutosha katika eneo lake.
Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wote wilayani kwake. Mafunzo yarudiwe kila mwaka.
Hao watakuwepo sema kwa majina tofauti. Ishu hao wanatakiwa kutoa huduma wanaogopa kuambukizwa. Inadaiwa hawajapewa vifaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe juu yenu nyote

Jana asubuhi na mapema kulizuka uvumi wa wagonjwa wa wa corona kudaiwa kutoroka hospitali ya Amana walipokuwa wakipatiwa matibabu.

Baadae DC wa ilala alijitokeza na kukiri hiyo hali kutokea.

Kwenye maelezo yake DC anadai wagonjwa walikuwa wakilazimisha waachiwe ili wakajitibu wenyewe wakiwa nyumbani.

Kutokana na tukio hilo, tujiulize kipi hasa kimepelekea hao wagonjwa kushinikiza kuondoka ilihali wapo sehemu salama(hospitali)?

Je, huduma inayotolewa hapo hospitalini hailizishi, jambo linalopelekea wagonjwa kudai kuondoka?

Mpaka muda huu tunaozungumza ugonjwa wa corona hauna chanjo wala dawa. Je huko hospitalini wanapatiwa matibabu gani?

Serikali kudai wagonjwa wanaendelea kupatiwa matibabu ni kauli ya geresha kuwatoa hofu watu ila wakifika huko wanatelekezwa?

Tusemezane kwa upole mpaka majibu yapatikane
 
kwa hili la wagonjwa kutoroka inaonyesha serikali haipo seriously,

na hapa ndio mwananchi anapokuwa na hofu huko mtaani halafu kuna mtu anaitisha comference anawaambia watu kwamb hawajatoroka wagonjwa ,NONSENSE kabisa
watu watashindwa kuwa hofu huko mtaani ya kuambukizwa corona kwa hili serikali bado haipo seriously and people will die slowly
 
Unategemea mwanachi huko mtaani akisikia atashindwa kuwa na hofu,
nonsense , hii vita ya corona these tanzanians not seriously

hawa wagonjwa washitakiwe kwa kuhatarisha maisha zaidi ya raia milion 50
 
Write your reply...mbona Jana nimeangalia taarifa ya habari wanasema hakuna aliyetoroka ila walikuwa wanadai wanata kuondoka


so which is which ?
 
Kuna taarifa zinasambaa ambapo inasemekana wagonjwa wa COVID-19 walikuwa wamelazwa hopitali ya AMANA wamevunja Geti na kutoroka.

Inasemekana hii ni kutokana na kutelekezwa bila ya kupatiwa huduma na kutelekezewa maiti hospitalini.

Mwenye update kamili atujuze mimi nimepata Clip za Audio nimeshindwa kuziweka hapa.

Nambiwa wanapanda magari sasa sijui wanarudi makwao au wanaenda wapi!?

Mungu atunusuru kwakweli.
---

UPDATES MWANANYAMALA

Wagonjwa waleta vurugu


Wagonjwa hao wa corona wamedai wamechoka kukaa hospitalini hapo na sasa wanapiga makelele waruhusiwe waondoke.

UPDATE

Mkuu wa Wilaya Ilala ambayo ndiyo Wilaya yenye Hospitali ya Amana amethibitisha wagonjwa kutaka kuondoka ili wakajitibie nyumbani. Zaidi soma > Ilala: DC Sophia Mjema athibitisha wagonjwa wa COVID-19 hospitali ya Amana kuleta fujo na kutaka kuondoka wakajitibie nyumbani
Duuuh hatari hii.
 
Back
Top Bottom