Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tanzania ujinga ni mwingi. Ila ujinga mkubwa naona upo kwa wasomi wa nchi hii. Yani wasomi tumekuwa walamba viatu vya makada wa sisiemu na viongozi wa nchi na tumesahau jukumu letu la kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali ili kuchochea maendeleo nchini. Ugonjwa wa uchawa umeenea kwa kasi hasa katika kundi la wasomi.

Wasomi tulitakiwa kuonesha changamoto na namna ya kuzitatua ili viongozi wachukue yale yanayowezekana. Tulitakiwa kukosoa serikali pale inapoyumba. Matatizo kibao nchini lakini kundi la wahandisi na wakandarasi ambao ni wasomi wao wanaona suluhisho ni kumnunulia Rais ndege ya kufanyia kampeni.

Siku za nyuma kidogo kundi la walimu wakuu walichanga fedha kumchukulia Rais fomu ya kugombea awamu ijayo. Wakasahau kueleza changamoto za walimu kwa ujumla. Huu ni upuuzi na ujinga uliokithiri.

Tunashindwa kukemea na kulaani matumizi mabaya ya fedha za umma kwenye misafara ya viongozi na magari zaidi ya mia. Manunuzi holela ya mashangingi ya viongozi kila mwaka. Mishahara mikubwa kupindukia ya wabunge na bado wanadai haitoshi wakati mwalimu, polisi nesi na watumishi lukuki wa serikali wanaishi na mshahara (take home) chini ya laki 6.

Matendo maovu ya polisi ya utekaji, uuaji na unyanyasaji wa raia. Tunashindwa kupigania katiba iliyobora ili kuhakikisha utawala bora.

Mambo ni mengi ya kushughulika nayo ila ni kama vile hayatuhusu. Ngoja kwanza tulambe viatu vya viongozi
 
Ingekuwa nchi yenye maadili ya kiutawala, nyie mlitakiwa msipewe kazi hata moja, kwa sababu mmetoa rushwa hadharani. Ni makosa sana, msomi anayejiita mhandisi, ingawa ni WA makaratasi,muulize mradi aliodesign na kuusimamia ukaisha, ni kama vile yule wa timu Fulani, eti engineer,kwa umri ule amefanya projects ngapi za kumtambulisha? Ndio sababu Magu aliwajua ni wababaishaji sana kwa sababu alikuwa nao karibu. Inawezekana Sasa hivi ni mteremko.
 
Hawana uwezo wa kununua helicopter. Kilichofanyika ni drama tu. Tumeibiwq za kwetu, kanunua mwenyewe hao Jamaa wamewekwa kama danganya toto tu. Watanzania poleni msipoamka mmekwisha
 
Kipi kinachokuhusu?
 

Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Wahandisi wameanza kisha walimu watafata kuchanga na kumnunulia fomu.....hadi raha
 
Haya ni majanga makubwa sector ya uhandisi manake ni kwamba watu wanapiga vibaya sana huko!
a
 
Kuna pesa imetakatishwa hapa yale mauzo ndio matumizi yanaendelea baada ya boda boda, tatizo hawajui kuigiza vizuri
 
Kwanini wasichangie chama badala ya mtu kwenye chama. Sasa mmiliki atakuwa aliyechanguwa au ni chama?

Ushauri: Mama tumia magari kwenye kampeni, waachie akina Msigwa hiyo chopa wazunguke nayo.
 
Ndio maana mnate
Ndio maana mnatengwa kwenye Dili kubwa kwaajili ya uchawa
 
Hawa si ndiyo wale wanalalamika kila siku kuwa wamepeleka certificates lukuki lakini hazijalipwa kwa sababu serikali haina fedha!

Hizi fedha kwa vyo vyote vile ni chafu zimetoka kwa Waarabu ambao wanakatiwa mapande ya ardhi yetu kwa kisingizio cha uwekezaji!
 
Ukute wame chomoa kwenye mfuko wak tusubiri na nyumbu UWT wachomoe za waalimu
 
Ni sawa tu maana hata kina Kier wamepewa na matajiri pesa ndefu tu

Ila hawa labda kwa sababu wamelipwa bila kurudisha gawio 😄
 
Wahandisi wameanza kisha walimu watafata kuchanga na kumnunulia fomu.....hadi raha
Hii ni nchi ya wapumbavu, as imejaa upumbavu wa kiwango kikubwa sana.. hao ni wahandisi, ngoja maticha waje, then madokta watamalizia huku wanasheria wakijiandaa kupindisha matokeo hulo tume huru!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…