Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa taarifa yenu siyo wakandarasi walionunua helikopita hiyo.....narudia tena siyo wakandarasi.....akili kumkichwaaa🤣🤣🤣🤣
 
Pesa zenu mlizitoa wapi zaidi ya kujengwa na kukopeshwa? Kwa nini hamkufanya wenyewe?
Ninapo soma maandishi ya aina hii toka kwako, najuwa kuwa najadili jambo muhimu na mtu asiye na upeo hata kiduchu. Na hii ndiyo sababu hata huyo 'Chura Kiziwi' hajui kabisa tofauti ya maswala haya.; "kukopa na kuuuza mali za nchi kwa hasara"!
 
Hii ni rushwa iliyokaa kimkakati sana. Ingekuwa JK Nyerere angewakemea hatari. Kwanza wasingethubutu.
 
Ninapo soma maandishi ya aina hii toka kwako, najuwa kuwa najadili jambo muhimu na mtu asiye na upeo hata kiduchu. Na hii ndiyo sababu hata huyo 'Chura Kiziwi' hajui kabisa tofauti ya maswala haya.; "kukopa na kuuuza mali za nchi kwa hasara"!
Wewe huna unalolijua ,unasugua maneno tuu kama kawaida yenu.

Hakuna swali langu umejibu ,unaanza kutafuta mlango wa kutokea 😂😂

Swali: Mtu mweusi wewe unaweza nini ikiwa hata Mwendokasi umekushinda?

Yaani Chadema nzima Kwa miaka zaidi ya 20 Sasa mumekosa mtu wankuongoza chama.zaisi ya Mbowe,huo ni uthibitisho kwmaba hakuna mnachoweza zaidi ya majungu,fitina na maneno Kwa Waarabu ila Wazungu Wala hatuwasikii 😆😆
 
Mbona inasound kama kick back hiv. kwanini asante yenu msinunue madawati au dawa hospitali.Kwa sababu hela hizo mlizopewa kandarasi ni kodi ya wanachi.
Heka heka na vimbwanga vinazidi kupamba moto, mpaka uchaguzi ufike tutaona mengi! Eti wanarudisha fadhila kwa yale Rais Samia amefanyia nchi! Kwa hali ngumu ya maisha na wizi unaoendelea serikalini kweli?

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Ndio tumeamua sasa hivi kila mtu kuwa chawa ili naye aende kula kwa urefu wa kamba yake?

Vijana tuamke kuokoa taifa hili, kwa haya yanayoendelea na nchi itafutika kwa kila mtu kuchota kwa nafasi yake bila kujali maslahi ya nchi.

===

Umoja wa Wakandarasi na Wahandisi Tanzania umemnunulia Helkopta Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aitumie Helkopta hiyo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakani (2025) atakapokuwa anapeperusha bendera ya CCM kama mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na wanahabari leo, Jumamosi Julai 20.2024 Msemaji wa umoja huo Mhandisi Yuda Thomas Kemincha amesema sambamba na kununua Helkopta hiyo lakini pia wametoa mafuta ya shilingi milioni 100 za Tanzania, huku akitumia nafasi hiyo kufafanua kuwa hatua hiyo inakuja kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia kuhusiana na yale aliyoyafanya nchini.

 
Sio ajabu kusikia na Umoja wa Machifu nao wamemchangia Mama na kumnunulia Chopa.
 
Utumwa upi unaopelekwa wewe? Bila Mwarabau kumpa Mafuta Nyerere Tanzania si inge collapse na kutishia kuwa ya kitumwa tena?

Narudia kuuliza ,nani mwenye uchungu na maisha Yako duni?
Kwanza elewa kuwa maisha ya mTanzania yeyote siyo duni, na ndiyo maana tutawaadabisha washenzi nyinyi mnaodhani maisha yetu ni ya duni.

Siku zote nilikuwa sijakuelewa nikuweke wapi, lakini leo kutokana na mstari huo wa juu nimetambua wewe hasa ni mtu wa aina gani hasa. Ni kundi lililoingia humu kupigania ajenda hii ya kuwadhalilisha waTanzania.

Kwa hiyo sasa nitakuchukulia hivyo, wewe ni kundi la wadhalilishaji wa waTanzania, kwa misingi ya uarabu wenu.

Kwa hiyo 'Chura Kiziwi' sasa hivi analipa fadhira kwa 'waarabu waliompa Nyerere mafuta'? Itakuwa akili zenu hazifanyi kazi sawasawa.
 
Pesa za kuuza maliasili zetu kwa wageni ndizo zinatumika kwa mlango wa nyuma.

Ajabu, wale makandarasi wanaolalamika kila siku hawalipwi pesa zao kwa wakati, leo wanatoa wapi pesa za kununua helkopta? na milioni 100 za mafuta?

- Wajinga wa awamu hii hawana hata akili na uwezo wa kutudanganya.

Hii awamu ya Samia niseme ndio ya hovyo kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya hili taifa, pesa za umma zinaibwa hovyo bila hatua kuchukuliwa, na kutumika hovyo kwenye mambo ya kijinga yasiyo na maana.

Mfano; mabango ya Samia nchi nzima nini maana yake? Samia anajigeuza Pepsi au Fanta anaanza kujitangaza kila mahali! simply wajanja wanapiga dili zao hapo nae amelala tu anajiita chura kiziwi.

Nchi inaongozwa na akili ndogo sana.
Tulia ww ela za ma engineer izo wacha watu waeke ela kwa kampeni .we kama ujaona mchango wake wenzako wameona
 
Kila mtu amsapoti mgombea wake, kongole kwao kwa kuamua hivyo

Hii iamshe ari kwa wengineo pia kuwasapoti wagombea wanaowakubali
 
Mianya ya Rushwa kubwakubwa baina Chawa wasomi na wafanyabiashara wanapojipendekeza katika siasa za Tanzania.

Matokeo yake umoja usio na afya wa kipigaji katika serikali na wakandarasi kuongeza bajeti ya miradi ya ujenzi ili fedha hizo za ziada ziende kugharamia shughuli za kisiasa za chama dola kongwe CCM.

Muungano huu wa TUCASA na CCM haukubaliki kabisa, kwa sababu unatengeneza mianya ya ufisadi, rushwa na matumizi ya ziada kugharamia chama cha kisiasa

TUCASA ni nani ni Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA)



TOKA MAKTABA :


KAZI ZA UJENZI ZIFANYIKE KWA UBORA NA UZALENDO - DKT. BITEKO​

28TH JUNE, 2024
8b0d21cf4ca08a9c754f9213c3833760.jpeg

KAZI ZA UJENZI ZIFANYIKE KWA UBORA NA UZALENDO - DKT. BITEKO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko amewataka makandarasi nchini kutekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora na uzalendo mkubwa ili wainue uchumi wa nchi na kuhakikisha unashikiliwa na Makandarasi wazawa.

Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 28 Juni, 2024 alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi lililoandaliwa na Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Shirikishi Tanzania (TUCASA) jijini Dar es Salaam.

Vile vile, amewataka kuheshimu matumizi ya fedha za miradi, kwa kufanyia shughuli za ujenzi, na faida watakayoipata kuiwekeza na kutunza kampuni zao.

Aidha, ameielekeza Wizara ya Ujenzi kuweka mkakati wa kuwainua makandarasi nchini na kuhakikisha unatekelezwa ipasavyo kuanzia ngazi ya Wizara ya Ujenzi yenyewe pamoja na Wizara ya Fedha kisha kuendelea na mazungumzo na mabenki ili kuja na mpango mzuri wa kuwawezesha makandarasi kimtaji.

Amesema Ofisi ya Waziri Mkuu itaelekeza sekta zingine zikiwemo Nishati, Maji, Uchukuzi, kuhakikisha zina wabeba wakandarasi wazawa; pamoja na kuziwekea malengo ambayo kila mwaka kwenye mkutano wa makandarasi unapima utekelezaji wa malengo hayo.

Aidha, amewataka kuiga mfano kutoka Wizara ya Kilimo ya BBT, Wizara ya Ujenzi iwasaidie vijana kuanzisha makampuni na kuwapatia kazi ndogo ndogo ili kuwajengea uzoefu.

Dkt. Biteko pia amesisitiza kuwa, serikali imeendelea kuwachukulia hatua watumishi wote wa umma wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Dkt. Biteko amesema, katika mpango mkakati wa kukuza makandarasi wa ndani, kumewekwa kipangele cha kuhakikisha kuwa miradi yote inayotekelezwa kwa fedha za mikopo kutoka kwa wadau wa maendeleo kunatengwa asilimia isiyopungua 20 kwa ajili ya makandarasi wa ndani.

Dhamira ya Mhe Rais ni kuwajengea uwezo makandarasi wazawa na ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa Serikali pamoja na watumishi wa ngazi zote kuhahakikisha wanatekeleza agizo lake la kuwakuza na kuwajengea uwezo wakandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza miradi mikubwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza Wizara kupitia Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) imefanikiwa kuanzisha mpango mahsusi wa kuwashirikisha Mahandisi vijana kupitia miradi ya ujenzi ili kuwajengea uwezo zaidi katika miradi inayoendelea ya ujenzi ambapo hadi sasa, vijana waliopitia program ya SEAP ni 12,772 na wanao endelea nayo ni 3,317.

Amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara imetenga miradi ya Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 120 za lami ambazo zitashindanishwa kwa Makandarasi wa ndani pekee pamoja na kutoa kipaumbele kwa Makandarasi wanawake ambapo imetenga kilometa 20.

Naye, Mwenyekiti wa TUCASA, Samwel Marwa, ameiomba Serikali iwe mlezi kwa TUCASA ili kuwajengea uwezo wa kufanyakazi na kusimama wenyewe. Pia ameiomba Serikali kuendelea kupambana na rushwa ili kuifanya TUCASA kufanya kazi kwa weledi na kupata faida katika majukumu yao.

14 July 2024
TUCASA CONTRACTORS DAY 2024 - PUBLIC PROCUREMENT REGULATORY AUTHORITY (PPRA) "Bi.Winifrida Samba"


View: https://m.youtube.com/watch?v=k8jHlYQmhGI

In a panel discussion, Ms. Winifrida Samba from the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) elaborated on the significance of the Public Procurement Act of 2023, highlighting new policies implemented by PPRA.

She discussed the enhancement of accountability mechanisms within procurement processes to ensure transparency and responsibility for public officials and service providers.

By implementing an electronic bidding system, PPRA aims to foster greater competition and facilitate the participation of small and medium-sized enterprises (SMEs).Additionally, the evaluation and awarding process of contracts has been streamlined to guarantee fairness and efficiency.

Recognizing the vital role of SMEs in economic growth, PPRA has introduced policies to support their involvement in government procurement, ensuring they have equal access to opportunities.PPRA has established robust quality assurance measures to ensure public projects deliver maximum benefits while maintaining cost-effectiveness.

The authority has also embraced digital transformation by introducing systems that streamline processes and enhance transparency.

To support compliance, PPRA provides online resources and guidance, promoting accessibility and transparency. Training programs and workshops are conducted to enhance stakeholders' understanding of procurement laws and best practices, fostering sustainable strategies to ensure accountability in public services and procurement processes.

Rigorous systems for auditing and controlling public expenditure have been established to maintain efficiency and transparency.Ms. Samba also emphasized the importance of promoting local contractors and suppliers. PPRA has prioritized local contractors in government projects, aiming to boost the local economy.

To help local contractors meet project requirements, PPRA offers capacity-building programs that enhance their technical and managerial skills. Financial support mechanisms, such as favorable financing terms and guarantees, have been introduced to help local contractors secure funding for large-scale projects.

Furthermore, PPRA encourages joint ventures between local and foreign contractors to facilitate knowledge transfer and experience sharing. Robust monitoring and evaluation frameworks have been implemented to ensure local contractors adhere to project specifications and deliver quality work.

By involving local contractors in government projects, PPRA ensures that communities benefit directly from public spending, fostering a sense of ownership and responsibility.

These measures demonstrate PPRA’s commitment to supporting local contractors, fostering economic growth, and ensuring that public procurement contributes to the overall development of the country.For more detailed information on PPRA's initiatives and policies, please visit their official website: PPRA Website
 
Swali: Mtu mweusi wewe unaweza nini ikiwa hata Mwendokasi umekushinda?
Muulize swali hilo 'Chura Kiziwi'. Ni wajibu wake kuhakikisha hilo halitokei na maswali ya aina hiyo hiyo yaelekeze kwake. Jibu siyo kugawa kwa waarabu. Asimamie na kuhakikisha kwamba sisi wenyewe tunamudu kazi hiyo. Uwezo huo tunao sana, ni yeye tu ndiye anaye tukwamisha, na ndiyo maana hatutaki nyinyi waarabu mtumie njia hiyo kujiingza hapa kwetu na kutufanya watumwa wenu. Huyu anawafanyia kazi nyinyi, waarabu, ili mrudi hapa kwa kisingizio kwamba sisi hatuwezi. Huu ni upumbavu.
 
Kwanza elewa kuwa maisha ya mTanzania yeyote siyo duni, na ndiyo maana tutawaadabisha washenzi nyinyi mnaodhani maisha yetu ni ya duni.

Siku zote nilikuwa sijakuelewa nikuweke wapi, lakini leo kutokana na mstari huo wa juu nimetambua wewe hasa ni mtu wa aina gani hasa. Ni kundi lililoingia humu kupigania ajenda hii ya kuwadhalilisha waTanzania.

Kwa hiyo sasa nitakuchukulia hivyo, wewe ni kundi la wadhalilishaji wa waTanzania, kwa misingi ya uarabu wenu.

Kwa hiyo 'Chura Kiziwi' sasa hivi analipa fadhira kwa 'waarabu waliompa Nyerere mafuta'? Itakuwa akili zenu hazifanyi kazi sawasawa.
Huna hoja wewe nyumbu.

Maswali yangu hujajibu 😂😂😂😂😂

Mwisho unajikanyaga kanyaga mara useme Watanzania maskini mara useme sio maskini Wala duni,be consistent basi husomeki 😆😆

Mwisho nakwambia hivi, Uwekezaji utaendelea kama kawaida na Waarabu waje Kwa Wingi sana Kwa sababu ndio wenye pesa Kwa Sasa Duniani na wewe kama unazo kawekeze usilete Makelele yasiyokuwa na msaada ,hakuna anaetaka kelele zako.
 
Back
Top Bottom