DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wahadhiri wa dini ya Kiislamu nchini wamesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akipingwa kutokana na asili yake ya Uzanzibari, jinsia yake ya kike, pamoja na dini yake ya Kiislamu. Wameeleza kuwa baadhi ya watu kutoka Bara wamekuwa wakitoa lawama zisizo za msingi na kuhusisha changamoto mbalimbali za uongozi na mambo binafsi. Pia, wamedai kuwa katika kipindi cha uongozi wa Hayati John Magufuli, matukio ya utekaji yalikuwa mengi kuliko kipindi chochote kingine.